Atleast serikali inaendelea kuonesha nia, ipongezwe; wasiwasi wangu ni kwamba, kwasababu inaonekana Samia ana copy & paste kila kilichofanywa enzi za JK, isije tokea huo mchakato wa Katiba Mpya ukafa kifo kile kilichotokea wakati ule, vyema ajitahidi yeye amalizie alipoishia mwenzake.
Kinyume na hapo, utakuwa ni muendelezo ule ule wa kuchezea pesa za walipakodi, usitokee; pia sitarajii kusikia maneno ya wahafidhina wamegoma kupitisha hiki au kile, hili taifa sio la wahafidhina, ni la watanzania wote, nao kwa umoja wao ndio wanahitaji Katiba Mpya, sasa muhimu maoni yao yafanyiwe kazi kwenye hiyo Katiba itakayopatikana.
Hatuhitaji Katiba Mpya ya watawala kama hii tuliyorithi toka kwa mkoloni, hili taifa limeshakuwa huru ni wakati wa kuonesha hayo kwenye Katiba Mpya, nchi sasa irudi mikononi mwa wananchi.