Serikali: Sasa ni ruksa kusafirisha wanyama nje ya nchi

Annunaki

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2021
Posts
2,042
Reaction score
3,674
IMG-20220604-WA0046.jpg
Hali iko hivyo, tunaelekea kule 7kule tulipotoka, sasa ni rasmi twiga wetu wataanza kupandishwa ndege tena kwenda Ughaibuni.

_______________

Wafanyabishara sasa huru kusafirisha wanyama Pori kutoka Tanzania

Marufuku hiyo imeondolewa kwa muda wa miezi sita ambapo wafanyabiashara watakuwa huru kusafirisha nje wanyama pori kuanzia Juni 6 hadi Desemba 5

Tanzania imeondowa kwa muda marufuku ya usafirishaji wanyama pori iliyokuwa imewekwa miaka sita iliyopita kwa lengo la kuwalinda wanyama pamoja na ndege katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Uamuazi wa kuondolewa marufuku hiyo kwa kipindi cha miezi sita kumewaibua watetezi wa mazingira na wanyama pori kutowa mwito kuwepo michakato ya ufuatiliaji kuwalinda wanyama dhidi ya ujangili ambao umepunguwa kwa kiasi.

Mamlaka ya wanyama pori nchini Tanzania ijumaa ilitowa taarifa ikisema serikali imekuwa ikitathmini biashara ya usafirishaji wanyama pori hai tangu ilipowekwa marufuku hiyo na hivi sasa imeamua kuondowa marufuku hiyo.

Taarifa hiyo imebaini kwamba wafanyabiashara watakuwa na kipindi cha miezi sita kuanzia Juni 6 hadi Desemba 5 kumaliza kuuza wanyama waliokuwa wamebakisha walioshindwa kuwauza wakati marufuku hiyo ilipokuwa ikitekelezwa.

Tanzania iliweka marufuku ya kusafirisha wanyama pori mnamo mwaka 2016 chini ya utawala uliopita uliokuwa ukiongozwa na hayati rais John Pombe Magufuli ambaye namna yake ya uongozi ilimfanya apachikwe jina la ''Bulldozer''.

Wakati huo serikali ilihalalisha marufuku hiyo kwasababu ya dosari zilizokuweko kwenye biashara,ikiwemo usafirishaji nje wa wanyama wanaolindwa.

Rais wa sasa wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan ameamua kujitenga na baadhi ya sera zilizokuwa zikifuatwa na mtangulizi wake,tangu alipoingia madarakani mwaka jana kufuatia kifo cha ghafla cha Magufuli.

WWF: Uamuzi huo usifute mafanikio yaliofikiwa

Shirika la kutetea mazingira na wanyama pori la WWF limetahadharisha kwamba kuondolewa kwa marufuku hiyo hakupaswi kuyaondowa mafanikio yaliyopatikana katika kuwalinda wanyama pori,na kuchochea kurudi hatua kama ujangili ambao umeonekana kupungua.

Amani Ngasuru ambaye ni mkurugenzi wa WWF nchini Tanzania ameliambia shirika la habari la AFP kwamba mifumo ya uhakika ya ufuatiliaji inahitajika pamoja na data kuenda sambamba na maamuzi kama yaliyofanyika.

Tanzania inafahamika kwa fukwe zake za kuvutia katika visiwa vya Zanzibar,lakini pia matembezi ya safari ya kutazama wanyama pori pamoja na mlima mrefu barani Afrika,Kilimanjaro,yote hayo yakiwa vivutio vikubwa kwa watalii.

Mnamo mwaka 2010 kiasi wanyama 116 pamoja na ndege 16 baadhi wakiwa ni wanyama wanaotakiwa kulindwa walisafirishwa kutoka uwanja wa ndege wa Kilimanjaro,huko kaskazini mwa nchi hiyo kwa ndege ya shirika la ndege la Qatar.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani ya Tanzania, miongoni mwa wanyama hao walikuwemo twiga wanne, aina chungunzima ya paa,na ndege aina ya Tai.

Mwandishi:Saumu Mwasimba

Mhariri:Hawa Bihoga
 
Serikali kupitia wizara ya maliasili na utalii kuanzia sasa imeruhusu biashara ya kusafirisha wanyama pori hai nje ya nchi iliyokuwa imepigwa marufuku tangu mwaka 2016.
IMG-20220604-WA0046.jpg

=====
Wafanyabishara sasa huru kusafirisha wanyama Pori kutoka Tanzania

Na Saumu Mwasimba | Marufuku ya kusafirisha nje wanyama iliwekwa 2016 | saa (0) nyuma

Marufuku hiyo imeondolewa kwa muda wa miezi sita ambapo wafanyabiashara watakuwa huru kusafirisha nje wanyama pori kuanzia Juni 6 hadi Desemba 5

Tanzania imeondowa kwa muda marufuku ya usafirishaji wanyama pori iliyokuwa imewekwa miaka sita iliyopita kwa lengo la kuwalinda wanyama pamoja na ndege katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Uamuazi wa kuondolewa marufuku hiyo kwa kipindi cha miezi sita kumewaibua watetezi wa mazingira na wanyama pori kutowa mwito kuwepo michakato ya ufuatiliaji kuwalinda wanyama dhidi ya ujangili ambao umepunguwa kwa kiasi.

Mamlaka ya wanyama pori nchini Tanzania ijumaa ilitowa taarifa ikisema serikali imekuwa ikitathmini biashara ya usafirishaji wanyama pori hai tangu ilipowekwa marufuku hiyo na hivi sasa imeamua kuondowa marufuku hiyo.

Taarifa hiyo imebaini kwamba wafanyabiashara watakuwa na kipindi cha miezi sita kuanzia Juni 6 hadi Desemba 5 kumaliza kuuza wanyama waliokuwa wamebakisha walioshindwa kuwauza wakati marufuku hiyo ilipokuwa ikitekelezwa.

Tanzania iliweka marufuku ya kusafirisha wanyama pori mnamo mwaka 2016 chini ya utawala uliopita uliokuwa ukiongozwa na hayati rais John Pombe Magufuli ambaye namna yake ya uongozi ilimfanya apachikwe jina la ''Bulldozer''.

Wakati huo serikali ilihalalisha marufuku hiyo kwasababu ya dosari zilizokuweko kwenye biashara,ikiwemo usafirishaji nje wa wanyama wanaolindwa.

Rais wa sasa wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan ameamua kujitenga na baadhi ya sera zilizokuwa zikifuatwa na mtangulizi wake,tangu alipoingia madarakani mwaka jana kufuatia kifo cha ghafla cha Magufuli.

WWF: Uamuzi huo usifute mafanikio yaliofikiwa

Shirika la kutetea mazingira na wanyama pori la WWF limetahadharisha kwamba kuondolewa kwa marufuku hiyo hakupaswi kuyaondowa mafanikio yaliyopatikana katika kuwalinda wanyama pori,na kuchochea kurudi hatua kama ujangili ambao umeonekana kupungua.

Amani Ngasuru ambaye ni mkurugenzi wa WWF nchini Tanzania ameliambia shirika la habari la AFP kwamba mifumo ya uhakika ya ufuatiliaji inahitajika pamoja na data kuenda sambamba na maamuzi kama yaliyofanyika.

Tanzania inafahamika kwa fukwe zake za kuvutia katika visiwa vya Zanzibar,lakini pia matembezi ya safari ya kutazama wanyama pori pamoja na mlima mrefu barani Afrika,Kilimanjaro,yote hayo yakiwa vivutio vikubwa kwa watalii.

Mnamo mwaka 2010 kiasi wanyama 116 pamoja na ndege 16 baadhi wakiwa ni wanyama wanaotakiwa kulindwa walisafirishwa kutoka uwanja wa ndege wa Kilimanjaro,huko kaskazini mwa nchi hiyo kwa ndege ya shirika la ndege la Qatar.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani ya Tanzania, miongoni mwa wanyama hao walikuwemo twiga wanne, aina chungunzima ya paa,na ndege aina ya Tai.

Mwandishi:Saumu Mwasimba

Mhariri: Hawa Bihoga
 
Nchi inafunguliwa wacheni watu walambe asali hauna cha kufanya cha msingi, tu watafute eneo kubwa wajenge Zoo ya kuhufadhi wanayama pori mbalimbali ili miaka ijayo watoto wetu wasiishie kusimuliwa, wawe wanawaona kwenye mazoo.

Mwingi unaendelea kupigwa.
 
Siku hizi ni ngumu kutenganisha habari ya Utani (Jokes) na Reality..., sababu ni kama tunaishi in a Fictional Non Logical World....

Kama ni vema kufanya hivyo why miezi sita ? kwanini isiwe to infinity ? Au ni kuwapa dili walio na shehena zao waweze kuzi-dispose....

Na pro and cons ya hili jambo ni nini ?

Na Je angalau si lingepita kule kwenye a rubber stamp ya serikali (bunge) ili likajadiliwe ili likibackfire tupate wengi walio responsible
 
Kufika 2030 wanyama watakua wameisha nchi hii maana sasa watasafirishwa kwa hasira sana kufidia muda ule ambao hawakua wanasafirishwa.

Hii nchi sasa ni ruksa kwa kila kitu, nchi imefunguliwa kwa rushwa, wizi, mikataba mibovu, na kila kitu.

Huyu mama kwao Zanzibar hawana wanyama zaidi ya pweza na ngisi anataka amalize wanyama wetu kisha arudi kwao Zanzibar.

Watanganyika tumekwisha.
 
Hatuna Rais kwa kifupi
 
Back
Top Bottom