Serikali: Kwa jiji la Dar es Salaam sasa darasa moja wanakaa Wanafunzi 35 - 40 tofauti na awamu iliyopita ambapo walikaa 70 - 80

Hii kushukuru watu (GoT) kutimiza wajibu wake Kama hisani sio sawa
 
Nakumbuka enzi nasoma mwalimu alikua anachanganya mkondo A,B na C kwenye darasa moja ili afundishe wote kwa pamoja, waliangalie na swala la walimu pia.
 
Uwongo usiandike jambo hujafanya utafiti darasa moja BENJAMINI HIGH SCHOOL WANAKAA WANAFUNZI 65 MSIMBAZI SEC WANAKAA 102 KARUME PR WANAKAA 85 MPAKA 90 usitudanganye
 
Huko sio Jiji la Dar es salam mkuu muwe mnaelewa au mmesahau mabadiliko yaliyofanywa na shujaa wetu. Huko ni Halmashauri ya Ubungo, hadhi sawa kama namtumbo tu au KilindišŸ˜†
 
Nonsense, Kama walimu wapya hawajaajiriwa, wanawezaje kumanage madarasa yote??

pia kwa elimu hii ya kufundisha Ngoni migration, hata kila mwanafunzi akiwa na darasa lake haisaidii kitu
 

Baeleze baelewe baache kusifia
 
Stori za awamu zimekua nyingi, kila awamu mafanikioo ... Aya bhanaaaa
 
Natamani vile vipindi vya TBCCM virudi
1. Kishindo Cha awamu hii
2. Tunatekeleza
Hivi mbona vilizimwa Kama mshumaa baada ya tukio?
 
Wanafunzi 40 kila darasa je waalimu wa kuzunguka darasa kwa darasa anafata hao wanafunzi 40 wapo wapi??? Mwalimu akisema aingie mkondo mmoja wa wanafunzi 40 kisha aende mwingine na mwingine na mwingine hadi kuisha si waalimu na wanafunzi watalala hapo shuleni. Emu serikali itoe ajira kwa waalimu waliopo kitaaa hali ni mbaya sana
 
Fimbo ya asali mimi nasema kama mtanzania yeye haoni kama matatizo yapo kila mahali halafu anazungumzia eneo moja tu tanuaga akili we mwalimu wa mataahira. Sasa aje na wa shinyanga aseme yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…