sajo
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 3,474
- 6,195
Ni zaidi ya miaka 5 sasa toka Rais JPM alipoagiza Wizara zote za Serikali kuhamia jijini Dodoma yalipo makao makuu ya nchi. Agizo la rais ni sheria, hibyo lilitekelezwa kwa ukamilifu na sasa Wizara karibu zote zimehamia Dodoma ambapo zina majengo katika mji wa serikali Mtumba.
Kwa miaka yote hiyo zaidi ya 5, majengo yaliyokuwa yakitumiwa na wizara hizo jijini Dar es Salaam yamebaki wazi, hayatumiki na yamekuwa kama magofu. Maana nyumba isiyotumika ni lazima ichakae.
Sasa basi ninaona ni muda muafaka, serikali ipangishe majengo haya kwa bei nafuu ili vijana wengi wanaojiajiri wapate ofisi wajiongezee thamani kwa kazi zao na pia wajipatie kipato.
Tunajua kuwa ofisi ni anuani, mteja anakuwa na amani akifanya kazi na mtu ambaye anakua na ofisi. Wekeni viwango hata vya Tshs. 10,000/= kwa skwea mita, mtakua mmetatua tatizo la ajira, mtakua mmeinua vijana na wakati huohuo mtaongeza chanzo cha mapato (kodi).
Kuna majengo kama lile lililokuwa likitumiwa na Wizara ya Katiba na Sheria lenye takribani ghorofa 10 hali yake kwa sasa inasikitisha, vioo vinavunjika, madirisha hayafungi ilhali lilikuwa ni jengo zima kabisa.
Pangisheni lile. Na pale ofisi za Takwimu yalipokua makao makuu ya NIDA kuna jengo limechoka vibaya kwa sasa lakini zamani lilikua vyema kabisa, pangisheni. Hata pale ilipokuwa wizara ya Kazi, jengo limebaki tu. Fanyeni hivyo kwa majengo yote yaliyobaki wazi na yanaendelea kuchakaa.
Tunaomba serikali mlifanyie kazi hili, kama mtakosa nguvu kazi ya kusimamia, niteueni mimi nifanye kazi hiyo, majengo yarudi kwenye ubora na vijana wapate ofisi.
Mhe. Dkt. Gwajima D wizara yako inahusika kabisa kwa upande wa maendeleo ya vijana, naomba ufikishe hili kwenye vikao vya baraza la mawaziri. Ahsante