Serikali kutumia kigezo cha kujitolea kuajiri Walimu siyo haki

Serikali kutumia kigezo cha kujitolea kuajiri Walimu siyo haki

Hii research yako ya ajabu uliifanyia wapi?!
Ndivyo ilivyo ktk nchi hii tangu tangu enzi na enzi. Hakuna mwanafunzi mwenye ufaulu wa flying colors anaweza kusomea ualimu. Hayupo!
 
Nyie mnaosema aende tu huko vijijini nyie mpo huko?

Sehemu ambayo haina maji, zahanati, unakuta kuna kaduka cha dawa kameandikwa jina tu, lakini ndani hakuna hata Aspirin!, unaweza vipi kuishi eneo kama hilo ukiwa na proper mind ili uweze kwenda kufundisha watoto darasani wakuelewe?

Kwanini hao watu wanaowaunganisha ndugu zao maeneo ya mijini wasiwapeleke na huko vijijini, kwani nao si wana tatizo la ajira, na ajira zipo huko mashambani kama mnavyosema, basi nao wapelekwe huko.

Vinginevyo mnaonekana selfish, mnamsukimia mwenzenu kijijini wakati nyie mko mijini, always talk is very cheap for the blind.

Ni bora mtu ujipange ufanye hata biashara, kama ni kilimo ujue mazao gani yana market eneo ulilopo, tembea kwenye mitandao kama huku JF kuna majukwaa kama la kilimo, biashara soma huko utapata idea zitakazo kuwezesha kupiga hatua kwenda mbele.

Kama suala ni mtaji unaweza tafuta watu muungane kikundi mchange pesa mfanye kitu, hizi ajira nyingi ni maumivu tu, mshahara mdogo halafu unapoteza muda mwingi, au unaweza kuifanya hiyo kazi ya ualimu kwa muda fulani ukishapata mtaji then wachana na hiyo kazi kafanye kitu kingine.
Mwambie apige chini kazi.
 
Acha wenzako waliovumilia wapate ajira, unataka wakose au wasiajiriwe kwasababu wewe hukuweza kujitolea?! Hukuna ajira acha watakaopata wapate, wewe utapata zingine zijazo.
 
Kama ndivyo, binafsi naona itakuwa sahihi, kwa sababu, vijana wa siku hizi tumekuwa selective Sana. Tunapenda kuajiriwa mijini tuu, hatutaki kupangiwa Vijijin au baadhi ya Mikoa. Mwezi May mwaka huu serikali iliajiri Madaktari 1000 nchi nzima. Hata hivyo, karibu asilimia 40 ya madaktar hao hawakuripoti kwa kisingizio Cha kupangiwa maeneo ambayo hawakuchagua hasa Vijijin. Sasa ili kukata mzizi huu wa fitina na lawama za kupangiwa sehemu ambayo hujachagua, Bora Upangaji wa vituo vya kazi ufuate mfumo wa Bottom to Top. Kwa sababu Kama mtu alijitolea sehemu, maanake anaikubali sehemu hiyo na akipangiwa ataripoti.
 
Lakini katika hali ya kawaida, iwapo kuna mtu alikubali kujitolea bure au kwa malipo kidogo na mkashikiana naye katika wakati mgumu, inapopatikana nafasi kwanini asianze kupewa yeye kwanza? Hilo mbona ni jambo la kawaida sana katika ofisi nyingi duniani? Na serikali imefanya hivyo mara nyingi tu katika miaka ya nyuma. Hata ofisi nyingi kuna watu wameajiriwa kupitia utaratibu huo kwahiyo si kitu kigeni wala.

Kama wewe ungekuwa na kampuni yako na mtu akaomba kujitolea kupata uzoefu. Katika kufanya hivyo akatoa mchango kwenye kampuni kuendesha kazi zake kwa gharama nafuu, ikipatikana fedha na unahitaji kuajiri utaacha kumfikiria kwanza? Tunapolaumu tujiulize pia kwanza.

Mimi naunga mkono hili la kuwaajiri kwanza wote ambsao walikubali kujitolea. nafasi zitakazobaki ndiyo wapewe ambao hawakufanya hivyo kwa ushindani wa kawaida.
Hili suala wala halina shida yoyote ile. Waajiri ulimwenguni kote huwapa kipaumbele wale waliojitolea kufanya nao kazi. Tatizo elimu ya bongo mtu anakariri kuanzia darasani mpaka nje kwenye maisha halisi. Wasomi wetu pia wajue serikali ni kama waajiri wengine, haipangiwi lini iajiri na imwajiri nani.
 
Imagine kuna mwl shule x anajitolea miaka 2, then ajira zimetoka wewe uliyekuwa unafundisha private unapata nafasi kwenye hiyo shule x nae mwl alokuwa anajitolea kwenye hiyo shule x hajapata nafasi.

No No sio kila kitu tupinge, kwa hili naipongeza serikali kama wametoa kipaumbele kwa wale wanaojitolea katika shule za serikali.
Serikali ilichokifanya ni kizuri tatizo wanaoharibu ni hao wakuu wa mashule na mafisa halmashauri kupachika watu wao.
 
Hii Serikali wasanii tu. Mke wangu ni Mwalimu wa Physics alikuwa anajitolea kufundisha shule moja kwenye Municipal moja,ajira zilivyotangazwa headmaster wa hiyo secondary akamuandikia recommandation kwamba anamuhitaji na ikipitishwa na DED. Ajira zilipotoka akapangiwa mkoa wa mbali huko yaan 2000km kutoka tulipo tena vijijini hata network ni shida. Kuna classmate wangu yupo TAMISEMI kanihangaikia ili abadilishiwe kashindwa anaambiwa ni maagizo kutoka juu hakuna kubadilisha. Hiyo ilikuwa 2017.
Shukuru Mungu kumbe alipata ajira tayari
 
Wananchi waliopo huko wanaishi vipi? Yaani wewe na kashahada kako ka ualimu ushajiona ni mtu maalumu Sana? Ili uende ualimu kwa vyovyote vile ulifeli. Sasa failure unaanzaje kuleta tambo na nyodo?
Mkuu heshima taaluma ya watu hata kama unawachukia.
Unadhani familia yako na wewe ulifundishwaje?
Comment yako inakosa busara.
Ni ushauri tu kuwa jenga hoja bila ya kuanza kutoa maneno yasiyofaa.
 
Wananchi waliopo huko wanaishi vipi? Yaani wewe na kashahada kako ka ualimu ushajiona ni mtu maalumu Sana? Ili uende ualimu kwa vyovyote vile ulifeli. Sasa failure unaanzaje kuleta tambo na nyodo?
We kweli sexless halafu, Nani kakwambia walimu ndo waliofeli??
Nina jamaa zangu walipata division 1 wengine two form six science ni walimu wazuri we unasemaje??
Kwa haraka haraka huna akili kichwan.
 
Umelalamika sana na kweli inaleta maudhi na simanzi, ila mtu akikuuliza kuwa mwaka 2015 ulichagua chama gani jibu litakuwa ni CCM!
Jamani! Suala la wakuu wa shule kutuma majina ya walimu wanaojitolea ofisi ya Rais-tamisemi kwa lengo la kupatiwa ajira ni ubaguzi na siyo haki kabisa.

Kama mtakumbuka baada ya ajira kuwa ngumu! Serikali ilitoa tamko vijana kutafuta fursa kwenye mashirika na shule binafsi pia serikali ilisisitiza vijana kujiajiri kwa lengo la kujikwamua kimaisha kwa kipindi chote wakisubiria fursa za ajira zitakapotangazwa.

Kweli! Baada ya matamko hayo vijana wengi walianza kutafuta fursa kila mahali! Kwenye mashirika, shule binafsi, kufungua mabanda ya chips, kulima bustani etc.

Lakini! Leo katika hali ya kushangaza serikali inapita kuchukua majina ya walimu wanaojitolea shule za serikali ili wapatiwe ajira za moja kwa moja!

Kinacho nisikitisha ni namna zoezi hili lilivyofanywa! Mfano mimi nilipomaliza chuo 2017 nilienda kujitolea sekondari fulani hapa jijini Dar! Lakini mazingira niliyokutana nayo ikiwemo kunyanyaswa kingono na walimu waajiriwa na gharama za nauli 800 kwa siku! kusema kweli ilifikia hatua nikashindwa kuendelea!

Mwaka huu mwezi wa pili! Wilaya ya temeke ilipotanga uhitaji wa walimu wa kujitolea nilienda kwa bahati mbaya huko nako nilipofika nikaambiwa wameshajaa hawahitaji tena!

Kwahiyo! Serikali inapotaka walimu waliojitolea ndio waajiriwe tu naona kabisa haitutendei haki ni bora ajira ziwe kwa wote ila wakujitolea wapewe kipaumbele kwanza!

Kitu kingine! Kwenye utumaji majina si kweli majina yote yaliyotumwa walikuwa wakijitolea! Wengine wameandikwa baada ya kusikia ofisi ya Rais- tamisemi inayahitaji. Yaani mkuu wa shule anamwandika ndugu yake kisha anamwambia awe anajisogeza sogeza hapo shuleni ili siku team ya tamisemi ikipita kufanya ukaguzi imkute!

Sisi ambao hatujuani na hatukuwa na hela za kuwaonga wakuu wa shule watume majina yetu naona giza tuturu kwa upande wetu! naomba serikali ilitazame upya suala la kujitolea kwa mapana zaidi ili na sisi wanyonge tupate fursa ya ajira!
 
Back
Top Bottom