Serikali: Sasa ni ruksa kusafirisha wanyama nje ya nchi

Serikali: Sasa ni ruksa kusafirisha wanyama nje ya nchi

View attachment 2250921Hali iko hivyo, tunaelekea kule 7kule tulipotoka, sasa ni rasmi twiga wetu wataanza kupandishwa ndege tena kwenda Ughaibuni.



_______________


Wafanyabishara sasa huru kusafirisha wanyama Pori kutoka Tanzania

Marufuku hiyo imeondolewa kwa muda wa miezi sita ambapo wafanyabiashara watakuwa huru kusafirisha nje wanyama pori kuanzia Juni 6 hadi Desemba 5

Tanzania imeondowa kwa muda marufuku ya usafirishaji wanyama pori iliyokuwa imewekwa miaka sita iliyopita kwa lengo la kuwalinda wanyama pamoja na ndege katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Uamuazi wa kuondolewa marufuku hiyo kwa kipindi cha miezi sita kumewaibua watetezi wa mazingira na wanyama pori kutowa mwito kuwepo michakato ya ufuatiliaji kuwalinda wanyama dhidi ya ujangili ambao umepunguwa kwa kiasi.

Mamlaka ya wanyama pori nchini Tanzania ijumaa ilitowa taarifa ikisema serikali imekuwa ikitathmini biashara ya usafirishaji wanyama pori hai tangu ilipowekwa marufuku hiyo na hivi sasa imeamua kuondowa marufuku hiyo.

Taarifa hiyo imebaini kwamba wafanyabiashara watakuwa na kipindi cha miezi sita kuanzia Juni 6 hadi Desemba 5 kumaliza kuuza wanyama waliokuwa wamebakisha walioshindwa kuwauza wakati marufuku hiyo ilipokuwa ikitekelezwa.

Tanzania iliweka marufuku ya kusafirisha wanyama pori mnamo mwaka 2016 chini ya utawala uliopita uliokuwa ukiongozwa na hayati rais John Pombe Magufuli ambaye namna yake ya uongozi ilimfanya apachikwe jina la ''Bulldozer''.

Wakati huo serikali ilihalalisha marufuku hiyo kwasababu ya dosari zilizokuweko kwenye biashara,ikiwemo usafirishaji nje wa wanyama wanaolindwa.

Rais wa sasa wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan ameamua kujitenga na baadhi ya sera zilizokuwa zikifuatwa na mtangulizi wake,tangu alipoingia madarakani mwaka jana kufuatia kifo cha ghafla cha Magufuli.

WWF: Uamuzi huo usifute mafanikio yaliofikiwa

Shirika la kutetea mazingira na wanyama pori la WWF limetahadharisha kwamba kuondolewa kwa marufuku hiyo hakupaswi kuyaondowa mafanikio yaliyopatikana katika kuwalinda wanyama pori,na kuchochea kurudi hatua kama ujangili ambao umeonekana kupungua.

Amani Ngasuru ambaye ni mkurugenzi wa WWF nchini Tanzania ameliambia shirika la habari la AFP kwamba mifumo ya uhakika ya ufuatiliaji inahitajika pamoja na data kuenda sambamba na maamuzi kama yaliyofanyika.

Tanzania inafahamika kwa fukwe zake za kuvutia katika visiwa vya Zanzibar,lakini pia matembezi ya safari ya kutazama wanyama pori pamoja na mlima mrefu barani Afrika,Kilimanjaro,yote hayo yakiwa vivutio vikubwa kwa watalii.

Mnamo mwaka 2010 kiasi wanyama 116 pamoja na ndege 16 baadhi wakiwa ni wanyama wanaotakiwa kulindwa walisafirishwa kutoka uwanja wa ndege wa Kilimanjaro,huko kaskazini mwa nchi hiyo kwa ndege ya shirika la ndege la Qatar.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani ya Tanzania, miongoni mwa wanyama hao walikuwemo twiga wanne, aina chungunzima ya paa,na ndege aina ya Tai.

Mwandishi:Saumu Mwasimba

Mhariri:Hawa Bihoga
Hili sikubaliani nalo kabisa, najua madhara yake. Kama ni hivyo basi hata hizo pembe zilizopo hapo stoo, mpingo house ziuzwe, kama tunafanya biashara ya wanyama hai kwanini tusamehe mabilioni (186 bil.) kwa wanyama ambao walishakufa aidha kutokana na uzee, kuliwa na predators au kuuliwa na poachers? TAWICO zama zile walikuwa wakitengeneza bilioni 20 tu, Wildlife dept. ikitengeneza chini ya hizo bil.20 kwa uwindaji, TAWA leo sijui wanatengeneza kiasi gani lakini ni kidogo sana kuliko hao wawili. Sasa tumepata pembe za 186 bil. tunaziacha ili tupewe sifa......za nini? Tufanye one and off sale....na hizo pesa zisaidie conservation siyo kujenga vyoo (tafuteni vyanzo vingine, uhifadhi bado kuna mengi ya kufanya na pesa hazitoshi)
Serikali acheni double standard, muwe wakweli. KURUHUSU KUUZA LIVE ANIMALS AU TROPHIES.....HAPANA, hatuna wanyama wa kutosha uzeni zile pembe zilizopo stock room pale mpingo house.
 
Maneno mazito sana. Hawa Wahindi wanaojiita WaTZ naona kama wanatuhujumu hivi? Na ndiyo hao wafadhili wa vyama, wapo kila sekta nyeti. Hivi kwa nini wanaaminiwa kijinga hivi?
1082611-Thomas-Sankara-Quote-He-who-feeds-you-controls-you.jpg
 
Sheria ilitugwa 2009 wewe unaona imetugwa Leo?.Na unaelewa nini ukisikia ruhusa ilitolewa ni ya miezi 6 tu?.Ulitaka hao wafanya biashara ambao tayari zuio la Magufuli lilikuja wakati tayari kwenye vitalu vyao kuna wanyama, wawapeleke wapi na ili hali serikali haikuwa tayari kuwachukua wanyama na kuwarudishia wafanya biashara gharama zao?.
Asante kwa kunielimisisha, kumbe wanataka kumlaumu Mama Samia bure tuu...
 
Asante kwa kunielimisisha, kumbe wanataka kumlaumu Mama Samia bure tuu...
Acha uzuzu wewe ...wanyama wetu ni mali yetu warudishwe porini jpm kaacha nchi hakuna hivyo vitaru vya kufuga wanyama ,ni mjinga tu anaweza kudanganywa . Wanyama poli wanachukua miaka mingi sana kuwa, fuga hadi kufikia kuzaa ....ukweli ni kwamba wanyama wote wananatoka mbugani hakuna kitaru cha kufuga tembo wala simba kwa ajili ya biashara .
 
Ngoja mama watafutie hela
Mkiongezwa posho mnashangilia
Wakiajiri mnashangilia
Mkiongezwa mishahara mnashangilia
Wanafunzi wote wakipatiwA mikopo ya elimu ya juu mnashangilia

Sasa pesa zinatoka wapi?

Je ni bora kuwa na wanayama maporini huku mnakufa njaa?
Kwamba Mnyamapori azeeke hadi ajifie ndo tufurahi?

Wauzwe tupate pesa!
Hii ni biashara na watu watapata pesa.

Maisha ni biashara, biashara yenye akili.
Siyo kupinga tuu under Emotional attacks.

Mama piga kazi
Sasa inakuwaje tena mnawaondoa wamasai ngorongoro. Si uzeni hao wanyama wamasai wabaki?
 
Back
Top Bottom