Serikali kusomesha chuo kikuu wanafunzi watakaofanya vizuri masomo ya sayansi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda (Mb) amesema katika bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/23 Wizara imetenga fedha kwa ajili ya kutoa ufadhili wa elimu ya juu (scholarships) kwa wanafunzi watakaofanya vizuri katika masomo ya Sayansi.

Waziri Mkenda amesema hayo Jijini Dodoma alipokutana na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ambapo amesema ufadhili huo utatolewa kwa asilimia mia moja kwa wanafunzi wachache na watasomeshwa ndani na nje ya nchi.

Amesema lengo la Serikali ni kuongeza fursa za upatikanaji wa elimu ya juu na kuhamasisha watoto wengi kupenda kusoma masomo ya Sayansi.

Pia ametoa agizo kwa Bodi hiyo kujipanga ili ifikapo mwaka wa fedha 2023/24 kuanza kutoa mikopo kwa wanafunzi watakaosoma masomo ya Ufundi na ujuzi kwa ngazi ya Diploma.

"Kilio cha watu wengi kwa sasa ni ajira na sehemu ambayo ajira ni rahisi zaidi ni kwenye ufundi na ujuzi hivyo ni vizuri kujiandaa. Hili tunalisema mapema ili wanafunzi watakaoomba katika kipindi hicho wajue pia katika vyuo vya ufundi kuna fursa ya kupata mikopo," amesema Prof. Mkenda.

Mhe. Mkenda ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza bajeti ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kutoka bilioni 464 hadi kufikia bilioni 570, kuondoa adhabu ya asilimia 10 ya wanaochelewa kurejesha mikopo na kufuta asilimia 6 ya kulinda thamani.

Aidha Waziri Mkenda ametoa wito kwa wanafunzi wanaoomba mikopo ya elimu juu kutoa taarifa zote zinazotakiwa kwa ukamilifu na kwa wakati ili waweze kupata mikopo hiyo bila changamoto.

"Mkopo unatolewa kulingana na taarifa anazotoa mwombaji, ukitoa taarifa ambazo sio kamili kunakuwa na changamoto hivyo toeni taarifa kamili na Bodi itaendelea kuchakata taarifa hizo ili wanaostahili kupata mikopo wapate," amefafanua Waziri Mkenda.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Eliamani Sedoyeka amesema kwa sasa Wizara imejipanga kuhakikisha Watanzania wengi wanapata fursa ya kusoma elimu ya juu kwa kuwezesha kufanya hivyo kulingana na malengo ya Taifa letu.

"Wote tunafahamu juhudi ambazo Serikali imeweka kwenye elimu msingi ambazo zimepelekea kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne na sita na wakiwa na ubora na kupelekea kuwa na vigezo vya kuendelea na elimu katika ngazi inayofuata hivyo kupekelea kuhitajika fedha kwa ajili ya kusomesha," amesema Prof. Sedoyeka.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Prof. Hamisi Dihenga amesema anatambua kuwa wana dhamana kubwa ya kuhakikisha utaratibu wa kutoa mikopo unaeleweka kwa Watanzania wote na unawasaidia wale wanaostahili kupata mikopo na kuahidi kushirikiana na Menejimenti ya Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu kuhakikisha hilo linafanikiwa.
IMG-20220430-WA0028.jpg
IMG-20220430-WA0029.jpg
IMG-20220430-WA0030.jpg
IMG-20220430-WA0034.jpg
IMG-20220430-WA0027.jpg
IMG-20220430-WA0033.jpg
IMG-20220430-WA0026.jpg
IMG-20220430-WA0031.jpg
IMG-20220430-WA0032.jpg
 
Wizara imepata mtu sahihi tofauti na yule mama
Hilo suala lipo muda mrefu na watu kibao wamekuwa wakipewa scholarships.

Binafsi sioni jipya, labda kama wameongeza budget.

Mfano, kwa waliopata mwaka Jana 👇👇👇

Mbona hii ni program ya muda mrefu
Waziri yuko sahihi

Magufuli katika vitu alichemka mimi kama mwana CCM ni hicho. Kikwete alikuwa akitoa mikopo kwa asilimia sehemu kubwa kwa wasoma digrii za sayansi ili ipatikane Tanzania ya viwanda na wanasayansi

Magufuli akashauriwa vibaya na wajinga fulani kuwa kigezo cha kuolewa mikopo kiangalie tu shule ulizosoma mfano msingi shule ya Serikali,sekondari ya kata form four na form six Serikali basi wewe unastahili mkopo unatoka familia maskini yenye umaskini mkubwa hata kama unaenda kusoma digrii ya vichekesho ambayo mwisho wa siku Haina ajira ndani na nje ya nchi!!

Kikwete alilenga fani za sayansi zenye uhakika wa kuajiri au kuajiriwa ndani na nje ya nchi ili mikopo ilipike mwisho wa siku
Magufuli akavuruga kila kitu na humu jamii forums zimo post zangu nilizopinga

Rwanda Haina Madini nk wameamua kuwekeza kwa rare professions za sayansi

Wanasomesha sana kila rare profession na Proffession za masomo ya digrii za sayansi wanasomesha bure ndani na nje na mtu akimaliza Serikali inalipia masomo yake awe internationally certified na international certification body sio local ili aweza kuwa rahisi kuajirika popote duniani sababu ans international certification ya bodies za kimataifa

Waziri yuko sahihi.Wafanya vizuri Serikali itafute scholarship nje nchi zenye elimu Bora waende huko na kama scholarship hazipo Serikali ilipie
 
Umesoma hiyo makala?

Ukimaliza soma na hii 👇👇👇

Wazo zuri, msije tu fanya kichaka cha kupeleka nje watoto wenu. Ufaulu mzuri ni kuanzia wapi hadi wapi? Combinations gani zinahusika?
 
Waziri yuko sahihi

Magufuli katika vitu alichemka mimi kama mwana CCM ni hicho. Kikwete alikuwa akitoa mikopo kwa asilimia sehemu kubwa kwa wasoma digrii za sayansi ili ipatikane Tanzania ya viwanda na wanasayansi

Magufuli akashauriwa vibaya na wajinga fulani kuwa kigezo cha kuolewa mikopo kiangalie tu shule ulizosoma mfano msingi shule ya Serikali,sekondari ya kata form four na form six Serikali basi wewe unastahili mkopo unatoka familia maskini yenye umaskini mkubwa hata kama unaenda kusoma digrii ya vichekesho ambayo mwisho wa siku Haina ajira ndani na nje ya nchi!!

Kikwete alilenga fani za sayansi zenye uhakika wa kuajiri au kuajiriwa ndani na nje ya nchi ili mikopo ilipike mwisho wa siku
Magufuli akavuruga kila kitu na humu jamii forums zimo post zangu nilizopinga

Rwanda Haina Madini nk wameamua kuwekeza kwa rare professions za sayansi

Wanasomesha sana kila rare profession na Proffession za masomo ya digrii za sayansi wanasomesha bure ndani na nje na mtu akimaliza Serikali inalipia masomo yake awe internationally certified na international certification body sio local ili aweza kuwa rahisi kuajirika popote duniani sababu ans international certification ya bodies za kimataifa

Waziri yuko sahihi.Wafanya vizuri Serikali itafute scholarship nje nchi zenye elimu Bora waende huko na kama scholarship hazipo Serikali ilipie
Yehodaya, haya maneno yanatoka kwako? Wengi tunakuona blni mtu wa kushangilia chochote cha CCM au kutoka kwa mwanaCCM, kiwe kizuri au kibaya.

Kati ya mambo yanayonikwaza sana JF ni tabia ya watu fulani kushangilia kika kitu alimradi kimefanywa na mtu fulani, au kupinga kila kitu kwa sababu tu kimefanywa na mtu fulani, jambo ambalo ni baya, na tunaifanya JF kuwa jukwa la kupiga soga na ushabiki badala ya kuwa JF la watu kujadili mambo ya msingi.

Mambo ya msingi ni lazima tuungane kama watu wa Taifa moja.

Kwenye hili la Prof. Mkenda naunga mkono 100%.

Samia kufuta adhabu ya kuchelewesha ulipaji mkopo na riba kwa mikopo ya wanachuo, naunga mkono 100%.
Lile la Jakaya Kikwete kupeleka wanachuo wa kwenda kufundisha masomo ya Sayansi UDOM, ulikuwa ni ubunifu mzuri wa kuweza kupata walimu wazuri,naunga mkono 100%. Magufuli kufuta huo utaratibu, ni uthibitisho wa hulka ya marehemu kutumia zaidi nguvu kuliko akili. Utaratibu ule urudishwe mara moja.

Sijawahi kuwa shabiki wa Jakaya, wala Samia, lakini kuna mambo mengi mazuri wanafanya, sasa nisiwapongeze kwa vile tu siyo shabiki wao?

Marehemu, kwa ujumla, brutality na primitivity inamfanya awe very unpopular. Na bahati mbaya kadiri miaka itakavyoenda,atasenwa sana kwa mabaya kuliko mazuri.

Tupiganie katiba mpya ili tukipata viongozi wa ajabu, tuweze kuwadhibiti.
 
Aidha Waziri Mkenda ametoa wito kwa wanafunzi wanaoomba mikopo ya elimu juu kutoa taarifa zote zinazotakiwa kwa ukamilifu na kwa wakati ili waweze kupata mikopo hiyo bila changamoto.

"Mkopo unatolewa kulingana na taarifa anazotoa mwombaji, ukitoa taarifa ambazo sio kamili kunakuwa na changamoto hivyo toeni taarifa kamili na Bodi itaendelea kuchakata taarifa hizo ili wanaostahili kupata mikopo wapate," amefafanua Waziri Mkenda.
Mikopo isiwe na masherti ya hivyo, hii ndiyo inasababisha urasimu.
 
tunahangaika sana aisee.....mpaka leo hii bado hatujui njia ya kurudia baada ya kupotea..
 
Inasomesha wanasayansi au wana historia ya SAYANSI??
 
Wanaongelea scholarships na wala siyo mikopo. Hivyo ni vitu viwili tofauti.

Back
Top Bottom