Serikali kupitia Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, inatarajia kuzindua rasmi Jukwaa la Vijana (Youth Platform) tarehe Januari 10, 2025, katika Ukumbi wa JNICC, jijini Dar es Salaam.
Uzinduzi huo utaongozwa na Waziri wa Maendeleo ya Vijana, Dkt. Joel Arthur Nanauka, ambapo jukwaa hilo litatoa nafasi kwa vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini kueleza changamoto zao, kubadilishana mawazo na kuunganisha nguvu katika kushughulikia masuala yanayowahusu moja kwa moja.
Aidha, Jukwaa la Vijana linatarajiwa kuwa chombo rasmi cha kusikiliza na kuthamini sauti za vijana, sambamba na kuwapa fursa ya kushiriki kikamilifu katika mipango na maamuzi ya maendeleo ya taifa, kwa lengo la kuimarisha mchango wao katika ujenzi wa uchumi na ustawi wa nchi.Serikali kupitia Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, inatarajia kuzindua rasmi Jukwaa la Vijana (Youth Platform) tarehe Januari 10, 2025, katika Ukumbi wa JNICC, jijini Dar es Salaam.
Uzinduzi huo utaongozwa na Waziri wa Maendeleo ya Vijana, Dkt. Joel Arthur Nanauka, ambapo jukwaa hilo litatoa nafasi kwa vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini kueleza changamoto zao, kubadilishana mawazo na kuunganisha nguvu katika kushughulikia masuala yanayowahusu moja kwa moja.
Aidha, Jukwaa la Vijana linatarajiwa kuwa chombo rasmi cha kusikiliza na kuthamini sauti za vijana, sambamba na kuwapa fursa ya kushiriki kikamilifu katika mipango na maamuzi ya maendeleo ya taifa, kwa lengo la kuimarisha mchango wao katika ujenzi wa uchumi na ustawi wa nchi.