Serikali lawamani kuruhusu Mkusanyiko wa Maelfu kwenye Kilimanjaro Marathon wakati Taifa linapambana na Virusi vya Korona

Serikali lawamani kuruhusu Mkusanyiko wa Maelfu kwenye Kilimanjaro Marathon wakati Taifa linapambana na Virusi vya Korona

Jifungie wewe na familia yako kama unataka!! Hapo hakuna wa kukuambukiza !. Kuna aliyekuzuia kujiwekea lockdown?? Watanzania wengi ni wanafiki!! Utaikuta mtu anailalamikia serikali lakini mwenyewe hana hata habari ya barakoa!
Heri wafe hao wasiojijali, ila tatizo wataambukiza wengine ambao siyo familia yao peke yao!

Au unadhani korona inaishia kwa mwenye kuipata tu? - Tatizo ni kuwa hao wasiojijali watasambaza korona kwa wingi zaidi wakirudi makwao
 
Hapo usishangae baada ya wiki mbili tukaaanza kuimba ule wimbo wa tumpeleke tumpelee
Tahadhari ni muhimu lakini tunamshukuru Mungu Tanzania corona haipo kivile!! Ikiwepo utaiona tu!! Tumshukuru Sana Mungu kuwa kutunusuru. Tumshukuru pia Rais wetu kuwa kutuongoza vizuri kwenye kuikabili corona.

Aliipambanisha corona na Mungu, na corona ikaangukia pia!! Yale mataifa waliojifanya wanajua kupambana nayo kisayansi mpaka leo wanalia nayo na wanazika kila siku kwa mamia na wengine kwa maelfu na maambukizi mapya kila siku kwa maelfu!! Halafu leo bila aibu eti wawe waalimu wa kutufundisha kupambana na corona!!! Hawana hata haya!!
 
Watu walikuwa wengi kwelikweli, ni maelfu ya watu wamekusanyika kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Kilimanjaro Marathon. Miongoni mwao wapo ambao hawakuvaa barakoa kabisa, na wamo amabao walizivaa na kuzivua....
Nimeona ni kama title haiendani na kilichomo ndani. Nilidhani labda ni taasisi fulani ndiyo imeilaumu serikali, kumbe ni mawazo yako tu mwanajf? Wakati mwingine title iendane na maudhui yaliyomo ndani
 
Kuna tatizo la baadhi ya watu kutokukubali uhalisia wa aina ya corona iliyopo nchini au afrika kiujumla,mwanzo tulianza kwa kufikiria kuoKota miili barabarani hadi sasa tunaelekea kuona corona ni ugonjwa wa wazee tu.
 
Watu walikuwa wengi kwelikweli, ni maelfu ya watu wamekusanyika kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Kilimanjaro Marathon. Miongoni mwao wapo ambao hawakuvaa barakoa kabisa, na wamo amabao walizivaa na kuzivua....
Kati ya watu 10 waliolike hii thread hakosekani muuza majeneza maana kwa mkusanyiko huo na hii hali.

Wanadamu tulipewa uwezo wa kupambanua mambo kwanini tunashindwa kuutumia uwezo huo kujiepusha na hatari iliyopo sawa tena pakiwa pametolewa directives na mamlaka husika?
 
Kwahilo serikali haihusiki kabisa, ni ujinga wa waliohudhuria........Kilimanjaro Mungu aepushe tu,ila wanaweza kuathirika na hizo mbio
 
Hivi mpaka leo Kuna watu wanaamin barakoa zinasaidia eeh
Me nawashaur tu ikiwezekana hameni nchi nenden huko wanakoo vaa hizo barakoa na hawana misongamano
Kwa usalama wenu zaidi
Yaan tatizo watu hatuna shukran tunaangalia upinzan tu anayetupony corona ni MUNGU sio hizo barakoa
Mkuu huyohuyo Mungu ndiye anampa binadamu maarifa ya kukabiliana na mambo.....tusimtwishe mzigo mkubwa Mungu wakati kuna baadhi ya mambo tunaweza kujisaidia
 
Nimeona mpaka wanotwit kumlaumu Namba Moja nao wamekusanyika kwenye hilo Marasoni.

Sasa sijui wanakua wanamfurahisha nani mtandanoni hapo hata Barakoa awajavaa
 
Ila watanzania tunastahili lawama kwa kiwango cha juu sana, haiwezekani pamoja na taarifa zote kuhusu Corona zinazosambaa kwenye mitandao na vyombo vingine vya habari japo huko wanaita "nimonia", bado kuna watu hawachukui tahadhari mpaka leo....
Mkuu wewe chakufanya chukua familia yako jifungie ndani, vaa balakoa na kaambali na mikusanyiko.

Tulianza na Mungu lazima tumalize na Mungu wacha dunia yote itushangae.
 
Huu ni uthibitisho kuwa hakuna corona kivile!! Viwanja vya mpira vinajaa kila weekend!! Kwenye dala dala hakuna cha siti levo! Sokoni ndio usiseme!! Mashuleni, vyuoni!! Kama tungekuwa na corona yenyewe, ndani ya wiki moja pasingekalika!! Vifo havifichiki!! Vifo tunavyoshuhudia ni vya kawaida...
Elimu, una shida ya kupata elimu juu ya corona kama walivyo wananchi wengi.

Kupata Corona si lazima uugue corona.

Kuugua corona si lazima ufe kwa corona.

Lakini corona ni ugonjwa unaoambukizwa kirahisi sana.

Korona inaua siyo lazima ikuue wewe, inaweza muua rafiki yako ,kiongozi wako au ndugu yako.

Covid 19 imeonekana kuweza kumutate. Na sasa inaua zaidi tofauti na mwaka jana. Nani anajua itakapomutate zaidi italeta madhara kiasi gani?

Kupamnana na corona siyo kupambana na serikali (ubongo wa walio wengi mnaokula kwa Kaisari mnadhani kuipinga korona ni kuipinga serikali)

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Mimi pia nilikuwepo kwenye Kili Marathon kwa mbio za 42k. Kulikuwa na tahadhari za kunawa mikono, kuvaa barakoa nk.

Mimi nilinawa mikono wakati wa kuingia, wakati wa kusubiri kabla ya mbio kuanza nilivaa baraka. Baada ya mbio kuanza nimekimbia na barakoa mita 300 mpaka nilipopata nafasi ya kutosha ya social distance ndipo nikaivua. Wakati wa kumaliza baada ya finish line unapewa barakoa na unawekewa sanitizer.

Baada ya mbio sikukaa hata dk 2 nikaondoka.
 
Mambo yalikuwa hivi
20210301_012900.jpg
 
Watu walikuwa wengi kwelikweli, ni maelfu ya watu wamekusanyika kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Kilimanjaro Marathon. Miongoni mwao wapo ambao hawakuvaa barakoa kabisa, na wamo amabao walizivaa na kuzivua.
Mkuu, naona ulitaka wakimbie wakiwa wamevaa barakoa!
 
Back
Top Bottom