Kevzy
JF-Expert Member
- May 23, 2026
- 976
- 1,712
Kwenu Serikali, mliyempa kandarasi ya kujenga dalaja hilo tajwa hapo juu naomba mumshupalie alimalizie, na kama mnalirekebisha ninyi wenyewe naomba mfanye haraka kulimalizia, limalizieni au lirekebisheni haraka
Kama wewe ni mkazi wa Kimara utaelewa nazungumzia nn! Simu yangu kiswaswadu nimeshindwa kuchukua picha
Hili daraja kama wameliongezea ngazi za kupanda juu upande wa kulia/kushoto ukitokea kulia na kushoto ukitokea kulia, sijui kama mmenielewa , aliyekuwepo karibu atusaidie picha kwenye Uzi hii
So huu upande ambao wanauunganisha uwe nao upande wa kupanda kuelekea juu Ili kuvuka daraja au kwenda kwenye mabasi na kituo Cha mwendokasi, hawajaunalizia na kuhatarisha watu ambao sio waelewa wanaoutumia hivyo hivyo, sio kila mmoja wetu muelewa wengine kidogo M/Mungu atuongoze
So ule upande haujawekwa nguzo za pembeni ambazo zinaweza kumkinga mtu kuanguka, pamejengwa tu ngazi za kupanda juu ila hawajamalizia nguzo za pembeni na si zani kama budget itagharimu hata milioni 5 au 6 kwanini hamlimalizii na watu wanatumia hivyo hivyo ni hatari sana na mnaona na kufahamu
Naomba mlimalizie, tena haraka iwezekanavyo
Watu wa njombe, Arusha, morogoro, singida,Dodoma, mbeya , iringa na pande zingine za Tanzania ambao hawajawahi kufika dar hawajui nazungumzia nn? Mtatumiwa picha hapa na modereta
Hii ni kero na naomba iangaikiwe haraka.
Pia soma ~ Daraja la Kimara Mwisho lawekewa kingo