Serikali na CCM walivyo na sikio la kufa lisilosikia dawa, tayari wanataka kuanzisha vita nyingine kubwa na hatari zaidi na Kanisa la Mungu

Serikali na CCM walivyo na sikio la kufa lisilosikia dawa, tayari wanataka kuanzisha vita nyingine kubwa na hatari zaidi na Kanisa la Mungu

Uzima Tele

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2023
Posts
1,270
Reaction score
2,822
Ni hatari sana..

Kuna kila dalili kuwa, baada ya tamko la Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC), vita ya skandali la bandari inakwenda kuchukua sura nyingine kati ya kikundi kilichomo ndani ya serikali kilichotengeneza uchafu huu na Kanisa la Mungu.

Na bila shaka TEC imetangulia tu na muda si mrefu The Christian Council of Tanzania (CCT) na The Council of Pentecostal Churches of Tanzania (CPCT) nao wanakuja na matamko yao na misimamo yao na tunafikiri yatakuwa ni matamko ya namna gani?

Obvious ni kuukataa mkataba huu kwani kwa sababu ziwazo zote, hakuna mtu yeyote mwenye akili timamu na hajahongwa anaweza kukubaliana na ujinga na uchafu huu unaoitwa IGA kati ya Dubai Emirate na Tanzania.

Kama Rais Samia Suluhu Hassan akishindwa kutumia fursa hii kwa serikali yake kurudi kwenye drawing board ili kufikiria namna sahihi, ya wazi na shirikishi kwa umma ya ubia (partnership) ya uboreshaji wa bandari zetu badala ya njia hii ya mkataba huu mbovu na Dubai kupitia kampuni yao ya DP World, basi awe tayari kuanza kuitumikia hukumu yake yeye na watu wake wote walio nyuma ya scandal hii.

Ni hukumu yake kwa sababu dalili zinaonesha kuwa hiki kikundi baada ya mara ya kwanza kufanikiwa kumshawishi Rais na kwa baraka zake mwenyewe akajiruhusu kujiingiza kwenye shida na aibu hii, basi mission ya kundi hili haijakamilika na linakwenda tena kwake (Rais Samia) na anaweza kutoa baraka zake tena ili kuanzisha vita na kanisa la Mungu wakidhania watafanikisha malengo yao maovu..

Hili likitokea, basi itakuwa ni heri ya wapiganiao haki maana hakuna mamlaka ya serikali yoyote ya kidunia imewahi kushindana na Kanisa la Mungu na mamlaka hiyo ikasimama na kushinda. Tunayo mifano mingi ktk historia ya Biblia kama vile Babeli ya kale, dola la Rumi ya kale, Misri ya Farao nk.

Rais Samia Suluhu Hassan, za kuambiwa changanya na za kwako mama. Wewe ni mwanamke, usiingie ktk historia ya wanawake viongozi wa hovyo waliowahi kuongoza nchi zao na kutoka kwa aibu.
 
IMG_20230817_195814_019.jpg
 
Duh

Kwani Hii ni mara ya kwanza Kanisa kutoa matamko?
Ni mara nyingi na mara zote serikali huwa haisikii na huanzisha ugomvi na kanisa...

Na matokeo ya serikali kutosikia sauti ya Mungu toka Kwa wawakilishi wake hapa duniani tunayaona ktk maisha yetu ya Kila siku, laana ya umasikini uliokithiri, magonjwa, ujinga na Kila aina ya uovu kutamalaki...

Unataka tuendelee kuwa upande huo na sasa?
 
Maslahi yakiguswa mahali kuna tonge na unawapokonya basi tegemea kelele za aina zote

Goods exempt from tax zilianza miaka yaani kabla hata ya Uhuru

Ila kuna watu wanaitumia vibaya wanaingiza kila kitu kupitia bandari wakisingizia msamaha wa Kodi.

Humo humo wanatakatisha na hela haramu.

Kila mmoja alipe kodi na tuache wizi na kujiita wapenda nchi na rasilimali zake huku kuna maslahi binafsi
 
Raisi yupo Kimya si atoke aongee aisee..... Haoni hili Giza Lilo likumba Taifa yeye amenyamaza tu
Mkubwa, hii ndiyo shida ya nchi kupewa mwanamke aongoze..

Kwa mfumo wa kisheria na kikatiba wa nchi hii, kumpa nchi mwanamke ni uharibifu mkubwa na ndiyo maana ya madudu haya tunayoyaona sasa..

Si yeye anaongoza nchi. Lipo jamaa au mijamaa fulani mahali inayom - remote na kumdhibiti aseme nini, wakati gani, wapi na kwanini. Na ni hatari sana kama kweli ni wajomba zake wa uarabuni ndiyo wako ndani ya ikulu yetu..!!

Hawawezi
 
Kinachotafutwa hapa ni vita ya udini baada ya kuonekana ya uzanzibari vs utanganyika umeshindikana,, Mungu bado anaipenda Tanzania tuendelee kuiombea,,
Sasa tunasubiria na Bakwata watoe Tamko hawa huku wale kule Tukutane kati kati
 
Ni hatari sana..

Kuna kila dalili kuwa, baada ya tamko la Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC), vita ya skandali la bandari inakwenda kuchukua sura nyingine kati ya kikundi kilichomo ndani ya serikali kilichotengeneza uchafu huu na Kanisa la Mungu..

Na bila shaka TEC imetangulia tu na muda si mrefu The Christian Council of Tanzania (CCT) na The Council of Pentecostal Churches of Tanzania (CPCT) nao wanakuja na matamko yao na misimamo yao na tunafikiri yatakuwa ni matamko ya namna gani?

Obvious ni kuukataa mkataba huu kwani kwa sababu ziwazo zote, hakuna mtu yeyote mwenye akili timamu na hajahongwa anaweza kukubaliana na ujinga na uchafu huu unaoitwa IGA kati ya Dubai Emirate na Tanzania...!!

Kama Rais Samia Suluhu Hassan akishindwa kutumia fursa hii kwa serikali yake kurudi kwenye drawing board ili kufikiria namna nyingine ya ubia wa uboreshaji wa bandari zetu badala ya mkataba huu mbovu na Dubai kupitia kampuni yao ya DP World, basi awe tayari kuanza kuitumikia hukumu yake yeye na watu wake wote walio nyuma ya scandal hii..

Ni hukumu yake kwa sababu dalili zinaonesha kuwa hiki kikundi baada ya kumshawishi Rais na Kwa baraka zake kinakwenda kuanzisha vita na kanisa la Mungu..

Hili likitokea, basi itakuwa ni heri ya wapiganiao haki maana hakuna mamlaka ya serikali yoyote ya kidunia imewahi kushindana na Kanisa la Mungu na mamlaka hiyo ikasimama na kushinda. Tunayo mifano mingi ktk historia ya Biblia kama vile Babeli ya kale, dola la Rumi ya kale, Misri ya Farao nk..

Rais Samia Suluhu Hassan, za kuambiwa changanya na za kwako mama. Wewe ni mwanamke, usiingie ktk historia ya wanawake viongozi wa hovyo waliowahi kuongoza nchi zao na kutoka kwa aibu...
Bado na SDA council wanakuja.
 
Ni mara nyingi na mara zote serikali huwa haisikii na huanzisha ugomvi na kanisa...

Na matokeo ya serikali kutosikia sauti ya Mungu toka Kwa wawakilishi wake hapa duniani tunayaona ktk maisha yetu ya Kila siku, laana ya umasikini uliokithiri, magonjwa, ujinga na Kila aina ya uovu kutamalaki...

Unataka tuendelee kuwa upande huo na sasa?
Nenda China uone kama kuna huo upuuzi wa makanisa
 
Maslahi yakiguswa mahali kuna tonge na unawapokonya basi tegemea kelele za aina zote
Goods exempt from tax zilianza miaka yaani kabla hata ya Uhuru
Ila kuna watu wanaitumia vibaya wanaingiza kila kitu kupitia bandari wakisingizia msamaha wa Kodi
Humo humo wanatakatisha na hela haramu
Kila mmoja alipe kodi na tuache wizi na kujiita wapenda nchi na rasilimali zake huku kuna maslahi binafsi
Kwa hiyo unataka kusema nini?

Je, una maana kuwa hii ni sababu ya uhalali wa IGA au mkataba huu wa waarabu wa Dubai kupitia kampuni yao ya DP World..??

Yaani ili kudhibiti mifumo ya kutakatisha pesa haramu bandarini, mipakani, vuwanja vya ndege au ukwepaji Kodi unahitaji kuleta mwekezaji toka Ulaya au Uarabuni..?

Unajua unasema nini kweli wewe?

Kama tunahitaji uwekezaji wa wazungu wa Ulaya au waarabu wa Dubai kudhibiti utakatishaji wa pesa na ukwepaji kodi kwenye bandari zetu au viwanja vyetu vya ndege, na mipaka ya nchi yetu nk, basi mahali sahihi pa kuweka mwekezaji wa Ulaya au Dubai ni ikulu yetu, bunge letu na mahakama zetu na idara ya polisi na TISS...!

Ukiona taasisi za serikali zinashindwa kutekeleza wajibu wake kikatiba na kisheria ili kusimamia haki na ustawi wa wananchi wote kiuchumi na kijamii, tambua kuwa serikali iliyopo madarakani itakuwa imesha - compromise na uovu na yenyewe hiyo kuwa ndio uovu huo na hivyo inakuwa imeshindwa (failed) na inapaswa kuondolewa kwa hiari au kwa nguvu..!
 
Back
Top Bottom