Serikali mwangalieni kwa jicho kubwa meneja TRA wa Masasi

Serikali mwangalieni kwa jicho kubwa meneja TRA wa Masasi

hp4510

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Posts
7,235
Reaction score
7,392
Nimepata bahati ya kuja masasi kula sikukuu ya xmass na nimepata bahati ya kuongea na watu tofauti tofauti hasa wafanyabiashara

Asilimia kubwa ya wafanyabiashara ambao tumekaa na kuongea nao malalamiko yao makubwa ni kutoka kwa Meneja wa TRA Masasi

Huyu jamaa anazorotesha sana biashara kwa kuwafungia watu maduka yao, yani yale mambo ambayo Rais huwa anaagiza kuwa watu wa TRA waongee vizuri na wafanyabiashara ni gumu sana kwa huyu jamaa.

Nilishangaa kusikia mpaka waendesha bajaji na wao wanamchukia sana, anafunga bajaji zao na kuzivuta kwa gari.

Wafanyabiashara wengi wameanza kuondoka Masasi na kwenda mikoa mingine kutokana na usumbufu wa huyu meneja.

Najua Serikali inapita kwenye hili jukwaa basi fanyieni kazi malalamiko ya wafanyabiashara hawa wa Masasi.
 
Acha kumuonea mzee wa watu, hata kama wewe ungekuwa Meneja TRA ungefanyaje? huyo baba ako anataka mapato, jaribu kuingiziwa hata milioni 20 uone moto wake
 
Hujaweka wazi hizo biashara zinafungiwa kwa sababu zipi? kwanini unasema wanaonewa? ingekua vizuri zaidi kama ungeonana na huyo meneja pia nakumsikiliza kabla hujafungua hii thd,kesi hua haiamuliwi kwa kusikilizwa upande mmoja.
 
CCM ya leo haipendi wafanyabiashara. Nyie wafanyabiashara ni wapiga dili, na mkiendelea kupiga vuvuzela zenu hapa JF, tutawapeleka kwa DPP tukagawane Kati kwa Kati kile chote mlichonacho
 
Nimepata bahati ya kuja masasi kula sikukuu ya xmass na nimepata bahati ya kuongea na watu tofauti tofauti hasa wafanyabiashara....
Nilisema, humu TRA wanalikufuli lao wakifika hutia kufuli ,Wala sio masasi tu ndugu yangu nimeyashudia sehem tofauti hapa Tv.
 
Serikali inataka pesa sasa kama hawatoi kwa maongezi ifanyeje wakati kila siku wanafanya biashara..kumbuka tuna kimbizana kutekereza ilani.

#MaendeleoHayanaChama
 
Acha kumuonea mzee wa watu, hata kama wewe ungekuwa Meneja TRA ungefanyaje? huyo baba ako anataka mapato, jaribu kuingiziwa hata milioni 20 uone moto wake
Sio mzee huyo mzee unaemsema ameshastaafu
 
Serikali inataka pesa sasa kama hawatoi kwa maongezi ifanyeje wakati kila siku wanafanya biashara..kumbuka tuna kimbizana kutekereza ilani.

#MaendeleoHayanaChama
Tofautisha kufanya biashara na kufungua maduka
 
Na wewe pia una matatizo. Huwez kusikikiza upande mmoja tu wa wafanyabiashara halafu unapata hoja za kuleta humu. Maliza kula sikukuu uondoke urudi kwenu utuachie masasi yetu.
Ndio maana nimesema serikali iangalie
 
CCM ya leo haipendi wafanyabiashara. Nyie wafanyabiashara ni wapiga dili, na mkiendelea kupiga vuvuzela zenu hapa JF, tutawapeleka kwa DPP tukagawane Kati kwa Kati kile chote mlichonacho
Then ww na familia yako unapata faida gani
 
Maagizo kutoka juu ndio ya kulaumiwa.
1609185287097.png
 
Hii ndiyo serikali ya awamu ya tano bana

Watu mlizoea kuishi maisha ya mazoea mazoea ya kukwepa kodi sasa Mzee JPM amemleta mtu awashughulikie vizuli vizuli
Nani alikwambia watu hawataki kulipa kodi.? Nani kakwambia watu wanakwepa kodi? Serikal lazima i consider ukusanyaji kodi bila kuumiza source ambayo ndio wafanya biashara. Wakifunga biashara hizo kodi zinatoka wapi? Shut your hole dumb niga. Think twice
 
Back
Top Bottom