Serikali kutolipa mishahara watumishi kwa kisingizio cha kutojaza majukumu yao kwenye mfumo wa ESS ni unyang'anyi usiotumia Silaha

Watumishi wa serikali ndiyo serikali yenyewe. Sasa itajivumiliaje? Hapa kilichotokea ni serikali imeamua kujiwajibisha. BTW. Mfanye mjaze hizo fomu wandugu. Nimeshangaa kibanda changu biashara imedoda kumbe kuna watu zaidi ya laki hawajachukua mpunga!!
 
CCM imeipenda wenyewe Wacha iwanyooshe na Bi Mkubwa anaupiga mwingi
 
Kama mtu siyo mtumishi anaweza kudhani umeandika kitu cha maana kweli kweli!

Sikieni enyi msiokosa cha kusema; serikali haijakurupuka katika jambo hili na ndiyo maana watumishi walipewa muda wa kutosha kushughulikia mambo yote kwenye mfumo. Hata baada ya tarehe husika kufika ilipokuwa bado wengine hawajakamilisha watumishi waliongezwa muda tena na tena ili kuhakikisha tu haachwi mtu katika zoezi lile. Kukazuka matapeli sana wakiwatisha watumishi kuwatoa kwenye ajira kwa kutokujaza huo mfumo LAKINI SERIKALI ILIWATOA HOFU WATUMISHI NA KUWAONGEZA MUDA WA KUTOSHA PAMOJA NA NJIA NZURI ZA KUWASILIANA IN CASE OF CHANGAMOTO YOYOTE

Sasa ikitokea kuna wakurugenzi sijui wakina nani wamefanyiwa hicho usemacho (kama ni kweli) basi ni sahihi kabisa tena mimi naona ilitakiwa yazuiliwe mishahara matumishi yenyewe yaliyofanya uzembe na wala siyo mwajiri au afisa

Imagine kwa mfano Elimu, (naichukulia mfano kwakuwa ndiyo nina uzoefu nayo na ndio kada yenye idadi kubwa) watu wamepewa vishikwambi, kukaundwa magroup ya WhatsApp, kukaundwa timu mbalimbali za utatuzi wa maswala hayo ya kimfumo, kukatengwa siku maalum za kukutana watumishi wote wenye changamoto kwa ajili ya kulimaliza jambo hili kwa pamoja. Wataalamu wote wa Halmashauri (Maafisa Utumishi, Wakuu wa Idara, watu wa IT na TEHAMA, nk) wanakwepo hapo kuhakikisha changamoto zote wanasolve

Halafu baada ya hatua zote hizo linatokea lijitu lizembe liseme limeonewa kweli!
 
Wengi hawajui wajibu wao, kwa hili serikali nipo nayo, wajaze kama hawataki kweli wakatwe mishahara yao
 
 
Timiza wajibu
 
Acha mbwembwe, jaza kazi zako, huu mfumo ni katika kuondoa, watumishi hewa!
Kama MTU hajajaza, automatic salary haiingii, system inafsnya kazi
 
Mkuu kuna ambao wanakimbilia kustaafu, hata kufungua smartphone hawajui, wengine wako chaka huko mtandao haupo tu akitaka kujaza lazima aende mjini.
Sio hivyo tu kuna mmoja imebidi niwe namsaidia kujaza na yupo mjini tu.
 
Una comment upuuzi tu tena hata ww ungekuwa mtumishi huenda usinge lipwa mshahara ww.
 
Sio swala kukwepa, mtu yupo kijijini huko hakuna mtandao anajazaje sasa ? Na hapo ndipo kituo cha kazi ??

Haya kujaza kunatakiwa kila siku ulichofanya hiyo pesa ya bando na gharama ziko hivi unafanyaje sasa ?
Kuna waropokaji tu humu kisa hawapo ajirani, hawa hawawezi elewa chochote
 
Una comment upuuzi tu tena hata ww ungekuwa mtumishi huenda usinge lipwa mshahara ww.
Acha uvivu na kupenda kulaumu. Jaza form na uwe una update kazi uzifanyazo fullstop. Hivyo tu yaani

Acha kufanya kazi kimazoea. Kila siku ruhusa hakuna productivity yoyote. We nitukane tu ila mwisho wa siku jifunze kufanya kazi na ku produce results. Usitafute excuses
 
Acha ubwege ww mm na update kila siku, na sijawahi kosa mshahara ila kunawatu hawajui hayo matumizi la laptop ww unahisi kila mtu ana ujuzi huo? Kuna sehemu hamna hata network ya kumpigia mtu sim. Msiwe mnakurupuka ku comment upuuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…