Serikali: Sanamu ya Nyerere imemlenga Nyerere wa miaka ya 60-80, imefanana naye kwa 92%. Serikali imeridhika yule ni Nyerere

Mnapenda sana Watanzania kujadili offpoints.

Mbona issue ya kufanana au kutokufanana ni issue ndogo sana!!. Nilitarajia vijana na wasomi wa Kitanzania wajikite kwenye mchango wa Nyerere kwa ukombozi wa nchi za southern Africa, kwanini iwekwe mwaka 2024 na siyo mwaka 1990 baada ya Uhuru wa Namibia iliyokuwa nchi ya mwisho kupata uhuru?.
Sanamu kama haifanani yaweza kubadilishwa wakati wowote. Lakini akili za watanzania zimejikita katika mambo peanut au mediocre. Yaani mnapenda udaku udaku tu
 
Nyerere alikuwa anayapenda madaraka, mpaka mwanae akamuita MADARAKA 🤣 , na alikaa madarakani kwa miongo 2 mfuatano
 
Ngoja tukamuulize Nyerere mwenyewe.
 
SIO NYERERE WALA HAWAFANANI HATA SISI MIAKA HIYO TULIKUWEPO
 
Mjadala unahusu mchango wa Baba wa Taifa au Sanamu inayosemekana ni ya Nyerere?...
Mbona macho yamekutoka?...kwani ulikuwa mmoja wa wana kamati?....
Wewe unaiona hiyo 92% hapo?
Punguza kudandia watu ....
 
Mjadala unahusu mchango wa Baba wa Taifa au Sanamu inayosemekana ni ya Nyerere?...
Mbona macho yamekutoka?...kwani ulikuwa mmoja wa wana kamati?....
Wewe unaiona hiyo 92% hapo?
Punguza kudandia watu ....
Yap !! Na wamekuambia ni appearance yake kipindi cha harakati za ukombozi wa nchi za southern Africa. Yaani 1960-1980s. Shida nyie mumekariri appearance ya Nyerere kwenye 1990s
 
Yap !! Na wamekuambia ni appearance yake kipindi cha harakati za ukombozi wa nchi za southern Africa. Yaani 1960-1980s. Shida nyie mumekariri appearance ya Nyerere kwenye 1990s
Hamna haja ya kubishana...
Kwa kifupi nikuambie tu hicho kipindi wanachosema nilikuwepo.
Ila hii Sanamu sio...
 
Wenzenu miaka ya 80 tulikuwa tunaishi vijiji jirani na Butiama. Alipokuwa shambani tunapita jirani na shamba lake kwenda shule tunamuona. Lakini hatukuwahi kuona Nyerere mwenye Sura hiyo. Huyu labda ni wa 2030.
 
Kwani Madaraka ndo nani? Tunamjua Nyerere wa enzi hizo, na hata picha za ujana wake, Nyerere hakubadirika sana! Aibu zenu! Na huyo anayeongea kichwani hamnazo!
 
Jamani ebo tusaidiane hapa, hii ndio sanamu yenye sura halisi ya muasisi wetu wa Taifa la Tanzania, Mwl. Julius K.Nyerere? [emoji849]View attachment 2912088
Halafu eti sirikali ya Tanzania imetumia jumla ya Tsh 487 milioni kwenye huu mchongo wa sanamu yenye sura feki !!!
 
 

Attachments

  • D_GcEG8XkAAil_d.jpg
    12.3 KB · Views: 3
  • nyerere-pic.jpg
    191.7 KB · Views: 3
  • maxresdefault.jpg
    65 KB · Views: 3
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…