Serikali na wadau Wana muongozo Gani juu wagonjwa na watu wa namna hii?

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
11,208
Reaction score
20,517
Kuna familia ipo jirani na Mimi,ni familia duni Kwa kweli, mke na mume walikuwa watu wa vibarua vibarua TU

Sasa limetokea tatizo Baba amepata stroke, mwili umepooza ni mwaka wa nne huu , akiwa hapo hapo kitandani akapata tena shida ya macho na Sasa macho hayaoni mke ndo anamuuguza Kwa maisha ya kuunga unga maana hana shughuli maalumu ya kumuingizia kipato

Watoto Bado ni wadogo hawajaanza kujitegemea Bado, Labda wangetoa msaada Kwa baba Yao na mama yao

Kiukwelii hali na mazingira yanatia simanzi Sana ukiona Kwa macho., ni familia ambayo inaishi Kwa tabu sana pasipokujua watakula Nini kila panapokucha

Ni vizuri pia serikali ikaangalia ni Kwa namna gani watu kama Hawa wanasaidika Kwa matibabu nk.
 
Labda wasaidie ku report kwa viongozi... ila pole sana kwao
 
Nashauri wamtafte Dr. Isaac maro wa Njia panda Clouds ili awasaidie kupata msaada wa hali na mali
 
Kuna familia ipo jirani na Mimi,ni familia duni Kwa kweli, mke na mume walikuwa watu wa vibarua vibarua TU

Sasa limetokea tatizo Baba amepata stroke, mwili umepooza ni mwaka wa nne huu , akiwa hapo hapo kitandani akapata tena shida ya macho na Sasa macho hayaoni mke ndo anamuuguza Kwa maisha ya kuunga unga maana hana shughuli maalumu ya kumuingizia kipato

Watoto Bado ni wadogo hawajaanza kujitegemea Bado, Labda wangetoa msaada Kwa baba Yao na mama yao

Kiukwelii hali na mazingira yanatia simanzi Sana ukiona Kwa macho., ni familia ambayo inaishi Kwa tabu sana pasipokujua watakula Nini kila panapokucha

Ni vizuri pia serikali ikaangalia ni Kwa namna gani watu kama Hawa wanasaidika Kwa matibabu nk.

Poleni,
Kwenye vituo vya afya hasa vya serikali kuna afisa usitawi wa jamiii/social welfare. Hatua za kuchukua ni kuwahusisha viongozi wa mtaa/kitongoji ili waweze kufatilia kwa muunganiko wa wewe, viongozi na afisa usitawi kwa upande wa tiba. Kuna mpango wa kunusuru kaya maskini/TASAF, ingawa ni jambo la kufatilia na kujua utekelezaji wake kwa eneo husika, ila uvumilivu ni muhimu kwa suala husika au masusla ya kiserikali.

Huwa kuna uzito, mlolongo na kuhitaji kusimamia kwa karibu kutokana na viongozi wengi kutokuwa pro-active.

Pia, kuangalia kuweza kutambua ndugu na jamaa ili kuwahusisha. Tumekuwa na kasumba ya sisi ndugu kujipoteza wakati mwanandugu anaumwa. Siku akipoteza uhai, unaona Vx zinakuja na watu kushika tenda za jeneza au chakula kwenye msiba au usafiri. Tubadilike.

Majirani na marafiki wema pia wanayo nafasi ya kutenda kwa kadri watakavyowiwa kwa kuanzia. Dunia ni mapito yetu sote.
 
Kwa dunia ya Leo majirani na marafiki ni wachache sana hasa unapokuwa katika wakati mgumu
 
Kuna familia ipo jirani na Mimi,ni familia duni Kwa kweli, mke na mume walikuwa watu wa vibarua vibarua TU

Sasa limetokea tatizo Baba amepata stroke, mwili umepooza ni mwaka wa nne huu , akiwa hapo hapo kitandani akapata tena shida ya macho na Sasa macho hayaoni mke ndo anamuuguza Kwa maisha ya kuunga unga maana hana shughuli maalumu ya kumuingizia kipato

Watoto Bado ni wadogo hawajaanza kujitegemea Bado, Labda wangetoa msaada Kwa baba Yao na mama yao

Kiukwelii hali na mazingira yanatia simanzi Sana ukiona Kwa macho., ni familia ambayo inaishi Kwa tabu sana pasipokujua watakula Nini kila panapokucha

Ni vizuri pia serikali ikaangalia ni Kwa namna gani watu kama Hawa wanasaidika Kwa matibabu nk.
Lucas Mwashamba na Gilbert Masawe saidieni huyu Mtanzania
 
Back
Top Bottom