Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Kwamba hizo nchi maisha yako hovyo kuliko Tanzania! Unajua unachoongea boss?Sasa mbona hizo Katiba Mpya hazina maana yeyote kwenye maisha yoa? Mbona Zina maisha hovyo kuliko Tanzania..
Mfano Huwa mnazunguka huko mitaani mnawaambia watu eti Katiba Mpya itazuia Serikali Kukopa ,Ghana
,Zambia na Kenya zimefilisika kwa nini Katiba Mpya haikuzuia hayo?
Katiba Mpya is overrated na nasisitiza ni Kwa maslahi ya Wanasiasa na Wala sio Wananchi wa kawaida..
Hivi Kwa mfano maskini hana pesa hiyo Katiba Mpya itamsaidia nini akidhulumiwa Haki Mahakamani?
Kwamba kuna watu wanasema katiba mpya itazuia nchi kukopa, acha upotoshaji usio na tija, au ni ili hoja yako ionekane ya maana nini?
Ni kweli hiyo katiba mpya ni kwa ajili ya wanasiasa, je hao wananchi wa kawaida wao ni maiti, kwanini hawajitokezi kudai hayo maslahi yao wanasubiri tu wanasiasa wadai maslahi yao?
Katiba hii ya sasa ndio inamruhusu mwananchi masikini kukopa, ila ikija katiba mpya ndio itamzuia kukopa? Hoja yako ni nini hapa, au unaleta ubishani wa jazba?