Serikali kupitia waziri wake wa kilimo imesema acha soko liamue ,sawa. lakini isiwe kilimo tu acha soko liamue kwenye huduma zote

Serikali kupitia waziri wake wa kilimo imesema acha soko liamue ,sawa. lakini isiwe kilimo tu acha soko liamue kwenye huduma zote

ZALEMDA

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2017
Posts
1,956
Reaction score
2,225
Waziri wa kilimo amesema kuwa acha solo liamue kuhusu Bei ya mazao.Ni sawa kwa maana ya kutaka wakulima wajikwamue.ndiyo maana Leo hii hata vijijini debe moja ya mahindi imefikia 25000 shilling ya kitanzania.
Lakini mh waziri unasahau madhara tamko lako.unasahau kuwa Kuna sehemu nyengine Serikali imeweka Bei elekezi na mahala pengine kusababisha migogoro mikubwa Kati ya walaji na watoa huduma.

Unaposema kuwa acha soko liamue kwenye kilimo ,kupitia Serikali ambayo wewe ni waziri acha soko liamue kwenye bidha zote na huduma zote nchi.kwa maana :

1.Acha wenye mabasi waamue Bei zao.
2.acha wenye bajaji waamue Bei zao.
3.acha wenye vituo vya afya waamue Bei zao .NHIF isiwapangie gharama waendesha huduma za afya .

4.Acha wenye usafiri wa ndege wajipangie Bei zao .

5.acha wenye shule wajipangie Bei zao .

6.acha wauza pombe na vinywaji kwa ujumla wajipangie gharama zao.

7.acha wauza mbolea wajipangie Bei zao.

Lakini ili kumudu mfumuko wa bei unaojitokeza kulingana Bei sokoni ,Serikali ijipange kuongeza mishahara minono kwa wafanyakazi wake .

Na mwisho tutaona 2025 CCM inapitaje !! Leo ukiwa na 100,000 yani unanunua debe moja tu ya mchele ??? daah.


Jumapili njema Wana JF
 
Kwani walowengi sasa hivi wanapangiwa na nani QATAR AIRWAYS kwa mfano?
 
Wapi huko debe moja la mchele linauzwa laki moja (100,000) naomba majibu?
 
Kwanza usiseme serikali ijiandae kuongeza mshahara kwa sababu sio wote wafanyakazi. Asilimia kubwa ni wajasiriamali wakubwa na wadogo. Hawa nani atawaongezea mshahara.?

Jingine waziri kusema acha soko liamue, kwa mtu mzima utapata picha. Ni kwamba hata yeye yupo kwenye mtanziko na anakutana na upinzani kutoka juu linapokuja suala la mfumuko wa bei.

Hiyo sio kauli yake ila ni kama ameitoa kwa jazba tu. Kazi mojawapo ya serikali ni pamoja na kudhibiti mfumuko wa bei. Ila uongozi wa juu kwa sababu ulishafeli na wako bize kutafuta madaraka na si kutoa huduma, hawawezi kuliona hilo.
 
Soma vizuri siyo unaparamia.yani hutu kwetu debe moja ya mchele mzuri ni 60,000

Soma Aya yako ya mwisho ulichoandika. Mtu ukiwa na 100,000 unanunua debe moja la Mchele?

Ndio maana nauliza wapi debe ni shillingi laki moja?.
 
Serikali kupangia bei za mazao hakutopunguza bei ya chakula. Mfano mzuri angalia Cuba. Wana mfumuko wa bei za vyakula kubwa sana pamoja na kwamba serikali inaamua na kupangia bei za mazao. Serikali ya Cuba ilivyoingilia kilimo, wakulima wengi waliacha kazi hiyo matokeo yake Cuba inaagiza vyakula vingi na bei imepanda.

 
Ni sahihi kabisa kuacha nguvu ya soko kuchukuwa nafasi yake adhim, jambo ambalo lilikosekana kwa muda mrefu. Udhibiti wa soko la mazao ya kilimo limewadunisha wakulima, limewaacha maskini kabisa. Pia limeondoa ubunifu, tija na ujaririamali katika kilimo.

Tafiti zimeonesha kuwa katika vipindi fulani fulani ambapo kilimo kiliachwa huru (nguvu ya soko) hakika kilifanya vizuri. Chakula kiliongezeka na bei zikashuka lakini pia wakulima walipata pesa nyingi kwani uzalishaji uliendana na mahitaji ya soko kwa maana ya mienendo yake..

Nashangaa kwa nini imechukuwa muda mrefu hivi kwa upande wa serikali kufaham namna ambavyo kuingilia soko (market distortion) la kilimo ina madhara mengi kuliko faida...
Sasa waziri aje na mpango mkakati utaoweka bayana namna serikali itakoma kuingilia soko katika mazao ya kimkakati yakiwemo kahawa, chai, mkonge, pamba, korosho, nk.
 
Back
Top Bottom