Serikali msijisahau katika hili la daktari kumtibia mtu wa jinsia tofauti na yeye

Serikali msijisahau katika hili la daktari kumtibia mtu wa jinsia tofauti na yeye

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Posts
11,837
Reaction score
17,412
Wakuu naomba niipongeze serikali kwa jitihada zake inazofanya katika kuhakikisha ile heshima ya jinsia zote inalindwa.

Tukiangalia katika majeshi hasa jeshi la polisi utakuta kuna askari wa kike ambao kama itatokea muhalifu ni mwanamke basi askari yule hakuajiriwa kwa bahati mbaya bali hiyo itakuwa ni kazi yake kumpekua sehemu za mwili wake.

Hali kadhaalika mwanaume atapekuliwa na askari wa kiume katika kulinda heshima.

Hata mashuleni kuna waalimu wa kike kibao ambao wao watashughulikia masuala mbali mbali ya wanafunzi wa kike.

Mbona sioni suala hili la kuheshimu jinsia na kulinda heshima ya mtu likifanyika na kusisitizwa katika kada ya afya ?

Kwanini isiwe kosa daktari wa kumtibia mgonjwa wa jinsia tofauti na yeye ikiwa katika hospitali hiyo ama maeneo hayo kuna daktari mwenye jinsia sawa na mgonjwa ?

Kama ambavyo polisi haruhusiwi kumfanyia upekuzi wa mwili mtu wa jinsia isiyekuwa yake wakati wa jinsia yake wakiwa pale hii ni kosa,vipi isiwe kosa katika hii kada ya afya ?

Yani utakuta hospitali kuna madaktari wa jinsia nyingi lskini mwanamke anatibiwa na mwanaume au kinyume chake.

Serikali isomeshe watoto wengi wa kike ili kuja kuepusha hii aibu,ipunguze vigezo vya kusomea udaktari kwa mwanamke hasa kwa mambo ya kawaida haya ambayo hayahitaji kujitoa sana wanawake wasomeshwe waje kuzalisha wanawake wenzao.

Chumba cha kuzalisha kuna madaktari wa kike watano na wa kiume mmoja,huyu wa kiume anatafuta nini,kwa nini isiwe kosa kisheria?
 
Naunga mkono hoja yaaan niende pumbu znauma nmwoneshe mwanamke ww uliskia waaaaaap ..hiii si sawaa kabsaa na ndo mana kuna kesi madokta wa kiume kubaka wagonjwaaa
Kinachouma mama mzazi anaenda hospitali anakutana na daktari ambaye ana umri kama wa mimi mwanae alafu madaktari wa kike wapo kabisa.

Kuna mama wa kipemba wakati anajifungua alitaka kuja daktari wa kiume, basi mama mpemba akamuuliza "uko radhi kuchungulia tv ya mamayo wee "?

Daktari akaenda mbio
 
Kama hufahamu kitu unauliza ndugu yangu..

Sheria/miongozo ipo inayotaka ukienda hospt ukahudumiwa na Dkt wa Kiume na wewe ni jinsia ya kike basi inabidi awepo nesi wa kike wakati wote ukiwa chumba cha daktari na huwa hivo hivo hata kwa wagonjwa wa jinsia ya kiume endapo watakutana na Dkt wa Kike. Na hii inatokea ili kuepusha malalamiko hususani ya wagonjwa wa kike kufanyiwa vitendo visivyo vya kiungwana na madaktar wa kiume.
 
Kwanza kabisa nakusihi uache wivu.

Tanzania Kuna madaktari wa kiume wengi kuliko wanawake. Lakini pia Tanzania wanao attend hospital wengi Ni wanawake.

Pia Kuna manesi wengi to wakiume waliosomea kuzalisha pale labour.
Vumilia tu Kaka, kuona si kuchukua Wala kutumia.
 
Mawazo ya kipuuzi kabisa, ugonjwa hauna jinsi, uchi ni uchi pale unavyotumika kwa mambo yanayoleta fedheha na tamaa ya mwili ila siyo ugonjwa, watu wanaume wanaogesha mama zao na bibi zao wakiwa hawana msaada, ije kuwa kwenye ugonjwa?utakapokuja kugundua mke wako anatiwa vidole kupima njia si utazimia wewe?acha wivu wa kijinga
 
Kinachouma mama mzazi anaenda hospitali anakutana na daktari ambaye ana umri kama wa mimi mwanae alafu madaktari wa kike wapo kabisa.

Kuna mama wa kipemba wakati anajifungua alitaka kuja daktari wa kiume,basi mama mpemba akamuuliza "uko radhi kuchungulia tv ya mamayo wee "?

Daktari akaenda mbio
Mkuu habari ya tiba ni kitu kingine kabisa, wanawake sio wazuri na kujali sana kwenye huduma,
Mwaka 2013 Temeke hospital mke wangu alienda kujifungulia pale akiwa na mimba ya mapacha, mmoja akatoka vizuri tu mwingine akagoma tena kaenda kujificha juu madr wa4 wa kike waliokua wanamhudumia wakawa wanashauri afanyiwe operesheni lkn kabla hawajafikiwa maamuzi wakaenda kuita madr wawili wa kiume walianza kumpushi yule mtoto wanavyojua wao hadi akajifungua kawaida.
 
Usiseme hiko kitu mkuu

Kuna mmama alikufa hivi hivi

Wanawake peke yao habari ingineeee km Mna biffu la nje siku ya kujifungua utaelewa vzur.

Kuna mmama alikufa kwa kuachiwa mikasi tumboni na walikuwa ni wanawake wote wa kiume alitoka mapema na kuwaachia wakike.

Sikushsuri wala siungi hoja.
 
Usiseme hiko kitu mkuu,,,



Kuna mmama alikufa hivihiv


Wanawake peke yao habari ingineeee km Mna biffu la nje siku ya kujifungua utaelewa vzur.


Kuna mmama alikufa kwa kuachiwa mikasi tumboni na walikuwa ni wanawake wote wa kiume alitoka mapema na kuwaachia wakike.




Sikushsuri wala siungi hoja.
Hili ni ambalo linafanywa hata na wanaume mm wake zangu wanazalishwa na madaktari wa kike na hiki unachokisema hakija tokea,kukosa umakini hakuzingatii jinsia ya dokta.
 
Back
Top Bottom