Serikali msijisahau katika hili la daktari kumtibia mtu wa jinsia tofauti na yeye

Mbona kuna hospitali flani wamama wanaojifungua wanapendelea manesi wanaume kuliko wanawake. Tena asiwe mwanamke aliyefunga uzazi tiyari, "panuaa unajifanya kuumia kama vile sisi hatujazaa bhana".
 
Hivi umeelewa hoja ya mtoa mada?

Mtoa mada analalamika mgonjwa kutibiwa na dk asiye wa jinsia wa jinsia yake wewe unasema sheria zipo zinataka kama mgonjwa ni ke na dr ni me basi awepo na dr/nesi wa kike,sasa huyo nesi wa kike atazuia vp dr wa kiume kumchungulia mgonjwa?

Hio sheria kama ipo basi itasaidia unyanyasaji wakijinsia ila mambo mengine kama kuchungulia hio sheria itasaidia vipi?

Nikuulize swali,hivi endapo ikitokea mama wa dr wa kiume ni mjamzito je huyu dr wa kiume anaweza kumzalisha mama yake chini ya uwepo wa dr/nesi wa kike?

Kwavyovyote dr ataomba ma dr wenzake wamzalishe mama yake kwani kwa utamaduni wakiafrika sio heshima.

Sasa inakiwaje vi dr vidogo vinapata ujasiri wakuchungulia wamama wenye rika sawa na mama zao?
 
Hapo sio kwamba wameweza kwa sababu ni wanaume ati na wale wameshindwa kwa sababu ni wanawake no no.

Hao wameweza pengine kwa sababu wana ujuzi zaidi na uzoefu kuliko hawa wanawake.

Wanawake wanahitaji wafundishwe vizuri sana kwa utawi wa jamii.

Alafu pia kwa kesi kama yako wapo madaktari wa kike wazuri kwa kuzalisha hao walikuwa labda wamepanick au maarifa madogo,lakini sio kwamba ati walishindwa kwa sababu ati ni wanawake hapana
 
Unapotetea uhai unajali Mambo ya aibu?
Huu NI ujinga kabisa
Mbele ya kifo unasema naona aibu!!!!
Madaktari NI wachache kwanza lazima muelewe
Mkuu kama umekereka tusamehe bure.

Ila hapa tunakubali kuwa madaktari ni wachache na ndio maana haya yote yanatokea.

Ndio maana tukatoa suluhisho kuwa wanawake wasomeshwe ili kusudi sasa hao madaktari wawe wengi,usipanick mkuu haya ni mambo ya kawaida
 
Mkuu ili haya yasiwe madai tuwekee ushahidi hapa wa hayo uliyoyasema ili tupate faida isiwe inaishia kwemye kudai tu mkuu
 
Ilikuwaje hapo awali ambapo ma Dr wa kike hawakuwepo, mambo siku hizi wamebadilika, unaweza kukuta mama yako kazaa midume tu na uzee umemfika na siku hizi kupata wahudumu au wasaidizi wa kazi ni kazi .
 
Kwa nini polisi katika upekuzi kumpekua mtuhumiwa hutumiwa wanawake,mbona hata polisi mwanaume asitumike kumpekua mhalifu wa kike ?

Unaonaje juu ya polisi wa kiume kumpekua kila sehemu mtuhumiwa wa kike ?
 
Unapotetea uhai unajali Mambo ya aibu?
Mkuu hata polisi anapotetea usalama akitumia hoja hii kwamba usalama kwanza manake polisi wa kiume ana haki ya kumpekua mpaka mtuhumiwa wa kike kwa maslahi mapana ya taifa pengine kaficha mabomu hata sehemu za siri.

.kwa nini polisi wa kiume asitumie hoja ya usalama kumpekua mtuhumiwa wa kike ?
Mbele ya kifo unasema naona aibu!!
Manake tuhalalishe polisi mwanaume akitaka kumpapasa mtuhumiwa mwanamke kwa kumkagua,mtuhumiwa akikataa na kusema hiyo ni udhalilishaji huyu polisi anaweza kumuambia "mbele ya usalama unaona aibu ?".

Hapana swrikali yetu iangalie hili jambo kwa upana wake
 
Ilikuwaje hapo awali ambapo ma Dr wa kike hawakuwepo
Kwa hiyo hata wanawake ambao wangesomeshwa udaktari wakaja kupunguza wimbi hili hawakuwepo hao wanawake ?

Hao madaktari wa kiume kumbuka wamwtengenezwa,basi na hawa wa kike tuwatengeneze pia.
 
Mimi hupenda kuhudumiwa na dr mwanaume hayo ya utu uzima sijali, pia ukiwa na dr wakiume nurse wa kike lazima awepo same applies na kukiwa na Dr wa kike lazima nurse mwanaume awepo, so uoga kwenye kuumwa hauna mashiko
 
Umeongea ovyo uonekane unalogic kumbe hewa tu kama hujui miongozo ya udaktari uliza ndo uje jukwaani
 
Kumbuka tu
Mficha uch hazai
Mficha maradhi kilio kitamuumbua
 
Mimi hupenda kuhudumiwa na dr mwanaume hayo ya utu uzima sijali, pia ukiwa na dr wakiume nurse wa kike lazima awepo same applies na kukiwa na Dr wa kike lazima nurse mwanaume awepo, so uoga kwenye kuumwa hauna mashiko
Ulikuwa wap kumuelekeza ndugu yetu mpka anakurupuka ivooo
 
Hili ni ambalo linafanywa hata na wanaume mm wake zangu wanazalishwa na madaktari wa kike na hiki unachokisema hakija tokea,kukosa umakini hakuzingatii jinsia ya dokta.
Ina maana una wake wangapi?
Acha umalaya na wivu unao huku mwenyewe una Kijiji Cha wanawake
 
Mbona kuna hospitali flani wamama wanaojifungua wanapendelea manesi wanaume kuliko wanawake. Tena asiwe mwanamke aliyefunga uzazi tiyari, "panuaa unajifanya kuumia kama vile sisi hatujazaa bhana".
Wanawake tunapenda ma Dr na na nurse wa kiume, ukikutana na mwanamke ni roho mbaya tu hawajui kupet pet
 
mkuu,

unaongelea pumb* zipi? kama ni hizi hizi za kwetu omba zisikuume..maana maumivu yake hatari... hutojali jinsi wala umri wa doctor...
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwa hiyo hata wanawake ambao wangesomeshwa udaktari wakaja kupunguza wimbi hili hawakuwepo hao wanawake ?

Hao madaktari wa kiume kumbuka wamwtengenezwa,basi na hawa wa kike tuwatengeneze pia.
Hii unayo ongelea au kutamani ni option
Kama Dr unayemtaka yupo, la sivyo awe Mwanamke au Kiume utatibiwa naye, uki kata ni juu yako na afya yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…