Serikali lazima itambue BAKWATA ni dhehebu moja tu miongoni mwa madhehebu ya Kiislamu, wala BAKWATA haina haki wala sifa ya chombo cha Waislamu

Serikali lazima itambue BAKWATA ni dhehebu moja tu miongoni mwa madhehebu ya Kiislamu, wala BAKWATA haina haki wala sifa ya chombo cha Waislamu

Waislamu msipende kutupa lawama kwa Serikali, serikali haijawahi kiwazuia kuunda combo kingine kinacho waunganisheni nyie, shida ni gharama za uendeshaji wa vyombo vyenu; mngependa combo mtakacho kiunda kigharamiwa na serikali, that's where the problem is; mwishoni mwa miaka ya 80 mliunda combo kinaitwa BARUKTA, why kilikufa? Serikali haijawahi kuwazuia kuunda any of them, make it now na mkasajiri na mgharamie wenyewe, simple as that
Ujuaji wako kuhusu serikali umeishia hapa.🤷

Ni vyema ukajua pia TAWALA inahitaji TU jicho lake.
 
Ujuaji wako kuhusu serikali umeishia hapa.🤷

Ni vyema ukajua pia TAWALA inahitaji TU jicho lake.
Acheni visingizio visivyo na msingi; Unaijua BARUKTA ya kina sheikh Kassim (RIP) wa msikiti wa kwa Mtoro miaka ya 80 mwishoni? Nani aliiua bro. I know what I'm saying. Waislam kila kitu duniani ni kulalamika tu. Anzisheni tuone kama serikali itakataa kusajiri.
 
Ujuaji wako kuhusu serikali umeishia hapa.🤷

Ni vyema ukajua pia TAWALA inahitaji TU jicho lake.
Unabishana na mtoto huyo wakati mwingine Bora kukaa kimya maana utapoteza muda hajui hata historia ya uislam na Bakwata ipoje
 
BAKWATA SIO CHOMBO CHA WAISLAAM WOTE...BALI NI KIKUNDI TU CHA DHEHEBU MOJA. IBAKI HIVYO.

Siasa katika Dunia ya Kiislamu

Hata Sheikh wetu nchini Tanzania, mwanazuoni Sheikh Abuu Iddi ambaye ni Msaidizi wa Mufti wa Tanzania aliwahi kuonya juu ya dhehebu moja kuanza fitna, misuguano, kutishiana n.k dhidi la dhehebu jingine, wakati wote ni dini moja ya ki-Islamu..

19 January 2023
Dar es Salaam, Tanzania

SHEIKH ABUU - HATARI INAKUJA TUSIPOTOA TAHADHARI KWA HAYA YANAYOENDELEA



Sheikh Abuu Iddi ambaye ni Msaidizi wa Mufti wa Tanzania ametoa tahadhari hiyo kwa kuwa inaweza kupelekea amani kuvunjika nchini Tanzania.

Sheikh Abuu Iddi CV (wasifu) yake imesheheni nyadhifa kadha wa kadha sawia na maktaba yake binafsi iliyosheni mabuku juu ya mabuku ya elimu duniya na ilm ya dini pia ktk utumishi ulitukuka kwa dini na jamii.

Pia sheikh Abuu Iddi ni imamu mkuu msikiti wa Masjid Mnyamani Buguruni jijini Dar es Salaam. Pia kwa miaka 16 amekuwa akiendesha kipindi ktk kituo cha televisheni cha Channel Ten kutoa daawa na darsa, mratibu Al Risala Foundation, Mratibu wa Kudumisha Amani katika mkoa wa Dar es Salaam, Mwandishi wa kitabu kinachokwenda kwa jina Misingi 15 ya amani, mwandishi wa makala katika gazeti kubwa la Mwananchi pia ni Mshauri wa dini na jamii wa Mufti Mkuu wa Tanzania.

Sheikh Abuu Iddi ameelekeza tahadhari hii hususan kwa madhehebu ya Sunni Saudia na Shia linaloegamia Iran yanayo shambuliana kupitia propaganda kutoka maeneo mbalimbali ya dunia ya mitandao ya kijamii wakiongozwa na viongozi wao wenye ushawishi wa kisiasa wa ndani na nje ya nchi kuchochea misuguano
 
Mzee Mohamed Said - BAKWATA ni mwiba mzito kwa Waislamu Tanzania

Mzee (Sheikh) Mohamed Said akitoa muhadhara kwa vijana wa kiislamu kufahanu historia ya taasisi za kiislamu Tanzania na michango ya taasisi hizi kwa uhuru wa Tanzania :

View: https://m.youtube.com/watch?v=IvodWTgWpSM
East African Muslim Welfare Society, migongano ya waislamu tanzania kwa kufuata asili ya mtu.

Mambo yakawa mazito 1968 muafaka miongoni mwa waislamu wa Tanzania ukashindwa kufikiwa.

Kina mama wa kiislamu watokwa macho kwa hali hii ya waislamu kuhitafiliana kwa kuangaliana asili, badala ya kuwa umma mmoja usio na chembe za kibaguzi .

Kuanzia hapo maendeleo na mipango ya waislamu ikavuzurugika, makundi ndani ya uislamu Tanzania yakaibuka

Wafadhili waliotaka kujenga Chuo Kikuu chini ya ufadhili wa Aga Khan wakatoweka kutokana na kutofautiana waislamu ndani ya Tanzania

Mzee Mohamed Said akaendelea na mudhara wake akawapa changamoto wanafunzi kama wanaelewa kwanini wanavaa hijabu, haikuwa kazi ndogo nitawaeleza ..
 
Waislamu msipende kutupa lawama kwa Serikali, serikali haijawahi kuwazuia kuunda chombo kingine kinacho waunganisheni nyie, shida ni gharama za uendeshaji wa vyombo vyenu; mngependa chombo mtakacho kiunda kigharamiwa na serikali, that's where the problem is; mwishoni mwa miaka ya 80 mliunda chombo kinaitwa BARUKTA, why kilikufa? Serikali haijawahi kuwazuia kuunda any of them, make it now na mkasajiri na mgharamie wenyewe, simple as that
ni BALUKTA, ilijigeuza ni chama cha siasa kikafutiliwa mbali, mwenyekiti wake alikuwa sheikh yahya husein.
 
Sisi wamatumbi weusi tunapuuzia historia

Kwa undani :

Toka maktaba:

Simulizi za Mjukuu wa Mfalme Mlinganaweka AleiwaLunga wa maeneo ya Wamachinga Pwani ya
Tanzania

Simulizi za wazee wetu : Waasisi wa madhehebu ya Ma- Shia nchini
Tanzania na kwanini dhehebu la Shia lina kanuni la kukubali vijana wao kuuliza maswali (tabligh) wakati Sunni hukataza vijana wao kuuliza maswali na kulazimishwa kuwa mkubwa ktk imani yaani sheikh / Imamu / Maalim akisema basi yeye ndiye anafahamu ilm yote ya dini

(NZIMA)-SIMULIZI YA MAREHEMU SHEIKH ABDALLAH SEIF (1939 -2020) - HISTORIA YETU part 1



KIU YA ILMU, SHEIKH ABDALLAH SEIF ILIMPELEKEA KUSOMA KWA MIAKA 11 MFULILIZO KATIKA NCHI ZA IRAQ, LEBANON NA IRAN (1968-1979)

Sheikh Abdallah Seif Linganaweka anatujuza kuwa Wenyeji wa Lindi jina Lao la asili ni Wakudewe kwa sasa almaaruf wanafahamika kama waMachinga wa pwani ya Lindi.

Babu yake Babu Abdallah Seif alikuwa mfalme Mlinganaweka AleiwaLunga mwenye watumwa baada ya kuwazidi wanyonge majirani kuja kuwatumikisha kujaza vyakula. Mfalme Alei(Ali)waLunga.. wa Lindi.

Baada ya kuja mkoloni Muingereza nchini Tanganyika, aliua ufalme na kubakiza uchifu. Sehemu za pwani ziliathirika kwanza kwa kupoteza ufalme mapema kabla ya watu wa bara.. Pwani wakabakia na usheikh na uchifu... usiokuwa na nguvu kama falme za asili za maeneo yao Lindi / Kilwa kabla ya kuja ukoloni...

Sheikh MbogaBure mjuzi wa lugha ya Kiarabu, dini pia mmoja wa waanzilishi wa madhehebu ya Shia Tanzania amuunganisha Mzee Abdallah Seif kupata scholarship kwenda Baghdad, Iraq mwaka 1968 kusoma zaidi dini...

Kijana Abdallah Seif mwaka 1968 alipokwenda Kijijini ashutumiwa kupotea kwa kuukumbatia u-Shia mojawapo ya madhehebu ya dini ya KiIslamu, wakati wengine wote ni Sunni. Lakini babu yake msomi wa dini madhehebu wa Sunni anayetambulika Lindi na Kilwa hakuwa anatoa shutma zozote alikuwa msikivu na kumtia moyo Abdallah Seif asome zaidi na ili kuifahamu dini vizuri zaidi.

Kilichomsukuma Sheikh Abdallah Seif kuvutiwa na u-Shia ni namna masheikh wa ki-Shia walivyokuwa wazi (tabligh) kukaribisha maswali tofauti na madhehebu mengine ya KiIslam ambapo kijana hakuruhusiwa kuhoji na pia kuuliza maswali ilikuwa inachukuliwa ni utovu wa nidhamu kwa waalimu au masheikh wake.

Safari ya Sheikh Abdallah Seif wenzie vijana wakiwemo kina Sheikh Isihaka Pingili kwenda Iraq kwa meli iliwachukua mwezi mzima kupitia bandari mbalimbali za Zanzibar, Tanga, Mogadishu, Bahrain na kuishia Basra nchini Iraq na kutua katika chuo cha Hawza mji wa Najaf Iraq

Ujio wao Basra, Iraq ulileta tafrani kwa mwenyeji wao Mpakistani mfanyabiashara mkubwa nchini Iraq enzi hizo na kupelekea Saadam Hussein kumshutumu mfanyabiashara huyo tajwa kuleta majasusi wa kiAfrika ikumbukwe ndiyo kwanza Saddam Hussein na chama chake cha Baath walikuwa wanajaribu kushika hatamu za kuongoza nchi baada ya mapinduzi nchini Iraq. Mpakistani huyo alinyongwa mwaka 1969 pamoja na wafadhili wengine kama kuna Bakri Sadr waliowezesha ujio wa vijana wa kiAfrika kuingia Iraq kwa dhumuni la kusoma dini.

Kutokana na hilo ikabidi Sheikh Abdallah Seif, Sheikh Isihaka Pingili na vijana wengine wa kiAfrika waondoke Iraq mwaka 1970 kwenda Lebanon kwenda kuendelea na azma yao ya kusoma dini.

Sheikh Abdallah Seif wakakaa Lebanon kuanzia mwaka 1970 mpaka 1978 ambapo mara nyingine masomo ya dini yakaingia changamoto baada ya vita baina ya Wapaletina waliokuwa kambi za ukimbizi Lebanon na waLebanon wenye nchi na kuzua vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mwaka 1978 Ikabidi Sheikh Abdallah Seif na wenzie wahamie nchi ya jirani ya Iran kwenda katika mji wa Qom city kuendelea na masomo yao ya dini. Iran ilikuwa imetulia nchi ya amani chini ya utawala wa mfalme (Shah) Mohammed Reza Pahlavi Historic Personalities of Iran: Mohammad Reza Shah Pahlavi miaka 7 waliakaa Iran wakiendelea kusomeshwa.

Wakati wa likizo Iran wengine wenda Ufaransa kuchuma zabibu mashambani au kufanya kazi sehemu za utalii wa ndani wa Iran au kuchukua mabusati ya kushona ya Iran yanayosifika Uarabuni kote kwenda kuyauza ktk nchi mbalimbali za Arabuni ndivyo mwanafunzi kama Sheikh Abdallah Seif na wenzie vijana walivyojiongezea fedha za kujikimu na kupeleka kiasi cha pesa nyumbani Tanzania.

Hatimaye mwaka 1980 baada ya kusoma kwa miaka 11 nje ya Tanzania ,walitunikiwa shahada ya baccalauréat ya masomo ya dini na kurejea Tanzania. Kwa miaka hiyo 11 ughaibuni pia waliweza kusoma elimu ya secular kiwango cha sekondari kwa njia ya posta masomo ya nchi ya Uingereza kwa msaada mkubwa wa swahiba wa kiongozi wa kijeshi wa Nigeria Jenerali Yakubu Gowon. Swahiba huyo alikuwa mfanyabishara wa vituo vya mafuta na makazi yake Uingereza.

Mahojiano haya yanakuja kwa hisani kubwa ya Ammar Dachi aliyemshawishi Mzee Abdallah Seif kufunguka historia ya mapito yake, ukoo , ilmu na utafiti wa mafuta 1955 na pia ujio wa madhehebu ya Shia nchini Tanzania


HISTORIA YA ABDALLAH SEIF (1939 -2020) Part - 2



Sheikh Alhaj Sheikh Abdallah Seif Linganaweka mzaliwa na mwenyeji wa kijiji cha Mnan’gole sehemu za Dimba mkoa Lindi Tanzania anaendelea kusimulia kazi kubwa aliyofanya ya kujitolea ya kueneza dini.

Sheikh Abdallah Seif anasisitiza umuhimu wa ilmu na elimu kwa wanazuoni wote wa KiIslamu.

Anasema ili sheikh awe mwanazuoni aliyekamilika kufundisha chuoni lazima kusoma ilmu ya dini kwa angalau miaka 15.

Anakumbuka alivyokuwa mjini Qom Iran akisoma chuoni alionana na wazee wenye umri wa miaka 70 wakijiendeleza na kuwaambia wao vijana kuwa inahitajika jumla ya miaka 35 ili kuielewa dini nje ndani kwa ufasaha. Wazee hao walicheka waliposikia vijana Sheikh Abdallah Seif, Sheikh Isihaka Pingili na vijana wengine toka Afrika wakisema wanataka kusoma dini kwa miaka 5 mpaka 10 tu ilihali wametoka Afrika na kuwaambia bila kupepesa macho kuwa ili wawe wabobevu wafikirie miaka angalau 15 ya ilmu ya dini ngazi ya chuo.

Hivyo akiwa amepikika kwa elimu tosha ya kidini baada ya kufanya kazi kwa takriban miaka 11 nchini Tanzania, mwaka 1990 sheikh Abdallah Seifu alikwenda Nampula jimbo la Cabo Delgado nchini Mozambique kufanya kazi ya dini.

Kisha sheikh Abdallah Seif alishuka mpaka mji mkuu wa Maputo Mozambique na alisaidia kufungua taasisi rasmi inayotambulika na serikali na kupewa leseni iliyosajiliwa Maputo Mozambique kwa ajili ya taasisi ya Shia Ithna-Asheri Muzdalifah . Sheikh Abdallah Seif anazungumza lugha za Kiswahili, Kiarabu, Kiingereza na Kireno.

Source : Asadiqmedia

RAMBIRAMBI NA WASIFU - Marhum Sheikh Abdallah Seif



Source : Asadiqmedia
 
13 November 2024
Sheikh Ponda : Waumini 12 kuiburuza BAKWATA mbele ya Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam,


View: https://m.youtube.com/watch?v=tKN_8LKHIQ8

Katibu wa Jumuiya ya Taasisi ya Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda aelezea kiini cha kesi hiyo ya Kikatiba baina ya Waislamu dhidi ya BAKWATA .. ni ...

Kiini ni Waislamu wanataka kuamua mambo yao kwa uhuru wa kujiamulia mambo yao wenyewe bila kubanwa na BAKWATA ..

Kujichagulia viongozi wao wenyewe waislamu, miradi ya kiuchumi, ardhi, shule za elimu, majengo ya wakfu mbalimbali ...

Chini ya Ukoloni waislamu walikuwa na uhuru wa kuamua mambo yao wenyewe ila baada ya uhuru ilipofika miaka baina 1963 hadi 1968 serikali iliingilia mambo ya waislamu na kuvunja mambo yaliyokuwa yanawapa uhuru kabla ya uhuru ..

Kutokana na hilo waislamu wameona kulikabili jambo hili kisheria kwa kulipeleka Mahakamani, maana uhuru wa waumini ni suala la kikatiba hivyo kuamua kufungua kesi ya kikatiba dhidi ya BAKWATA inayoendeshwa na watu wachache wasiochaguliwa na waislamu na pia kudai uhuru wa kujiamulia mambo ya waislamu bila kubanwa na BAKWATA ...
 
Kupitia jukwaa hili naomba, kuifahamisha Serikali...na isijifanye hailioni hili...

BAKWATA ni dhehebu la TWARIQA, miongoni mwa madhehebu tu kama vile lilivyo, HIZB TAHRIIR, TABLIIGH, SALAFY, SHIA...

Ndio maana hata namna yao ya kuendesha mambo yao na uteuzi wa watu wao kuanzia Mufti mpaka imaam wa msikiti lazima uwe MTU WA TWARIIQA...Huwezi kuwa hata MUADHINI MSIKITINI usipokuwa TWARIIQA.

Je ina haqi gani ya kujifanya baraza la WAISLAAM na kukasimishwa mambo ya waislaam wao...

Wengi walioko Bakwata ni wajanja wajanja tu waliojifunza kiarabu zaidi na kuwa mtu unayetembea na masheikh zao wa twariqa kwenda kwenye dhikr mbalimbali basi utapewa nafasi Bakwata..

Ndio waliopo hata kwenye zinazoitwa Mahakama za Qadhi...

Haakim wa MAHAKAMA YA QADHI...lazima mtu awe mtu aliyebobea katika sheria ya kiislaam kwa kauli mbalimbali za wanachuoni wanaotegemewa katika UISLAAM...

Lakini wamepewa uqadhi Mamuriid...na wazee waliozeeka na ujinga wao...na wala sio elimu...

Sisi katika UISLAAM ELIMU MBELE ZAIDI YA UMRI...

KWA SABABU UMRI SIO DALILI YA HEKIMA NA BUSARA...KWA SABABU HATA WAJINGA NA WAPUMBAVU HUZEEKQ VILEVILE...

Ila bakwata wale wazee wa Al faatiha msikitini na wajanja wajanja wasio na elimu ya dini waliofeli elimu ya shule...kwakuwa baba zao walikuwa masheikh...wakaona palipobaki ni huku...kwa connection za wazee wao na waliopo bakwata...ndio maana MASUALA YA NDOA YA KINA MAMA YAMEKITHIRI KWENYE OFISI ZAO BILA MSAADA WOWOTE KWA AKINA MAMA HAO WENYE KUDHULUMIWA.

WITO KWA SERIKALI INABIDI IITAMBUE CHOMBO CHA BAKWATA KAMA VILE WANAVYOTAMBUA JUMUIYA ZINGINE ZA DINI...

Haiwezekani misikiti ikiwa na migogoro kidogo tu ikabidhiwe BAKWATA.

BAKWATA SIO CHOMBO CHA WAISLAAM WOTE...BALI NI KIKUNDI TU CHA DHEHEBU MOJA. IBAKI HIVYO.
ninyi wa mashia na iran yenu hamuachagi chokochoko. hebu acheni fujo.
 
ni BALUKTA, ilijigeuza ni chama cha siasa kikafutiliwa mbali, mwenyekiti wake alikuwa sheikh yahya husein.
Sasa lawama kwa Serikali zinaingiaje? Wewe umesahiri kitu kwa muktadha wa kidini, unageuza kazi za hicho chombo kua jambo lingine, huoni kama wameji contradict wenyewe? Vyombo vya Kikristo vimejikita kwenye them zao, CCT, TEK, PCT nk. Hutakuja kusikia wamebadiri vision, ingawa huaga wana shauri serikali pale wanapo Ona kama serikali inakosea na hua wanapongeza pale serikali inapofanya vizuri, na hivyo vyombo wanavigharamia wao wenyewe. Waislamu wana shindwa nini?
 
BAKWATA=Balaa kuu la waislam Tanzania.

Kazi yao kubwa ni kuwapigia Ccm kampeni msikitini wakati wa uchaguzi, na kuzusha mambo yasiyokuwepo kwenye dini
Ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya.
Mbwa huyu ni kichaa.
 
Back
Top Bottom