Ninachofahamu ni kuwa Mh. Rais Samia alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba. Anajua "A" mpaka "Z" ya kilichotokea, hivyo kwa kuwa sasa yeye ndiye raia namba moja mwenye nguvu zaidi, na kwa kuwa kama kweli atakuwa na nia ya dhati ya kutengeneza katiba mpya, sioni chochote wala yeyote wa kumfanya asitimize hili.
Naomba Watanzania wote tunaoitakia mema Tanzania yetu, tumuombee na kumpa ushirikiano ili lengo hili litimie kwa mustakabari mwema wa vizazi vya sasa na vijavyo.
Mungu ibariki Tanzania.
Mungu mbariki Mh. Rais Samia SS.
Mungu tubariki Watanzania.