Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Serikali kuweka siku ya jumamosi kuwa siku ya Usaili ni kuwakosea HAKI Wahitimu waumini wa kisabato.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Sabato Njema. (itikia Njema Sana).
Wahitimu wa kisabato wanasikitika baada ya baadhi Yao kukosa kwenda kwenye Usaili kutokana na siku iliyowekwa kwaajili ya Usaili ni siku ya ibada. Sikukuu ya Mungu wao wanaomuamini.
Ikumbukwe kuwa Sabato kwa waumini wa kisabato ni Moja ya amri kubwa na kuu wanaamini wameagizwa kuifuata na Mungu wao wakirejelea Torati ya Musa katika Biblia, katika Kutoka 20:8-11
Tunafahamu kuwa serikali huenda ilifanya kwa bahati mbaya kwa kusahaukundi hili la Wasabato. Na hatutaki kuamini kuwa imefanywa makusudi bila kujali au kwa kudharau Wasabato kwa Sababu zozote zile.
Wasabato sio Watu wakujihusisha na mambo ya siasa na kiserikali na hii huenda ni Moja ya sababu ya wao kusahaulika hata kwa mambo muhimu kama ya Ajira.
Mimi Kama Taikon Master, ambaye ni Msabato. Baada ya kupewa taarifa hiyo kwa kweli nilisikitika Sana. Nikaona kuinyamazia inaweza kujirudia na kuwafanya Wananchi wa Kitanzania, wanaoabudu katika dhehebu la Wasabato wanaweza kukosa Haki Yao kwa wakati Mwingine.
Serikali kupitia Wizara husika, ifuatilie Jambo hilo na kulifanyia marekebisho.
Taikon Acha nipumzike sasa.
Kesho tukutane, KANISA LA MWENGE SDA, DAR ES SALAAM.
SABATO NJEMA