Tetesi: Serikali mbioni kuchapisha noti mpya, kuna hatari ya kuelekea kwa Mugabe, harufu ya tenda za kifisadi zatawala

Mafisadi mnaogopa lazima kiwanuke, hizo hela zenu zinawaozea lah-sivyo zirudi ktk mzunguko.

JPM kawabana kama mjusi chini ya Mlango
 
ku print noti mpya ni kitu cha kawaida na kinafanyika kila mara, kama ni kuprint mpya lakini zenye sura hiihii hufanyika ili kufidia noti zilizochakaa ambazo huharibiwa na BOT, na ili kumpata wa kuzi print ni lazima utaratibu wa manunuzi ya umma ufuatwe (kutangaza zabuni N.K), lakini pia kama ni ku chapa noti zenye sura mpya bado haina madhara kwani tumeshafanya hivyo mara nyingi tu, na pia husaidia kurudisha fedha kwenye ma benki kutoka uvunguni mwa watu
bila kujali unachapa noti zipi kitu chenye madhara ni kuwa na noti nyingi kuliko uchumi halisi wa nchi, hii ilikuwepo sana enzi za JK na ndio maana watu wanajiuliza JK aliwezaje lakini hawajiulizi kwanini thamani ya shilingi ya tanzania ilikua inaporomoka kwa kasi
 
Kuprint not mpya me sijaelewa yaani nizilezile ila wanaziongeza nyingine au wanazibadilisha kabisa wanaleta zaaina nyingine

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani serikali haina pesa za kutosha kugharamia mambo yake na imeshindwa kupewa mikopo na dhamana haziuziki so inataka iprint pesa zingine ili igharamie shughuli zake sasa pesa hii itaingia kwenye mzunguko itakuwa nyingi kuliko shughuli za uzalishaji matokeo yake pesa itaporomoka thamani zaidi.
Kuchapa pesa zaidi kupo ila tu pale inapohitajika yaani ikiwa scarce zaidi
 
Mafisadi mnaogopa lazima kiwanuke, hizo hela zenu zinawaozea lah-sivyo zirudi ktk mzunguko.

JPM kawabana kama mjusi chini ya Mlango
Tuko karne ya 21 hao unawaita mafisadi hawataumbuka tutaumbuka sisi walala hoi. Dunia imebadilika kama inaweza kwenda popote duniani na card ya bank ya Tanzania na ukatoa pesa kwenye ATM ya nchi hiyo, au ukanunua na card ya tembo kwenye dika lolote duniani bado unafikiri kuna kuumbuka kwa mafisadi na siyo sisi wakala hoi? Nchi kama Uingereza ukinunua nyumba ya kawaida kwa cash na resident permit wanakupa unafungua account na siyo lazima uishi uingereza unafungua business zako. Huoni watafungua account kwenye nchi za jirani hata Kenya na business zao.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila mkuu hii taarifa inauhakika kiasi gani maana habari nzito hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mtu wenu kashindwa kuendesha uchumi sasa kama kawaida mnatafuta kichaka cha kujificha kwa Jk.Kama ndivyo mbona Sera zenu zimedololesha uchumi na pesa haijaimarika zaidi?
Mbona mnataka kuzalisha kuongeza money supply fake kwenye uchumi? Jk hapo anahusikaje? Hivi hamjui Sera za kubana matumizi ni mbaya kwenye uchumi dhaifu kama wetu? Mbaya zaidi Sera zenu zimeua purchasing power ili tuishi kama mashetani hatari sana..
Kama hizi habari ni kweli nyie masisiemu mnataka kutuua
 
Kama litafanyika hili basi tutegemee kutumbukia shimoni kabisa maana uchumi ukishaharibika kuurekebisha ni kazi ngumu lakini yote haya ni mavuno ya kutokuwa msikivu na kujifanya anajua kila kitu mkemia yy, injinia yy, mchumi yy lakini ifahamike wazi hawa aliowaita wanyonge watapata tabu sana kiasi cha kujuta kuzaliwa Tanzania
 
Fungua hiyo attachment utaelewa.
 
Ila mkuu hii taarifa inauhakika kiasi gani maana habari nzito hii

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijui maana hata mm ndo nasoma hapa inatumia Wasiwasi kuhold pesa benki tena kwa denomination ya shilingi ya Tzn ni vyema wahusika waweke sawa hii taarifa inatia mashaka tuendako
But ukitaka kujua ukweli hebu angalia muitikio wa dhamana za setikali lakini pia je wafanyabiashara wanachukua mikopo benki? Na je benki zinakopesha? Juzi kati nilisoma humu pia benki kuu imeshusha riba ya kukopesha commercial banks hiyo ilikuwa round ya pili kama sikosei
 
Dah hiii hatari kama itakuwa Nikweli nibora tungepambana kivingine lakini sio kuingiza pesa not mpya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni hatari kuliko kawaida Mungu aepushe mbali na wahusika wawe wasikivu mara mia hizo pesa zisichapwe kwa minajiri ya mtoa mada mtasambaratisha familia zetu jamani
 
Huyu jamaa akiprint pesa nchi itakufa kwa speed moja ya ajabu sana, ngoja nikabadili account zangu zote za bank ziwe in USD mapema sana.
 
Hii ni FAKE NEWS PER EXCELLENCE!!
 
Dah hiii hatari kama itakuwa Nikweli nibora tungepambana kivingine lakini sio kuingiza pesa not mpya

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa sasa ukipata fedha ya akiba bora uitunze kwenye dollar tena cash sio bank maana huwa kuna kipindi rationing au ukomo wa kuwithdraw unawekwa bila kujalisha uliitolea jasho au pesa yeyote ya nje yenye thamani maana yajayo yanatia mashaka
 
Kwa sasa ukipata fedha ya akiba bora uitunze kwenye dollar tena cash sio bank maana huwa kuna kipindi rationing au ukomo wa kuwithdraw unawekwa bila kujalisha uliitolea jasho au pesa yeyote ya nje yenye thamani maana yajayo yanatia mashaka
Hivi mkuu kwalocal bank kama nmb naweza kuwa naweka pesa ila kwadola yaani naenda nahela zakibongo ila nikifika nawaambia waziweke kwamtindo wadola inawezekana?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…