japotenda
JF-Expert Member
- Jan 9, 2020
- 203
- 159
kwel kbsa[emoji2][emoji2][emoji2] ila wewe unachangamsha kijiwe tu
kwel kbsa[emoji2][emoji2][emoji2] ila wewe unachangamsha kijiwe tu
kwel kbsa
lakini watu wana dhana hyo hadi leoKubeba failures ilikuwa ni mkakati wa kujaza walimu wa shule za msingi ili kufidia deficiency wa walimu nchini; sera ilipita mwaka 2006 ikawa na utekelezaji mwaka 2007
Nazungumzia gharama za kujikimu kila siku kama chakula na maradhi nani wa kutuhudimia tukiwa twajitolea huko vijijini?Mkuu kwani huko vijijini hakuna watu wanao ishi? Maisha ni wewe uyakavyo amua yawe tu
Hata ktk waliopata div one kwenye ushindani kuna waliofeli: aliyepata one ya points 5,6 na 7 amefeli ukimlinganisha na mwenye one ya points 3 na 4. Sasa wewe unaongelea wenye two za points10 !!!we ndo unadanganya nenda kaangalie majina wanayoyojiunga pale UDSM mwenye alama ndogo ana daraja la 2.10 hyo ilikuwa 2012, vitu vingine usiongee bila ya kuwa na uhakika ni aibu
Hata ktk waliopata div one kwenye ushindani kuna waliofeli: aliyepata one ya points 5,6 na 7 amefeli ukimlinganisha na mwenye one ya points 3 na 4. Sasa wewe unaongelea wenye two za points10 !!!
Acha kudanganya umma
Mwaka 2000 niliingia UDSM kusoma Education nikiwa na Div 1 ya Point 7 kutoka kidato cha 6. Kwahiyo usibishe kuwa kuna watu wana ufaulu wa madaraja hayo wanaingia kusoma ualimu.
Dogo umesema kweli waliojitolea Ni wachache hivyo wasitumie hicho kigezo kupenyeza watu wao kuweni waangalifu Sana na hao maccm no noma sanaJamani! Suala la wakuu wa shule kutuma majina ya walimu wanaojitolea ofisi ya Rais-tamisemi kwa lengo la kupatiwa ajira ni ubaguzi na siyo haki kabisa.
Kama mtakumbuka baada ya ajira kuwa ngumu! Serikali ilitoa tamko vijana kutafuta fursa kwenye mashirika na shule binafsi pia serikali ilisisitiza vijana kujiajiri kwa lengo la kujikwamua kimaisha kwa kipindi chote wakisubiria fursa za ajira zitakapotangazwa.
Kweli! Baada ya matamko hayo vijana wengi walianza kutafuta fursa kila mahali! Kwenye mashirika, shule binafsi, kufungua mabanda ya chips, kulima bustani etc.
Lakini! Leo katika hali ya kushangaza serikali inapita kuchukua majina ya walimu wanaojitolea shule za serikali ili wapatiwe ajira za moja kwa moja!
Kinacho nisikitisha ni namna zoezi hili lilivyofanywa! Mfano mimi nilipomaliza chuo 2017 nilienda kujitolea sekondari fulani hapa jijini Dar! Lakini mazingira niliyokutana nayo ikiwemo kunyanyaswa kingono na walimu waajiriwa na gharama za nauli 800 kwa siku! kusema kweli ilifikia hatua nikashindwa kuendelea!
Mwaka huu mwezi wa pili! Wilaya ya temeke ilipotanga uhitaji wa walimu wa kujitolea nilienda kwa bahati mbaya huko nako nilipofika nikaambiwa wameshajaa hawahitaji tena!
Kwahiyo! Serikali inapotaka walimu waliojitolea ndio waajiriwe tu naona kabisa haitutendei haki ni bora ajira ziwe kwa wote ila wakujitolea wapewe kipaumbele kwanza!
Kitu kingine! Kwenye utumaji majina si kweli majina yote yaliyotumwa walikuwa wakijitolea! Wengine wameandikwa baada ya kusikia ofisi ya Rais- tamisemi inayahitaji. Yaani mkuu wa shule anamwandika ndugu yake kisha anamwambia awe anajisogeza sogeza hapo shuleni ili siku team ya tamisemi ikipita kufanya ukaguzi imkute!
Sisi ambao hatujuani na hatukuwa na hela za kuwaonga wakuu wa shule watume majina yetu naona giza tuturu kwa upande wetu! naomba serikali ilitazame upya suala la kujitolea kwa mapana zaidi ili na sisi wanyonge tupate fursa ya ajira!
Tuweke dau uje nikuoneshe na ukague na vyeti. Ukishindw unanipa hela nikishindwa nakulipa usumbufu.Acha kudanganya umma
Kumbe kuna watu hadi wakati huu wana mentality kwamba waliosomea ualimu wote walifeli, kweli kama taifa tupo kwenye mkwamo.Wananchi waliopo huko wanaishi vipi? Yaani wewe na kashahada kako ka ualimu ushajiona ni mtu maalumu Sana? Ili uende ualimu kwa vyovyote vile ulifeli. Sasa failure unaanzaje kuleta tambo na nyodo?
Una tatizo kubwa la ufahamu i.e kusoma kitu kilichoandikwa na kuweza kufahamu ujumbe uliomo kwenye kitu hicho.Hata ktk waliopata div one kwenye ushindani kuna waliofeli: aliyepata one ya points 5,6 na 7 amefeli ukimlinganisha na mwenye one ya points 3 na 4. Sasa wewe unaongelea wenye two za points10 !!!
Sijui kama zatoka lini! Ukweli anaujua jaffo!Hizo ajira zinatoka lini ?
Hii Serikali wasanii tu. Mke wangu ni Mwalimu wa Physics alikuwa anajitolea kufundisha shule moja kwenye Municipal moja,ajira zilivyotangazwa headmaster wa hiyo secondary akamuandikia recommandation kwamba anamuhitaji na ikipitishwa na DED. Ajira zilipotoka akapangiwa mkoa wa mbali huko yaan 2000km kutoka tulipo tena vijijini hata network ni shida. Kuna classmate wangu yupo TAMISEMI kanihangaikia ili abadilishiwe kashindwa anaambiwa ni maagizo kutoka juu hakuna kubadilisha. Hiyo ilikuwa 2017.
Umenena! BarikiwaKwa nini nijitolee wakati nilifaulu mtihani?
Kwa nini unipime uzalendo kwa kunilazimisha nijitolee wakati hujui wapi napata chakula, mavazi, usafiri na malazi?
Ni kwa nini nijitolee katika mazingira yanayokifanya nionekane mtumwa?
Mwisho, kama ajira zipo watu wapewe na kama hazipo tamko litoke ili tuzoee na tuache kusumbuana.