Hofu kubwa imetanda kwa Wananchi wa Kijiji cha Mbatakero, Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro kutokana na uvamizi unaofanywa na wafugaji wa Kimasai kwa Wakulima Maskini wa kijiji hiki huku uongozi wa kijiji hasa Mwenyekiti ukishutumiwa kupokea rushwa kutoka kwa hawa wafugaji ambao ni wageni eneo hili. Mazao ya Wakulima yanavamiwa na mifugo, wanapigwa, wanajeruhiwa lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa.
Siku za hivi karibuni, mifugo imekuwa ikivamia na kuharibu mazao ya Wakulima na pale Wananchi hawa wanapochukua hatua za kwenda kituo cha polisi, Mwenyekiti huyo anawatishia na kuwakatisha tamaa na huwa anafanya juhudi za kuwatetea hawa wafugaji waharibifu.
Kama haitoshi Wananchi wengi wamejeruhiwa hadi kulazwa hospitali na kila wakienda kuripoti matukio haya Kituo cha Polisi Bomang'ombe hakuna msaada wowote wa Kipolisi wanaoupata, wakati mwingine inasemekana, Polisi wa hiki kituo hupokea rushwa kutoka kwa hawa Wafugaji na pale waathirika wanapofuatilia kesi zao kwa wapelelezi, wanakatishwa tamaa na kushawishiwa na hawa wapelelezi kuwa warudi nyumbani wakaelewane na watuhumiwa.
Hadi wakati huu ninapoandika hapa, Wananchi zaidi ya nane ndani ya miezi miwili, wamevamiwa na mifugo ya mfugaji mmoja kwenye Vitongoji ziwili katika kijiji hiki, mazao yao yakaharibiwa, wengine wakapigwa, wengine wakajeruhiwa vibaya hadi kulazwa Hospitali ya Wilaya ya Hai.
Walipoenda Polisi walichukuliwa maelezo wakapewa PF 3 na RB lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na Jeshi la Polisi kuwakamata, ama kuwahoji wahalifu, badala yake inasemekana huyu mmiliki wa mifugo hii amekuwa akifika kituo cha polisi na kutoa rushwa ili asikamatwe ama kuhojiwa, kwa kuwa Wananchi wanamtuhumu mkuu wa kuti kuwa huyu Bwana ni rafiki yake.
Mathalan, Mnamo 05/06/2025, Vijana wa huyu jamaa walipeleka mifugo ikala na kuharibu mazao ya Renalda Mushi wa Kitongoji cha Kinamiri, huyu mama alipoanza jitihada za kufukuza mifugo, Vijana hawa walimpiga na kumjeruhi kwa sime, fimbo na mawe.
Alipoenda kutoa taarifa Kituo cha Polisi Bomang'ombe aliwataja waliomjeruhi na ushahidi ulikuwa waziwazi.
Hadi naandika ujumbe huu, hakuna hatua yoyote iliyowahi kuchukuliwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Bomang'ombe ili kumsaidia mama huyu pamoja na kwamba alijeruhiwa vibaya na kulazwa Hospitali ya Wilaya ya Hai.
Polisi walichofanya ni kumpatia RB NO. BOM/RB/1939/2025, Mama huyu baada ya kupona, huyu jamaa alimfuata na kumwambia anaomba amsamehe na kwamba atamchinjia Mbuzi, lakini huyu mama alimwambia hataki hata kumwona nyumbani kwake, na anadhamiria kurudi polisi kufuatilia shauri lake. Ndipo huyo jamaa (Mlimili wa mifugo) alipomwambia hata akienda huko hatapata haki yake kwa kuwa tayari keshaziba njia zote.
Katika kipindi hichohicho, alijeruhiwa pia ndugu Ombeni Lema ambaye alikuwa anafanya juhudi kuzuia mifugo ya huyu jamaa isiendelee kuharibu mazao yake. Naye alijeruhiwa vibaya na kutibiwa Hospitali ya Wilaya ya Hai, akabaki na RB yake na hakuna hatua zozote ambazo zimewahi kuchukuliwa na jeshi la polisi zaidi ya vitisho hakuna anayeweza kumkamata hapo kituoni Bomang'ombe.
Kama haitoshi, Mwenyekiti wa Kitongoji kimojawapo kiitwacho Mlimafaru kinachounda Kijiji hiki, naye amewahi kuvamiwa na mifugo ya huyu bwana ikiwa inachungwa na vijana wawili, katika harakati za kuifukuza hiyo mifugo alipigwa na kujeruhiwa na hao vijana.
Naye alikata RB Kituo cha Polisi Boma na aliwataja kwa majina Vijana waliomshambulia, akatibiwa na hadi leo hajakaa vizuri kiafya, wakati anafuatilia ili sheria ichukue mkondo wake, Mwenyekiti na kijiji hicho, akamtishia kuwa,hata akirudi polisi hawezi kusaidika lolote bora amalizane na Bwana anayetembeza rushwa.
Hadi leo hakuna aliyekamatwa, wala kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo. Ikawa ni utamaduni wa kupiga, kujeruhi na kuharibu mazao ya wananchi huku serikali ya kijiji ikiwa kimya na wakati mwingine kufanya juhudi za kuficha uovu na kuwatetea waharibifu wa amani.
Haikuishia hapo, wakulima waliendelea kuvamiwa na makundi makubwa ya mifugo hii na kuharibiwa mazao yao,wao wakiishia kupigwa, kutishiwa na kujeruhiwa, na hawajawahi kuchukuliwa hatua zozote.
Tarehe 09/08/2025, majira ya asubuhi, mifugo hiyo hiyo ya huyu bwana ikiwa inachungwa na vijana wawili ilivamia shamba la Bwana mmoja aitwaye Tadei, ikala majani ya mahindi na mahindi kwa pamoja. Huyu Bwana alipopewa taarifa, akamchukua Mwenyekiti wa Kitongoji na kwenda kuokoa mali yake.
Alipofika, hawa vijana walimshambulia yeye, mwenyekiti wa kitongoji na dada yake aitwaye hadi kupelekea majeraha makubwa. walikimbizwa hospitali ya Wilaya ya Hai na kupatiwa matibabu, lakini mmoja alikuwa ameumizwa sana kicwani na kenye mbavu kiasi cha kupelekea kushonwa na kulazwa hositalini hapo hadi tarehe 15/08/2025.
Tadei mwenye namba za simu ndugu zake wengine walitoa taarifa kituo cha polisi Bomang'ombe na wakapewa RB No. BOM/RB/2711/2025 (Shambulio la Mwili) na BOM/RB/2720/2025 (Kuharibu Mali). Mpelelezi wa kesi hii alikuwa afande Rashid wa kituoni hapo. Huyu mpelelezi akaomba Tadei na wengineo washirikiane naye ili kuwatambua na kuwakamata watuhumiwa.
Hawa ndugu wakarudi kijijini(umbali wa km 25) kutoka kituoni, wakalazimika kupita kwa uongozi wa Kitongoji ili kupata taarifa zitakazoweza kusadia wahalifu kukamatwa. Mwenyekiti wa Kitongoji akakiri wazi kuwa anawafahamu vijana waliovamia na kujeruhi kwa sababu anawaona, na anamfahamu mmiliki wa hiyo mifug.o, na kwamba wakati hizo vurugu zinatokea alimpigia mwenyekliti wa kijiji kumjulisha hali hiyo, lakini mwenyekiti akasema kwa kuwa mifugo imeshajulikana mwenyewe isizuiwe, aichwe iende. Ikawalazimu hawa ndugu waongozane na Mwenyekiti wa kitongoji kwenda kuomba ushirikiano kwa Mwenyekiti wa Kijiji.
Kufika nyumbani kwa Mwenyekiti wakamweleza kuhusu hali iliyotokea na majeruhi waliopo hospitali, na kumuomba mwenyekiti huyo wa kijiji atoe ushirikiano utakaopelekea wahalifu kukamatwa. Cha kustaajabu huyu Mwenyekiti alipiga simu kituo cha Polisi Bomang'ombe na kusema amevamiwa na ndugu wa wale majeruhi wa mchana, hivyo anahitaji msaada wa haraka. Mmoja wa ndugu hao naye akampigia simu mpelelezi afande Rashid na kumweleza hali hiyo,afande akashauri hao ndugu waondoke wakapumzike, huyo mwenyekiti ataiwa kituoni.
Baada ya hapo hadi naandika malalamiko haya, hakuna mtuhumiwa yeyote aliyekamatwa wala kuhojiwa na jeshi la polisi Bomang'ombe, Tadei amekuwa akienda kituoni kila siku kuulizia hatua zilizochukuliwa lakini hakuna jibu la maana alilopewa. Ni maajabu kuwa, Huyo mmiliki wa hiyo mifugo alienda kituoni jumanne tarehe 12/08/2025, akaonana na vigogo wa hapo na akaondoka bila kuhojiwa, wala kukamatwa ili awapeleke vijana wake wawili waliojeruhi na kuharibu mali.
Taarifa zinaelezaa kuwa, Mwenyekiti wa kijiji alifanya jitihada za kumjulisha mtuhumiwa siku hiyo ya uharibifu usiku akahamisha mifugo yake kwenye Boma alilokuwa anawalaza na kuhamishia sehemu nyingine ili kuudhoofisha ushahidi.
Baada ya huyo mtuhumiwa kutoka kituoni, Mwenyekiti wa kijiji naye alienda kituoni na inasemekana kuwa aliagizwa ampeleke mtuhumiwa (Maigizo) lakini hadi sasa hajafanya hivyo.
Mgonjwa aliyejeruhiwa tarehe 09/08 ameruhusiwa tarehe 15/08, lakini jeshi la Polisi kiuto cha Bomang'ombe hakijakamata wahalifu waliofanya uhalifu hao ingali wanajulikana na kila mmoja. Juhudi zinazofanyika sasa kuficha kwa nguvu uovu huu kama kawaida ndio maana wananchi tunaiomba serikali, jeshi la polisi ngazi za juu na TAKUKURU watusaidie kuondoa huu uovu.
Jitihada zimefanywa na baadhi ya wananchi kumpata mkuu wa Wilaya ya Hai lakini ziligongwa mwamba mapema, vile vile tumehangaika kumfikia RPC mkoa wa Kilimanjaro lakini alikuwa kwenye Semina huko CCP Moshi, alitumiwa malalamiko haya kwenye simu yake ya Whatsap lakini hadi naandika ujumbe huu alikuwa hajajibu chochote.
Wananchi wameamua kuanza kuhamasishana kujilinda wao, mali zao na afya zao kutokana na kukosa usaidizi wa uongozi wa serikali ya kijiji na jeshi la Polisi Bomang'ombe. Wamehangaika kutoa taarifa kwenye vyombo vya habari lakini baadhi ya vyombo (Moshi Fm Radio na Boma Hao Fm) wamekaa kimya pamoja na kuombwa na wananchi wawasaidia kupaza sauti ili viongozi wa ngazi za juu wasikie kilio chao na kuwasaidia.
Kilichobaki sasa wananchi wanajikusanya wafanye maandamano ya amani kwenda kwa mkuu wa wilaya na kituo cha Polici Bomang'ombe ili sauti zao zisikike. Wasiwasi wao wanaweza kupigwa, kujeruhiwa na hata kuwekwa ndani kwa kuwa wanaolalamikiwa ni serikali ya kijij na kituo cha polisi Bomang'ombe. Wanaomba uongozi uisikie sauti yao sababu wanahasira dhidi ya wanaowafanyiwa maovu na hawachukuliwi hatua.
Jana tarehe 15/08/2025 mifugo hiyo hiyo ya mtuhumiwa imevamia tena shamba la mpunga la mkulima mdogo kwenye kitongoji cha Kinamiri, vijana hao hao waliumiza na kujeruhi watu wiki hata haijaisha, wamejeruhi wengine na kumtukana vibaya Mwenyekiti wa Kitongoji. Hii ndiyo kiburi ya rushwa, haya ndiyo madhila wanayofanyiwa wananchi wa Kijiji hiki cha Mbatakero kilichopo wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro umbali wa Km 20 tu kutoka ilipo ofisi ya mkuu wa wilaya, Km 6 pekee kutoka eneo la Kwasadala.
Wananchi wanaogopa kutoka taarifa kituo cha Polisi Bomang'ombe kwa sababu hawapati msaada woeote wa maana, tena wengi wao wanasema kabisa huyu mtuhumiwa ukimpeleka polisi unapoteza muda wako bure na hela, hivyo wengi wamebaki na maumivu mioyoni, wanajipanga kujitetea.
Serikali yote ya kijiji ni ya Chama cha Mapinduzi, hadi sasa hakuna hatua zozote ambazo zimechukuliwa na chama kunusuru hali hii, Mwenyekiti alivamiwa, akapigwa, akaumizwa na mazao yake yakaharibiwa, hakuna hatua zozote srikali ya kijiji imechukua, wala chama. Badala yake huyo Mwenyekiti wa kijiji ameanza kampeni za kuzikataa baadhi ya familia zinazokataa maovu kuwa sio sehemu ya kijiji chake. Anawapiga vita na anaapa ya kuwa hizo familia atazifukuza kwenye kijiji chake. Sijui ametumwa na serikali ipi. Kuna wazee hapo aliwakuta alipotoka huko Machame na kuhamia kijiji hicho, hata alipokuwa upinzani(CHADEMA) wazee hawa walikuwa wanakitetea CCM kwa gharama za damu zao,leo hii amepokea rushwa(tuhuma) anataka kuwahamisha wazawa ili abaki na wageni waharibifu?
Hakuna kikao cha wananchi kimewahi kufanyika kuwakataa wananchi wenzao kwenye kijiji hicho,wala hakuna kikao ambacho kimewahi kuwakaribisha wageni wafugaji kwenye kijiji hicho.Ni ubabe umetamalakai kama vile wananchi hawa hawako Tanzania.
Ni maombi yetu wananchi wa kijiji hiki kuhakikisha serikali ngazi za juu,Jeshi la Polisi na TAKUKURU wanaingilia kati kuwanusuru wananchi hawa dhidi ya wahalifu wanaolindwa na mamlaka za serikali ya kijiji na jeshi la Polisi Bomang'ombe. TAKUKURU Mkoa na Wilaya ya Hai hatujaweza kuwapata wachunguze swala hili kwa sababu ni wazi kuna dalili za Rushwa kwa mamlaka za serikali ya mtaa, ama kituo cha Polisi Bomang'ombe
View attachment 3442986
Naambatanisha baadhi ya picha za majeruhi, na baadhi ya video zilizorekodiwa wakati wa tukio la tarehe 09/08/2025 na mengineyo.