Serikali punguzeni utitiri huu wa Taasisi ni mzigo kwa walipa kodi

Serikali punguzeni utitiri huu wa Taasisi ni mzigo kwa walipa kodi

... halafu nchi inaagiza ngano, sukari, na mafuta ya kula billions of money! Kuna bodi ya sukari by the way. Kazi yao kutoa vibali vya kuagiza sukari.

Wizara za Kilimo na Afya nadhani ndio zinaongoza kwa kuwa na taasisi nyingi zisizo na tija.
Kilimo na mifugo utawataka kwa kuanzisha bodi, hapa tuna bodi ya mbegu, bodi ya mbolea, bodi ya nafaka, kule bodi ya maziwa, bodi ya nyama, bodi ya ngozi etc, etc, etc...
 
Nawasalimu kwa jina la JMT..na Kazi iendelee.

Ifike wakati serikali ichukue maamuzi magumu na yenye tija kwa Taifa kwa kupunguza utitiri wa Taasisi zake zilizo chini ya Wizara mbalimbali.

Ukiacha kwamba hazina tija kwa Nchi bali ni mzigo mkubwa sana wa walipakodi wa Tanzania kwani zinaongeza gharama za utawala zisizo na msingi na kuleta urasimu,gharama na usumbufu kwa wananchi.

Serikali chukueni hatua ya kuziunganisha na kufuta zile zisizo na tija.

Just imagine Wizara moja ya Viwanda na Uwekezaji ina Taasisi zaidi ya16 zilizo chini yake.Sasa piga hesabu kuna zaidi ya Wizara ngapi hapa Tanzania.

Hamuoni kuwa na lundo la Taasisi kunaongeza urasimu,usumbufu na gharama zisizo za msingi kwa wawekezaji na wananchi?

Kwa kuwa mh.Rais wewe ni Msikivu na Ili kuleta ufanisi ,basi shughulikia na hili maana imekuwa ni kichaka cha upigaji wakati ufanisi ni zero👇


Pengine tunakwama sababu hatufanyi study ya muundo wa serikali na taasisi zake. Pengine umepitwa na wakati. Kuna dublication ya majukumu na muingiliano mkubwa wa baadhi ya taasisi.
Mfano, TBS na Government Chemistry...etc
 
The National Development Corporation ilianzishwa na serikali kwa ajili ya kuchochea,kuendeleza na kukuza maendeleo ya kiuchumi ya Taifa kwa sectors zote.
Imeshafanya hivyo? Hiyo na Planning Commission tofauti yao ni ipi?
 
Mfano Geological Survey of Tanzania(GST) na tume ya madini zinatakiwa ziunganishwe iwe taasisi moja
 
Weeeee hhh waguse hukohuko, huku kwetu watuache tujenge nchi.
Hizi bodi ndio zifutwe
Bodi ya maziwa
Bodi ya nyama
Bodi ya korosho
Bodi ya pamba
Bodi ya kahawa
Bodi ya filamu
Bodi ya bahati nasibu
Bodi ya misitu n.k
Hivi watumishi wa hizi bodi huwa wanalipwa mishahara kila mwezi au malipo yao yapojwe?

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Ugatuzi ni serikali za majimbo au wananchi wawachague viongozi wao wengi.
Karibu wakuu wa hayo mashirika yote na hizo bodi wanateuliwa na mtu mmoja amabaye ndiye anateua pia msururu wa viongozi watakaozisimamia.Uwekwenye idara na taasisi serikalini madaraka yanagatuliwa

Ugatuzi ni serikali za majimbo au wananchi wawachague viongozi wao wengi.
Karibu wakuu wa hayo mashirika yote na hizo bodi wanateuliwa na mtu mmoja amabaye ndiye anateua pia msururu wa viongozi watakaozisimamia.
Ugatuzi ni muhimu sana... Sasa sijui kwanini serikali ya ccm inaamini katika kuwashikilia wananchi na kuwafanya watumwa wa kutoa kafara ili mambo yao yaende.
 
... halafu nchi inaagiza ngano, sukari, na mafuta ya kula billions of money! Kuna bodi ya sukari by the way. Kazi yao kutoa vibali vya kuagiza sukari.

Wizara za Kilimo na Afya nadhani ndio zinaongoza kwa kuwa na taasisi nyingi zisizo na tija.
Bodi zetu zinaongozwa na wasomi makada. Hawana uwezo wa kuyakataa maelekezo ya wanasiasa wenye maslahi binafasi.
Kwenye sukari ni aibu tupu... Kagera Sugar, Mtibwa Sugar, Bagamoyo Sugar, TPC, Zbar, alafu bado sukari haitoshi nchini bodi inatoa vibali kuagiza nje ya nchi!
Kwenye samani ni aibu tupu kama kwenye magari...from 1961 hadi leo 2022 miaka zaidi ya 60 bado tunaendelea kuwa soko la bidhaa za kichuuzi kutoka nje ya nchi!

Bila system-overhaul tutaishia pabaya!
 
Wizara inaundwa na kupitia hizi Taasisi.

UTI wa mgongo wa wizara ni hizi Taasisi, zisipokuwepo hakuna wizara.

Kazi kubwa ya wizara ni kuzisimamia hizi Taasisi.

Kwa iyo ni vyema tukawa na taasisi tukaua wizara
 
Hata nafasi ya msemaji wa serikali na Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu inatakiwa iwe nafasi moja.
Unaweza kujiuliza kuna Mamlaka ya Dawa na vifaa tiba TMDA then kuna Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali,TBS and such nonsense..

Eti saizi wanataka waanzishe bank ya ushirika wakti tayari kuna benki ya kilimo na Kuna CRDB ambayo ndio ulikuwa Bank ya Ushirika..Haya ni matumizi mabaya ya Kodi ya Wananchi.👇

Screenshot_20220520-083659.png
 
Back
Top Bottom