Inashangaza sana ...tena sana tu; Kabla ya zoezi la sensa tuliambiwa Serikali imetenga bajeti ya sensa, iwe kwa kupewa au bajeti kuu ilifanyika. Pamoja na mambo mengi kwenye sensa hiyo, anwani za makazi pia zilijumuishwa, tukaahidiwa kuwekewa vibao vya mitaa sambamba na namba za nyumba. Waziri mwenye dhamana aliruka na helikopta kukagua zoezi zima akiwa angani..... Ukweli ni kuwa hadi leo iko mitaa na vitongoji haina hivyo vibao vya mitaa, wala namba za nyumba, kisa ... hawana bajeti wezeshi kugharamia usimikaji wa vibao ambavyo vina bei ya shilling 7000 kwa kila nyumba na shilling 75000 kwa kila kibao cha mtaa, viwili ni sawa na 150000.
Leo nimeona helikopta nyingine ya jeshi ikiruka kwenye ile shughuli ya kutangaza matokeo ya sensa, ikipeperusha bendera ya taifa ya ujumbe wa sensa. Ni mafuta kiasi gani yametumika kuzungusha bendera ya taifa kwenye tukio hilo? Je pesa hiyo kwa nini isingetumika kulipia vibao vya mitaa vilivyododa kwenye ofisi za Serikali za mitaa kwa wananchi kukosa pesa ya kuvilipia?
Hali kiuchumi ni mbaya na huenda ikawa mbaya zaidi siku zijazo kwa hali ilivyokuwa tete Dunia nzima. Najiuliza tu; ni kwa nini shilling millioni 480 zitumike kwenye hafla ambayo ingeweza kutangazwa tu redioni au kwenye luninga?.... Haya ni matumizi mabaya ya pesa za wananchi...