Serikali kutumia kigezo cha kujitolea kuajiri Walimu siyo haki

Serikali kutumia kigezo cha kujitolea kuajiri Walimu siyo haki

Hii Serikali wasanii tu. Mke wangu ni Mwalimu wa Physics alikuwa anajitolea kufundisha shule moja kwenye Municipal moja,ajira zilivyotangazwa headmaster wa hiyo secondary akamuandikia recommandation kwamba anamuhitaji na ikipitishwa na DED. Ajira zilipotoka akapangiwa mkoa wa mbali huko yaan 2000km kutoka tulipo tena vijijini hata network ni shida. Kuna classmate wangu yupo TAMISEMI kanihangaikia ili abadilishiwe kashindwa anaambiwa ni maagizo kutoka juu hakuna kubadilisha. Hiyo ilikuwa 2017.
Mkuu katika ili wewe sio mtu mwema...kwahiyo unataka vijana wanaokaa huko mikoani wasifundishwe Fizikia
 
Jamani! Suala la wakuu wa shule kutuma majina ya walimu wanaojitolea ofisi ya Rais-tamisemi kwa lengo la kupatiwa ajira ni ubaguzi na siyo haki kabisa.

Kama mtakumbuka baada ya ajira kuwa ngumu! Serikali ilitoa tamko vijana kutafuta fursa kwenye mashirika na shule binafsi pia serikali ilisisitiza vijana kujiajiri kwa lengo la kujikwamua kimaisha kwa kipindi chote wakisubiria fursa za ajira zitakapotangazwa.

Kweli! Baada ya matamko hayo vijana wengi walianza kutafuta fursa kila mahali! Kwenye mashirika, shule binafsi, kufungua mabanda ya chips, kulima bustani etc.

Lakini! Leo katika hali ya kushangaza serikali inapita kuchukua majina ya walimu wanaojitolea shule za serikali ili wapatiwe ajira za moja kwa moja!

Kinacho nisikitisha ni namna zoezi hili lilivyofanywa! Mfano mimi nilipomaliza chuo 2017 nilienda kujitolea sekondari fulani hapa jijini Dar! Lakini mazingira niliyokutana nayo ikiwemo kunyanyaswa kingono na walimu waajiriwa na gharama za nauli 800 kwa siku! kusema kweli ilifikia hatua nikashindwa kuendelea!

Mwaka huu mwezi wa pili! Wilaya ya temeke ilipotanga uhitaji wa walimu wa kujitolea nilienda kwa bahati mbaya huko nako nilipofika nikaambiwa wameshajaa hawahitaji tena!

Kwahiyo! Serikali inapotaka walimu waliojitolea ndio waajiriwe tu naona kabisa haitutendei haki ni bora ajira ziwe kwa wote ila wakujitolea wapewe kipaumbele kwanza!

Kitu kingine! Kwenye utumaji majina si kweli majina yote yaliyotumwa walikuwa wakijitolea! Wengine wameandikwa baada ya kusikia ofisi ya Rais- tamisemi inayahitaji. Yaani mkuu wa shule anamwandika ndugu yake kisha anamwambia awe anajisogeza sogeza hapo shuleni ili siku team ya tamisemi ikipita kufanya ukaguzi imkute!

Sisi ambao hatujuani na hatukuwa na hela za kuwaonga wakuu wa shule watume majina yetu naona giza tuturu kwa upande wetu! naomba serikali ilitazame upya suala la kujitolea kwa mapana zaidi ili na sisi wanyonge tupate fursa ya ajira!
wapo sawa! popote unapotuma maombi ya kazi wanataka uzoefu na utaje huo uzoefu ni muda gani!! hawa waliokuwa wanajitolea CV zao ni tofauti na wale waliokuwa Majumbani wanaangalia Series za Kituruki😁
 
Back
Top Bottom