Serikali: Sasa ni ruksa kusafirisha wanyama nje ya nchi

Serikali: Sasa ni ruksa kusafirisha wanyama nje ya nchi

zama za Beijing kushika hatamu kila rangi ya wizi na ufisadi tutaiona! hii ni trela tu muvi kamili baada ya uchaguzi 2025. kweli Mungu ni wa kipekee kukausha mti wa mpingo na kuchipua mpodo! ashukuriwe sana
 
Serikali kupitia wizara ya maliasili na utalii kuanzia sasa imeruhusu biashara ya kusafirisha wanyama pori hai nje ya nchi iliyokuwa imepigwa marufuku tangu mwaka 2016.
View attachment 2250504

=====
Wafanyabishara sasa huru kusafirisha wanyama Pori kutoka Tanzania

Na Saumu Mwasimba | Marufuku ya kusafirisha nje wanyama iliwekwa 2016 | saa (0) nyuma

Marufuku hiyo imeondolewa kwa muda wa miezi sita ambapo wafanyabiashara watakuwa huru kusafirisha nje wanyama pori kuanzia Juni 6 hadi Desemba 5

Tanzania imeondowa kwa muda marufuku ya usafirishaji wanyama pori iliyokuwa imewekwa miaka sita iliyopita kwa lengo la kuwalinda wanyama pamoja na ndege katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Uamuazi wa kuondolewa marufuku hiyo kwa kipindi cha miezi sita kumewaibua watetezi wa mazingira na wanyama pori kutowa mwito kuwepo michakato ya ufuatiliaji kuwalinda wanyama dhidi ya ujangili ambao umepunguwa kwa kiasi.

Mamlaka ya wanyama pori nchini Tanzania ijumaa ilitowa taarifa ikisema serikali imekuwa ikitathmini biashara ya usafirishaji wanyama pori hai tangu ilipowekwa marufuku hiyo na hivi sasa imeamua kuondowa marufuku hiyo.

Taarifa hiyo imebaini kwamba wafanyabiashara watakuwa na kipindi cha miezi sita kuanzia Juni 6 hadi Desemba 5 kumaliza kuuza wanyama waliokuwa wamebakisha walioshindwa kuwauza wakati marufuku hiyo ilipokuwa ikitekelezwa.

Tanzania iliweka marufuku ya kusafirisha wanyama pori mnamo mwaka 2016 chini ya utawala uliopita uliokuwa ukiongozwa na hayati rais John Pombe Magufuli ambaye namna yake ya uongozi ilimfanya apachikwe jina la ''Bulldozer''.

Wakati huo serikali ilihalalisha marufuku hiyo kwasababu ya dosari zilizokuweko kwenye biashara,ikiwemo usafirishaji nje wa wanyama wanaolindwa.

Rais wa sasa wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan ameamua kujitenga na baadhi ya sera zilizokuwa zikifuatwa na mtangulizi wake,tangu alipoingia madarakani mwaka jana kufuatia kifo cha ghafla cha Magufuli.

WWF: Uamuzi huo usifute mafanikio yaliofikiwa

Shirika la kutetea mazingira na wanyama pori la WWF limetahadharisha kwamba kuondolewa kwa marufuku hiyo hakupaswi kuyaondowa mafanikio yaliyopatikana katika kuwalinda wanyama pori,na kuchochea kurudi hatua kama ujangili ambao umeonekana kupungua.

Amani Ngasuru ambaye ni mkurugenzi wa WWF nchini Tanzania ameliambia shirika la habari la AFP kwamba mifumo ya uhakika ya ufuatiliaji inahitajika pamoja na data kuenda sambamba na maamuzi kama yaliyofanyika.

Tanzania inafahamika kwa fukwe zake za kuvutia katika visiwa vya Zanzibar,lakini pia matembezi ya safari ya kutazama wanyama pori pamoja na mlima mrefu barani Afrika,Kilimanjaro,yote hayo yakiwa vivutio vikubwa kwa watalii.

Mnamo mwaka 2010 kiasi wanyama 116 pamoja na ndege 16 baadhi wakiwa ni wanyama wanaotakiwa kulindwa walisafirishwa kutoka uwanja wa ndege wa Kilimanjaro,huko kaskazini mwa nchi hiyo kwa ndege ya shirika la ndege la Qatar.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani ya Tanzania, miongoni mwa wanyama hao walikuwemo twiga wanne, aina chungunzima ya paa,na ndege aina ya Tai.

Mwandishi:Saumu Mwasimba

Mhariri: Hawa Bihoga

Pindi Chana: asitisha uuzaji wanyama Hai nje ya nchi. Kinana akasirishwa na kauli ya waziri​

 
Urithi kwa namna gani? Wanyama wanazaliana kila mwaka.

Mimi nimekuwa positive kwasababu unless kufanyike utafiti utakaotoa majibu negative, sioni ubaya wa kuuza na kutengeneza fedha za kuboresha huduma kwa jamii.
Uliwahi kusikia Australia wanauza Kangaroo? au huwa hawazaliani?
 
Acha ujinga. Wanyama huwa wanaongezeka Sana hivyo huhitaji kuvunwa. Wakivunwa wakauzwe huko duniani. Wewe wa Kantalamba huko huna hata faida kwenye mbuga kwenyewe huwa huendi
Umewaona wakiongezeka..? Vipi faru wanaopungua kwa kasi..?, Vipi twiga, vipi vipepeo, vipi.... Yani dah
 
Wengi wanapinga kwa kigezo cha utalii bila kufanya utafiti wowote. Watalii huku lazima waje kwao kunapokuwa majira ya baridi au joto kali (middle east)

Inaweza kufanyika cost benefit analysis kuona kama ina athari zozote.

Kama kuuza kunaleta fedha za maana hakuna tatizo kama wanyama wapo wengi.
Kama Serikali imetoa go ahead unataka utafiti upi mwingine ufanyike
 
Mbona tumeshakwambia wanaouzwa ni wale waliozidi? Halafu Bahamas hakuna wanyama na watu wanaenda.

Hospitality industry sio suala la maliasili, ni suala la ubunifu wa kiakili.
Leta takwimu za wanyama waliokuwepo 5 years ago vs waliopo mpaka may 2022 tujue walioongezeka ni wangapi basi, naona unabweka sana
 
Yaani sisi Waafrika ni manyang'au kweli...

Sasa ukishapeleka hao wanyama huko nje, hao wazungu watakuja kwetu kweli wakati huko kwao watakakuwa tayari wana hao wanyama!!!
Tena watawazalisha kwa wingi kwa matumizi ya baadae
 
Bado kuna watu wanafurahia biashara ya wanyama pori
Screenshot_20220606-000422.jpg
 
Leta takwimu za wanyama waliokuwepo 5 years ago vs waliopo mpaka may 2022 tujue walioongezeka ni wangapi basi, naona unabweka sana
Huu mjadala niliamua kuuacha kwasababu exposure yangu nadhani iko juu kidogo kuliko watanzania wa kawaida.

Utalii sio maliasili wala wanyama. Utalii ni hospitality industry na ndio maana nchi zinazoongoza kwa utalii duniani hazina hivyo mnavyoita maliasili.

Ukijaliwa fika Spain, Bahamas, Mauritius nk then utakuwa na mtazamo mpana kuhusu hii sector.

Hawa wanyama tulionao Tanzania nimewahi kuwaona kwenye zoo kule Switzerland, France, Thailand, US, Dubai, Qatar etc hivyo kama ni kuwaona wanyama tàyari wapo kule.

Hii mitazamo general na ya kijamaa ndio inafanya hii nchi wakenya wananufaika nayo. Watanzania wanalima halafu wanauza kwa bei ya kutupa kwa wakenya ambao wanafanya packaging na kuuza masoko ya dunia ya kwanza.

Hii mitazamo isipobadilika tukajua nini hasa ni tourism leo hii fukwe tu za bahari ya hindi zingeweza kuleta watalii milioni 20 kwa mwaka kama tungewekeza kwenye huduma zinazofanya mtalii aje.

Naishia hapa.
 
Kufika 2030 wanyama watakua wameisha nchi hii maana sasa watasafirishwa kwa hasira sana kufidia muda ule ambao hawakua wanasafirishwa.

Hii nchi sasa ni ruksa kwa kila kitu, nchi imefunguliwa kwa rushwa, wizi, mikataba mibovu, na kila kitu.

Huyu mama kwao Zanzibar hawana wanyama zaidi ya pweza na ngisi anataka amalize wanyama wetu kisha arudi kwao Zanzibar.

Watanganyika tumekwisha.
Uko sahihi mkuu,huko zanzibar wamepiga marufuku wanyama aina ya mbega kuwindwa ili kudhibiti kutoweka maana ni kitoweo huko wenye nchi wameona hawatakuwa na cha kujivunia.Mwenye shamba ndiye mwenye uchungu nalo.
 
Back
Top Bottom