Kwa heshima na taadhima niiombe serikali kupitia TANROADS NA TARURA kuangalia namna ya kujenga barabara kutoka mafinga,kinyanambo c mpaka mlimba hata kwa kurekebisha au kujenga hata kwa changarawe hasa sehemu zile korofi ili kuwasaidia wananchi kuepuka na adha ya usafiri hasa kipindi cha masika.
Nmeandika ujumbe huu kwa serikali kwasababu barabara hii ilikuwa kwenye mpango wa kujengwa tangu mwaka 2012 mapaka watu wa barabara kwa maana ya TANROADS wakaweka alama za "X" kwenye nyumba za watu amabzo ziko karibu na barabara hivyo wananchi pamoja na makampuni yalianza uwekezaji kwenye upandaji wa miti ya mbao na mashamba mbalimbali ya mazao tofauti na hivi sasa ni wakati wa kuvuna kwahyo magari makubwa yanayobeba mizigo yanafanya barabara inayotumika kwa sasa ionekane haifai kutoka na kuzidiwa katika suala zima la matumizi.
Pia barabara hii ikijengwa wawekezaji watajenga viwanda vya kuchakata pamoja na kuzalisha mazao mbalimbali ya mazao ya miti.
Tofauti na hilo pia ujenzi wa barabara hii pindi itakapojengwa wananchi watapata ahuweni na nauli kutoka mjini mafinga kwenda vvijiji tofauti vinavyopitiwa na barabar hyo. Mfano kutoka mafinga mpaka mapanda kuna kilomita zisizozidi 100 lakini nauli ni sh.10,000/=ambapo kiwango cha nauli hyo kinachangiwa na ubovu wa barabara yenyewe.
Lakini pia ujenzi wa barabar hii utachangia pakubwa sana kwenye kupandisha thamani ya mazao yanayolimwa hasa mazao ya miti.
Kingine pia,jimbo la mufindi kaskazini linaonekana kama limetengwa kwenye suala zima la maendeleo licha ya kuchangia pato la taifa kwa kiasi kikubwa sana jambo ambalo sisi watumiaji wa barabara hii korofi tunaona kama kuna hujuma za watu wachache wanaochelewesha kujengwa hii barabara.
Yakwangu ni hayo tu..