Serikali msijisahau katika hili la daktari kumtibia mtu wa jinsia tofauti na yeye

Serikali msijisahau katika hili la daktari kumtibia mtu wa jinsia tofauti na yeye

Kinachouma mama mzazi anaenda hospitali anakutana na daktari ambaye ana umri kama wa mimi mwanae alafu madaktari wa kike wapo kabisa.

Kuna mama wa kipemba wakati anajifungua alitaka kuja daktari wa kiume, basi mama mpemba akamuuliza "uko radhi kuchungulia tv ya mamayo wee "?

Daktari akaenda mbio
Nmecheka kweli....lkn unakuta hawa wadada hawako competent kwahyo,ili kuokoa uhai basi wakunga wa kiume wanakuja...japo Dah


Em niwaite wafamasia na madaktar hapa


Cc

Baba Swalehe Mwifwa
 
sababu ni kua hakuna athari yeyote impatayo mgonjwa endapo atahudumiwa na Dr wa jinsia tofauti na yake
Haiwezekani isiwepo athari kwa daktari kumhudumia mgonjwa wa jinsia tofauti alafu iwepo athari kwa polisi kumpekua mtu wa jinsiia tofauti.

Hii ni kutunza utu ndio maana polisi wa kike anamkagua wa kike,na wa kiume kwa wa kiume.

Sasa ukiniambia hakuna athari kwa nini katika upekuzi inazingatiwa jinsia alafu kule kwenye kuvua nguo hasa mtu anakuona isizingatiwe na kuvua nguo ni jambo kubwa kuliko huko kupekuliwa ?
unaposema kwanini itumike onyesha ulazima kwa kuweka vigezo na sio kutumia muktadha kutoka idara fulani iwe applied kwenye afya
Hivyo vigezo vya idara fulani pia ni katika kuonesha ulazima wa kutumia jambo hilo katika idara nyingine huwezi kukatenganisha mwanamke anaekaguliwa na polisi na huyu mwanamke anaetibiwa na daktari,hawa wote ni wanawake.

Tena huyu anaekaguliwa ilikuwa akaguliwe na mtu yeyote yule kwa sababu pengine ni mhalifu hivyo asizingatiwe sana,lakini hata kwa mhalifu kumbe jinsia inaheshimiwa vipi kwa mgonjwa tusihemshimu jinsia yake wakati kuumwa sio uhalifu.

Sikusudii kuwa mhalifu apekuliwe na polisi wa jinsia tofauti,bali nakusudia kuwa mgonjwa ana haki zaidi ya kuhifadhiwa ile jinsia yake kutokana na matatizo yake.
jinsia haina mchango wowote kupelekea mgonjwa kupona, kinachosababisha mtu kupona ni taaluma ya daktari
Ssahihi kabisa mkuu jinsia haina mchango wowote kwa mgonjwa kupona nakubaliana na wewe kama ambavyo upekuzi hauna mchango wowote wa mhalifu kukutwa na kitu ama asikutwe,anaweza akapekiwa na mwanaume lakini pia akipekuliwa na mwanamke akakutwa vile vile.

Na mimi sikusema ati kwa vile mwanamke basi avae koti akatibu hapana,nilichosema mimi kuwa wazidi kusomeshwa madaktari wa kike ili waje kuwa madaktari wasome vizuri zaidi.

Hii maana yake navunja ule mtazamo wako kuwa ati mimi ninachokiona kuwa jinsia ndo inatibu,jinsia haitibu kinachotibu ni elimu na utaalamu wa mtu.

Ila jinsia ichukue nafasi ya KUHIFADHI JESHIMA YA MTU KATIKA SIRI ZAKE ZA MAUMBILE kama ambavyo idara zingine zimaheshimu hili jambo na kwemye afya pia iheshimiwe.
kwani kipi ambacho hakina malalamiko?

kukiwa na watu ambao wanawalalamikia wenye mtazamo kama wako kua mmepotoka kwasababu kutibu mgonjwa kunahitaji taaluma na sio jinsia, utakubali kwa kigezo hicho kua umepotoka kwasababu watu wamelalamika?
Kwanza sijawahi kuwa na mtazamo wa kuwa kutibu mgonjwa kunahitaji jinsia huku ni kunakili kwako kimakosa mtazamo wangu na sikulaumu kwa sababu ndio ubinadamu sote tunapita humo.

Ndio maana nasisitiza sana kuwa hao wanawake pia wasomee huo udaktari kwa wingi ili tupate jinsia zenye elimu.

Kwa hyo hoja yangu sio jinsia basi hoja yangu ni JINSIA YENYE ELIMU ndio maana nasisitiza suala la wanawake kusoma.
kipi kinachokufanya uone upande ulioko wewe hauna
Ni kwa sababu baadhi ya kada kam vile katika ulinzi polisi wanazingatia hilo katika upekuzi.

Pia maeneo mbalimbali kuna kutenganishwa baina ya wanawake na waume hilo linanifanya nione kuwa ni sahihi kutenganisha zaidi katika suala la matibabu hasa yale yanayohusisha sehemu za siri za watu.

Kwa maana hiyo kuwepo kwa mtengano huu kunanifanya nione pia ni sahihi mtengano huo ukiwepo katika afya ikiwa wataalamu watakuwa wakutosha.
kuna walalamikaji wengi wanataka ndoa za jinsia moja zihalalishwe, kwa vigezo vyako ulivyotumia unaonekana unakubaliana na hili kundi

nipe sababu au vigezo vyenye kuonesha kila malalamiko dhidi ya jambo fulani basi jambo hilo sio sahihi na linatakiwa kufanyiwa kazi kama walalamikaji wanavyotak
Siwezi kukupa vigezo wala sababu kwa sababu sikusema kama ulivyosema wewe.

Sikusema kuwa kila malalamiko dhidi ya jambo fulani basi jambo hilo sio sahihi,sikusema hivi kwa hiyo siwezi kutoa sababu juu ya jambo ambalo sikulisema.

Umetoa mfano wa raisi nimekujibu kwa mujibu wa mfano wa raisi uliotoa ila wewe unaninukuu kwa ujumla wake wakati mfano wako sio wa jumla bali ni maalumu.

Hivyo siwezi kutoa sababu na vigezo juu ya jambo ambalo sijalidai.
ni kwasababu hizo ni protocols za upolisi sio udaktari
Hapa hatuangalii proroko tunaangalia sababu ya protoco.

Sababu ni kuheshimu jinsia ya pande ingine ndio maana hiyo protocol haivunjwi,sasa huku kuheshimu jinsia kunahitajika kwa kada zote sio polisi tu bali hata kwenye afya.

Kama ambavyo kuuliza tatizo kwa mgonjwa na kumhoji ni protocol za kidaktari lakini lengo ni kujua tatizo basi ndivyo hata polisi wanatumia protoco ya kuhoji mtuhumiwa na sio mgonjwa kwa lengo lile lile la lutaja kujua tatizo na mkosa ili kutatua shida.

Kwa hiyo suala sio protoco suala ni lengo la hiyo protoco,lengo lake kama linahitajika na sehemu zingine baasi lipitishwe pia itumike kwingine.
hii ni personal opinion, kwa polisi hata kama hayupo polisi wa kike zoezi la upekuzi haliwezi kukwama wakitaka kukupekua watamwita hata mpita njia yeyote wakike ilimradi tu awe na utimamu wa kiakili.
Sasa unaona kwamba suala la jinsia ni muhimu sana kiasi kwamba akiwepo polisi asiye na kigezo maalumu cha jinsia atatafutwa mtu mwingine ?

Au tunakubaliana na mimi kuwa wanawake wakisomeshwa na wakawa wengi madaktari basi inawezekana hili suala la jinsia kufanyiwa kazi ?

Hapo ishu ni kwamba mtu wa kiume kwa kiume,wa kike kwa kike.
Ukisema suala la elimu maana yake unakubaliana na mimi kuwa hao wanawake wasomeshwe sasa kwa wingi.
Sio rahisi
Hata mimi nakubali kuwa sio rahisi,ila INAWEZEKANA PIA.kwa sababu madaktari wa kike wapo.

Kwa hiyo sio rahisi lakini inawezekana.
ni sahihi ila ni ngumu kwa mazingira ya maisha yetu kuchagua daktari kama nyanya gengeni, wenzetu wame undergo unakuta kila familia ina daktai wao
Sasa nani kasema kuwa ni rahisi ndugu scars.hata mimi nakubali kuwa ni ngumu kama unavyoona wewe na ndiyo naama nikaja na mawazo yangu haya na nikasema huko juu hili sio suala la mwaka au miaka miwili.
hata kama sio kuokoa maisha ila mgonjwa hatakiwi kukosa huduma hata kama anaumwa jipu sehemu za siri
Sasa si nimetoa mfano mmoja tu,siwezi kumaliza mifano yote hapo.

Nakubaliana na wewe mgonjwa hatakiwi kukosa huduma ati kwa kuwa daktari wa kike hayupo,apatiwe huduma na mwanaume ili apone tatizo kwa sababu ndio hali tunayoishi nayo.
usiseme hivyo kwasababu watu hufanya yale wanayoyapenda kwa interests zao
Ninasema hivyo mzee,hata wanawake wanaweza kufanya wanayoyapenda kwa interest zao lakini kuna vikwazo wakipitia wanashindwa kufikia malengo yao.
halafu mara nyingi swala la udaktari linahusisha team ya watu zaidi ya wawili kwenye sensitive issues humo utakuta madaktari na manesi combined wanashirikiana. sasa ni ngumu kukuta daktari yuko ofisini anakula kiyoyozi haendi kutoa assist kwenye operation muhimu eti kwakua yupo mwenzake mwenye ujuzi kama wake
Ikibidi katika masuala sensitive kuwa wakusanyike kama tunavyoona katika operesheni kubwa kubwa basi hakuna shida kwa sababu ndio hali ilivyo japokuwa wakiwepo wataalamu wa kike nao pia inawezekana wakawepo team ya wataalamu wa kike tupu.
atasubiria kwa muda gani?
Asubiri mpaka watakapokuja,kama hawaji atapumzika.kama ambavyo daktari haendi kutafuta wagonjwa bali husubiri mpaka wakifika basi na yeye hivyo hivyo asubiri wafike.
unaelewa kila apartment ina wataalamu wao, na kila mtaalamu haruhusiwi ku interfere apartment ambayo hakusomea?

labda wanakuchanganya wale nurses unaowaona nyomi kila hospitali unahisi wote wanaweza kuzalisha, au kwasababu kuna watu wanazalia hadi nyumbani ndio sababu umemu-underrate Obstetricians
Ingekuwa nachanganya basi nisingekuja kusema humu kuwa madaktari wa kike au wataalamu ni wachache.

Kitendo cha mimi kuwaona manesi wengi na bado nikaona kuna tatizo katika upungufu wa madaktari wa kike hilo ni uthibitihso kuwa naelewa kazi ya manesi na wala hawanichanganyi.



MWISHO NIKIKUULIZA.

JE TUNAKUBALIANA KUWA ENDAPO MADAKTARI WA KIKE WATAKUWA WENGI NA WAKIUME WATAKUWA WENGI BASI HILI SUALA LA MATIBABU KWA KUZINGATIA JINSIA LINAWEZA KUFANYIKA ?
 
Wakuu naomba niipongeze serikali kwa jitihada zake inazofanya katika kuhakikisha ile heshima ya jinsia zote inalindwa.

Tukiangalia katika majeshi hasa jeshi la polisi utakuta kuna askari wa kike ambao kama itatokea muhalifu ni mwanamke basi askari yule hakuajiriwa kwa bahati mbaya bali hiyo itakuwa ni kazi yake kumpekua sehemu za mwili wake.

Hali kadhaalika mwanaume atapekuliwa na askari wa kiume katika kulinda heshima.

Hata mashuleni kuna waalimu wa kike kibao ambao wao watashughulikia masuala mbali mbali ya wanafunzi wa kike.

Mbona sioni suala hili la kuheshimu jinsia na kulinda heshima ya mtu likifanyika na kusisitizwa katika kada ya afya ?

Kwanini isiwe kosa daktari wa kumtibia mgonjwa wa jinsia tofauti na yeye ikiwa katika hospitali hiyo ama maeneo hayo kuna daktari mwenye jinsia sawa na mgonjwa ?

Kama ambavyo polisi haruhusiwi kumfanyia upekuzi wa mwili mtu wa jinsia isiyekuwa yake wakati wa jinsia yake wakiwa pale hii ni kosa,vipi isiwe kosa katika hii kada ya afya ?

Yani utakuta hospitali kuna madaktari wa jinsia nyingi lskini mwanamke anatibiwa na mwanaume au kinyume chake.

Serikali isomeshe watoto wengi wa kike ili kuja kuepusha hii aibu,ipunguze vigezo vya kusomea udaktari kwa mwanamke hasa kwa mambo ya kawaida haya ambayo hayahitaji kujitoa sana wanawake wasomeshwe waje kuzalisha wanawake wenzao.

Chumba cha kuzalisha kuna madaktari wa kike watano na wa kiume mmoja,huyu wa kiume anatafuta nini,kwa nini isiwe kosa kisheria?
Niliwahi kuhoji sababu ya kuwepo gynaecologist mwanaume afanye kazi ya kupekenyua nyuchi za dada, mama na wake zetu? Hii inakiuka maadili yetu ya kiafrika. Naunga mkono jinsia ya KE kupewa nafasi kusomea kozi za namna hii.
Ubarikiwe mleta mada hii.
 
Niliwahi kuhoji sababu ya kuwepo gynaecologist mwanaume afanye kazi ya kupekenyua nyuchi za dada, mama na wake zetu? Hii inakiuka maadili yetu ya kiafrika. Naunga mkono jinsia ya KE kupewa nafasi kusomea kozi za namna hii.
Ubarikiwe mleta mada hii.
Aameeen kwa sote pia mkuu.

Hapa kuna watu hawaoni shida kabisa mkuu wanaona sawa wakati sekta zingine hili suala linazingatiwa sana.

Uhaba wa madaktari wa kike ni katika sababu pia
 
Pendekezo lako ni lipi kwenye hiyo mikakati?
Mkakati upi huo ambao unaona haupo na ndio kikwazo?
Mikakati ni Mingi sana nadhani ni mada kando hiyo kwa muono wangu tumalize kwanza tunalojadili kisha tuje kwenye mikakati.

Mikakati iwepo ama isiwepo haibatilishi hoja yangu hii ambayo nimeianzishia uzi
 
Back
Top Bottom