Serikali Kushindana na JF?

Serikali Kushindana na JF?

  • Thread starter Thread starter MegaPyne
  • Start date Start date
Kutapatapa ndio inayoonekana hapa! Sasa watanzania wengine wasianzishe Forum basi tu kwa sababu JF imekuwa inasomwa sana? Ebo...Yaani hii inanikumbusha Uhuru-Mzalendo/Daily News era! Lazima JF ikubali competition if not opposition! Malumbano mengine humu hayana maslahi ni uzushi, personal attacks, na mazinga-ombwe! Toba... kukurupuka bila ya kuelewa kinacho-hojiwa! Yaani Kutapatapa Tu!
 
Mods take note and watch the trend...

Ngabu,
Huyo ni "intateina," version ya ze comedy online. Kwahiyo ondoa (wasi)2 sidhani kama ana mpango wa kuvurumisha matusi kama yule desperate housewife(vicious reckless savage). kwikwikwi i'm crossing my fingers.

Hivi umeona kuna mjinga kamuua SEAN TAYLOR number 21 wa Washington Redskins?? very sad, the guy was becoming a rising star in the league......nilikuwa napenda sana zile touchdown zake za ku-dive. Sean Taylor(1983-2007), RIP.
 
Yeah man hata mimi nimesikitika sana...
Can't wait for thursday...packers vs cowboys
 
Sura ya Kwanza,

Ingawa wengine wameamua kukudharau, mimi nitakuelimisha. Hakuna aliyechukia kuanzishwa kwa forum huko serikalini. watu walikuwa wanatoa taadhari tu kuwa watu wawe makini. Ndio maana utaona mwanakijiji na Kitila na Kada mpinzani wamejiunga.

Sasa kuhamaki kwako inatia shaka, au unatakaje?
 
FD, Nyani msijisumbue na huyo sura ya kwanza. Kazi yake ni spinning na huyu mtu ana ID kede kede, just see the structure of his writing.
 
Sura ya Kwanza,

Ingawa wengine wameamua kukudharau,
Heshima kitu cha bure...kula tano!
mimi nitakuelimisha.
Asante!
Hakuna aliyechukia kuanzishwa kwa forum huko serikalini. watu walikuwa wanatoa taadhari tu kuwa watu wawe makini. Ndio maana utaona mwanakijiji na Kitila na Kada mpinzani wamejiunga.
Na ndio midahalo invyoendelea! hii makini
Sasa kuhamaki kwako inatia shaka, au unatakaje?
Ambaye hajahamaki humu ahamaki na ye basi!
Mbivu hizi na mimi nataka!🙂
 
FD, Nyani msijisumbue na huyo sura ya kwanza. Kazi yake ni spinning na huyu mtu ana ID kede kede, just see the structure of his writing.
Na kizuzungu nimekipata kwa hili! Huna uadilifu huo wa uchunguzi! Kwani wewe hio ID ya Kinyau inamaainsha wewe kinyau au ndio Id kede kede? 😕 lete hoja hapa sio kuniongelea sura-ya-kwanza ! Hivi unajua wale wanaongelea watu saa zote wanaupungufu wa mawazo katika jamii?😉
 
Mie sioni shida ya watu kujiunga na hiyo Forum nyingine. ni vizuri watu wakaingia kule waone nini mawazo ya watu... unaangalia pia wengine wana hoja gani.. unajua mahali kukiwa na upinzani kunakuwa pazuri sana.. kunakuwa na changamoto.. kwa hiyo wanJF tusiogope
 
nadhani pia muwe waangalifu ambao mnajiunga kule kwani ni rahisi kuwa tracked and hakuna privacy kama JF kwani sijaona desclaimer ya administrators wao hawana statement ya kulinda ip za watu. Mnaokwenda kule sio mbaya mkajua hilo.

tangu nijiunge JF nimekua kiakili na sasa nategemea kuoa karibuni ingawa mnanibania michango yenu

..salaam!

..kuoa ni tendo linalohitaji barkha za mwenyaazi mungu!

..katu pesa haitoifanya ndoa yako kuwa bora!

..kama unanuia kweli,muoe huyo dada. isiwe ikawa unatafuta sababu za kumkimbia!
 
Kutapatapa ndio inayoonekana hapa! Sasa watanzania wengine wasianzishe Forum basi tu kwa sababu JF imekuwa inasomwa sana? Ebo...Yaani hii inanikumbusha Uhuru-Mzalendo/Daily News era! Lazima JF ikubali competition if not opposition! Malumbano mengine humu hayana maslahi ni uzushi, personal attacks, na mazinga-ombwe! Toba... kukurupuka bila ya kuelewa kinacho-hojiwa! Yaani Kutapatapa Tu!

..watu wana uhuru wa kusema,kuhoji na kutoa mawazo juu ya vitu!

..mtu asiye elewa ataona ni attacks and the likes!

..faida yake ni watu kufahamu nini kinachoendelea!

..kama umekasirika,susa sisi tutakula!
 
Hiyo Kweli kabisa Mwanakijiji hata mimi nimeshangaa Zitto kuwekwa kama Category nadhani labda hawajapata mtu anayejua ku-set up Forums vizuri au labda wanasubiri hadi Kikwete aende tena Scandinavia kuomba watalam wa ku-set up Forums.

Geeque.......

taratibu kaka,yaani duh unatudharau ndugu zako,wa-tz wenzako licha ya kuwa tumekula shule na tumo serikalini hatuwezi kufanya kazi hiyo mpaka tukachukue mtaalamu skandanavia?TUOMBE RADHI NDUGU TENA KWA MAANDISHI MAKUBWA.
 
nilikuwa sina mood ya kucheka.. lakini hii imenivunja mbavu..big ups geeque..

mkjj........... and ALL JF MEMBERS....

samahani leo nataka nikutolee UVIVU kidogo,unajua kawaida ya wanaume huwa hamgombani kwa maneno,wanaume mnashikana mashati na kupigana and then hapo baada ya mmoja kupigwa basi kila mmoja atamuwekea HESHIMA MWEnzeke.

jamani tanzania ni nchi yetu sote,mie wewe na wengine,hivi unaona unaona ufakhari kuona wadogo zetu kule kijijini hawaendi shule,ubadhirifu unaofanyika na mengine mengi.leo m-tz anashindwa kula hata mlo 3 kwa siku kutokana na umaskini.tumeshakosoa sana serikali yetu,naamini wameshasikia jamani mie naona ilobakia kuanzia sasa tuwe tunawapa ushauri jamani nini cha kufanya na sio kila siku RA,EL etc jamani yatosha hebu kuanzia sasa tuwe tunawapa mawazo serikali yetu na viongozi wetu jamani.

sawa kila mmoja ni mpenziwa chama mbali mbali,lakini tujue serikali iliopo madarakani ni ya CCM kama kuna jambo viongozi wetu wamekosea basi tuwarekebisha mie naamini na wao wale ni binadamu wanasikia na kuona haina haja tena kuwatolea kashfa zao MUDA UMEFIKA WA KUWAAMBIA NINI WAFANYE.

HIVI ndugu zangu mfano kama suala la madini alosema ZK hivi tunaona raha tukiona wengine wanakula aislimia kubwa na sisi wenye nchi tunaumia?tutoeni mawazo jinsi gani ya kurekebisha,suala la umeme TANESCO tutoeni mawazo jinsi gani shirika linaweza kupata vyanzo ya incomes,migogoro ya ardhi,matatizo ya maji,tatizo la barabara na mengi mengineo.

tuchukulie hilo suala la forum kama ya serikali,kweli kama tuna uchungu na nchi kwa nini msitupe mawazo jamani na sisi tukiwa kama ma-IT technicians wa serikali nini tufanye ili kitu chetu kionekane makini na kizuri?msiwe mnatuponda na ktusagia jamani,turekebisheni ndio kwanza tumerudi shule fresh kabisa hatuna experienced bado ya mambo,kwa maana hiyo wenzetu mshakuwa exposed na mengi tupeni HINTS nini tufanye na sisi taifa letu liendelee ktk nyanja za IT.

JAMANI MUDA UMEFIKA WA KUIKOSOA SERIKALI YETU NA SIO KUIKOSOA TU BALI KUJA NA MAWAZO YA KUPELEKA TAIFA LETU MBELE.

NATANGULIZA SAMAHANI ZA DHATI KAMA KUNA MEMBERS YOYOTE NILOM-KWAZA

naomba Kutoa HOJA.
 
Msanii Ile Forum Ni Ya Phpbb Ile Haiwezi Kuhifadhi Ip Address Mpaka Mtu Anawe Ana Monitor Moja Kwa Moja Yaani Ukiwa Online Ndio Aweze Kutrace Lakini Majukumu Mengine Yote Yanaihusu Phpbb Na Kama Ukiregister Unafuata Terms Za Phpbb Na Sio Daily News

Kwahiyo Usiwe Na Wasi Wasi Sana

Ahsante
 
Geeque.......

taratibu kaka,yaani duh unatudharau ndugu zako,wa-tz wenzako licha ya kuwa tumekula shule na tumo serikalini hatuwezi kufanya kazi hiyo mpaka tukachukue mtaalamu skandanavia?TUOMBE RADHI NDUGU TENA KWA MAANDISHI MAKUBWA.

..shule inawezekana mmekula mbona IT ya serikali ni zero kabisa na mnafabnya kazi gani maana file bado ni mtindo mmoja,inaonekana hamfanyi kazi yenu na mnahitaji msaada...angalieni Kenya sasa update kwenye nomination za candidates next election ambazo zinaendelea ziko updated in real time,nyie vipi hayo mavumbi ya mafile hayawasumbui? JK hajui hayo na wala simlaumu,nyie mnaokula kodi zetu ndio mnatakiwa kudemand na kubadilisha kila kitu la sivyo tutaendelea kuwalipa hao scandinavian kwa kazi ndogo ndogo mpaka mtie akili
 
Koba

Ahsante Kwa Comment Zako

Unatakiwa Ujue Kwamba It Imegawanyika Makundi Mengi Sana Mfano Mimi Ni Mtu Wa Ufundi , Usimamizi , Usalama Na Mipango Katika It , Kuna Wengine Ni Katika Utengenezaji Wa Programu , Michoro , Video Na Kadhalika Kwahiyo Kazi Zinaendelea Kama Kawaida .

Hizo Kazi Za Serikali Kama Webzao Na Kadhalika , Kile Serikalini Wana Webmaster Wao Na Wataalamu Wao Wa Mambo Ya Web Katika Hizo Wizara Sehemu Nyingi Nimeona Kwahiyo Kama Wamepewa Jukumu Hilo Na Wakashindwa Kulitengeneza Kikamilifu Basi Wahukumu Hao Na Sio Wote Kama Sisi Tuliokuwa Katika Sekta Binafsi .

Pia Sio Kila Kitu Ni Raisi Au Chama Kinahusika Ukisema Hivyo Utakuwa Unakosea Heshima Taifa Lote La Watanzania Kwa Ujumla Tunaomba Unapotoa Comments Zako Siku Nyingine Sio Wewe Peke Yako Kama Ni Za Kitaalamu Kasome Au Tafuta Habari Zaidi Ili Uje Kutoa Comments

Mwisho Kabisa Katika Tekinologia Hatupendi Siasa , Uwongo Na Majungu Haya Ni Mambo Ya Kweli
 
Shy mbona sijasema chochote kuhusu sekta binafsi na wala sijaingiza siasa hapo,lakini bila spin yeyote ukweli ni kwamba IT katika serikali wako nyuma sana na bado wanatumia paper file kwa kazi zao nyingi za kila siku na hata sekta binafsi kubali tuu mambo ni bado sana hapo TZ!
 
Sina hakika kama watahili ukweli wa moja kwa moja maana hawa kazi yao ni ku twist issues.Wacha tuone maana wanalilia wembe .Kama ni habarfi wanazitaka katika jamvi lao tutawapa tu .
 
Back
Top Bottom