Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Kufuatia taarifa ya Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu la kutaka nchi 36 kutaka kufanyia kazi baadhi ya mambo kadhaa ya kiuhamiaji ambayo yanaweza kuzuia raia wa Kitanzania kuzuiwa kuingia Marekani Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa amesema " Naomba kuujulisha umma kuwa tayari Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje imeanza kufanya mashauriano wa wenzetu upande wa Marekani kujua maeneo ambayo yanatakiwa kufanyiwa maboresho hususani yanayohusiana na masuala ya kikonselii ili kuharakisha Tanzania isiwe moja ya nchi zitakazozuiwa kuingia Marekani."
Kauli hii ya Msigwa inakuja baada ya Donald Trump kutaka nchi 36 zimetakiwa kufuatilia na kutoa taarifa kabla ya Julai 18, 2025 kuhusu utayari wa nchi zao kuboresha hati za usafiri kwa raia wao, pamoja na kuchukua hatua kuhusu raia wao walioko Marekani kinyume cha sheria.
Orodha ya nchi hizo 36 ni; Tanzania, Angola, Antigua and Barbuda, Benin, Bhutan, Burkina Faso, Cambodia, Cameroon, Cape Verde, DRC Congo, Djibouti, Dominica, Ethiopia, Misri, Gabon, Gambia, Ghana, Ivory Coast, Kyrgyzstan, Liberia, Malawi, Mauritania, Niger, Nigeria, St. Kitts na Nevis, St. Lucia, Sao Tome na Principe, Senegal, South Sudan, Syria, Tonga, Tuvalu, Uganda, Vanuatu, Zambia pamoja na Zimbabwe