Serikali msihangaike na madai ya wafanyabiashara ambayo hayatekelezeki. Njaa itawarudisha sokoni

Serikali msihangaike na madai ya wafanyabiashara ambayo hayatekelezeki. Njaa itawarudisha sokoni

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Nitoe wito Kwa Viongozi wa Serikali wasihamgaike na hao wafanyabiashara wanaotumika Kisiasa.

Wacheni wafunge biashara Kwa sababu njaa itawarudisha sokoni bila hata Nguvu.

Huwezi ukajua na madai ya kipuuzi na yasiyo na msingi.Madai Yao ni Kodi ambazo zimekuwepo Toka enzi ya Mkapa alipoleta VAT na service levy Sasa Leo hii ushindani umeongezeka wanataka kuifanya Serikali kana kwamba imeleta pendekekezo jipya wakati hizo ni Kodi za miaka yote.

Serikali isije ingia kwenye mtego wa kuburuzwa na wafanyabiashara, tujifuka hapo watapanga na kuamua nani awe Kiongozi na kuhatatisha maisha ya watu wa chini.👇👇

===
Leo June 27,2024 ikiwa ni siku ya nne ya mgomo wa Wafanyabiashara katika baadhi ya Mikoa Nchini ikiwemo Dar es salaam, AyoTV imepita katika soko la Kariakoo na kukuta baadhi ya maduka yakiwa yamefunguliwa huku wengine wakiendelea kugoma kufungua maduka yao.

Baadhi ya Wafanyabiashara wameendelea kugoma licha ya matamko kadhaa kutoka kwa Viongozi wa Serikali na Viongozi wa Wafanyabiashara wakiwataka wasitishe mgomo na kufungua maduka yao kwani kero zao sasa zinatatuliwa na Serikali baada ya kukaa nao chini kuwasikiliza.

Ayo TV imeshuhudia idadi ndogo ya Wanunuzi wa bidhaa tofauti na inavyokuwa siku za kawaida zisizo na mgomo huku magari ya matangazo yakipita kuwasihi Wafanyabiashara kufungua maduka yao na kuendelea na biashara.

Screenshot 2024-06-27 154009.png
Screenshot 2024-06-27 154019.png
Screenshot 2024-06-27 154029.png

====
My Take
Nchi hii ni ya kijamaa, kamwe wafanyabiashara hawatakuja kuiweka Serikali mfukoni.

Naomba Serikali iache kuwachekea hao watu wanakwepa Kodi na wanapanda mbegu mbaya za vurugu wakichochewa na Wakenya.

=====

Pia soma:
Mgomo wa Wafanyabiashara: Biashara zafungwa Kariakoo leo Juni 24, 2024
 
Hii nchi ni yetu sote, ni vizuri kusikilizana, sio kukomoana. Mtu mpaka anafanya maamuzi ya kufunga biashara ujue anaumia.
Ni lini Serikali ilikataa kusikiliza Kwa utaratibu ulioko?

Unapogoma si ndio unamkomoa? Nao Wanakaa kimya kwani shida Iko wapi?
 
Kwaiyo unataka kuaminisha watu kuwa wafanyabiashara hawana hoja? Yaan from no where waanze tu kugoma? Kama umefwatilia vizuri mkasa taja sababu tano walizotoa wafanyabiashara tuzichambue ili tuone wana haki au laa!
Wewe unazingua hoja zao? Zitaje
 
Back
Top Bottom