Serikali tusaidieni kuondoa Magogo mabuchani

Serikali tusaidieni kuondoa Magogo mabuchani

Watetezi wa matumizi ya magogo wao ututaka kujiuliza kwa nini visu vya mashine ya kukatia nyama uisha na kutakiwa kubadilisha na kuweka kisu kipya. Wakimaanisha nyama iliyokatwa kwa kisu cha mashine ubaki na chembechembe za chuma kilichotumika kutengenzea kisu ambazo tunazila kupitia nyama hizo na mwisho wa siku tunapata madhara ya kiafya.
Mkuu ni kweli...ila hata kwenye mashine za kusaga nafaka.....kuna vyuma mule huwa vinabadilishwa na kuwekwa vipya kila baada ya muda fulani...navyo hutumika kuponda nafaka na kuwa unga......hakuna tulipo salama mkuu.....Mungu ndie mlinzi mkuu....
 
Hayo magogo yenyewe wanayasafisha vipi, pia wasisahau kuweka tiles za sakafuni na ukutani na AC kwenye kila bucha....tushachoka mambo ya ujima.
 
Nunua nyama kwenye butcher yenye mashine tu. Wakikosa wateja nao watatafuta mashine.
 
Sure asee hii tabia ya kucharanga nyama kwa shoka kwenye magogo ni ya enzi za ujima. Ukinunua nyama inakiwa na vimifupa vidogo vidogo ukipika chakula unaweza kuvunjika jino wakati wa kula.

Watumie mashine za kukatia nyama zinakata mpaka mfupa vizuri tu. Hii ya kucharanga inakera sana. Inaharibu nyama.
Naunga mkono hoja.. Huu usasa unatuletea madhara na maradhi mengi bila kujua
Mashoka na magogo anatumika bila kubalishwa? hayaishi?
Kwangu Mimi kero kubwa ni mizani za enzi za ukoloni. Twende na digitali sasa
 
Mashoka na magogo anatumika bila kubalishwa? hayaishi?
Kwangu Mimi kero kubwa ni mizani za enzi za ukoloni. Twende na digitali sasa
Kwa mizani ni sahihi kabisa nakubaliana nawe
 
Habari za mda huu

Naenda moja kwa moja kwenye mada. Serikali tumekuwa tukikatiwa nyama kwenye magogo toka enzi za uhuru. Bucha nyingi hasa mikoani ni magogo.

Binafsi sijaona madhara au kusikia madhara ila ukweli ni kwamba kutokana na mabadiliko ya teknolojia yanayoenda kasi dunian kote na pia hulka ya binadamu, kila mtu anapenda kitu kizuri.

Tunaomba mtutolee haya magogo buchani kama mliweza mifuko ya Rambo hili sidhani kama kwenu ni shida. Tunaomba msamini pia kipato chetu tunapata kwa shida sana bado kodi kama zote basi tunaomba na sisi tupate anagalau kitu bora, isue ya mizani buchani hiyo imewashinda kucheki kama inapima sawa au sio sawa, ila hilo la magogo lipo ndani ya uwezo wenu.

Kuna kipindi nilisikia mnataka kutoa magogo badae ikawa kimya. Ila hongeren sana kuweza kusimamia ili la usafi jumamosi za mwisho wa mwezi hapa mkoani kwangu panarizisha sana.

Asanteni
Hakuna kitu kibaya kukatia nyama kwenye plastic bora magogo ni organic.
 
Naunga mkono hoja.. Huu usasa unatuletea madhara na maradhi mengi bila kujua
Watu wanaona ufahari tu nyama ikatwe na mashine wajione washua😅!!! Bucha ilikata nyama kwa gogo na shoka toka uko kinda na ulikula bila kelele leo una kikazi chako na unafuu wa maisha unadharau bucha linalokata nyama kwa shoka na gogo
 
Kwa taarifa yako gogo linaoshwa na bucha lote pia.. Usipofanya hivyo nyama ya the next day haitauzika au haitalika kwa harufu..damu iliyooza ina harufu kali na mbaya
Damu iliyokauka kwenye gogo au chembechembe za gogo havina athari kama chembechembw za chuma toka kwenye msumeno wa umeme
Safi sana bro. Nilikua najaribu kuwaelimisha watu kwamba gogo ni organic kwa maana linaweza kuoza ila plastic au chuma wanavopigia kampeni ndo vibaya zaidi kiafya. Alietoa mada nafikiri ni mjinga ambae hana elimu ya organic na inorganic matter. Ye anachofikiria ni kuona nyama inakatiwa kwenye plastic nzuri zilizopakwa rangi
 
Me siamini kabisa, chuma ipo ila kiasi kidogo sana hata kisu cha jikoni kinaisha. Visu vyenyewe vya buchani vinaisha. Sufuria zenyewe zinaisha na kutoboka.
Chuma haina kwere sababu ikipungua mwilini pia lazma ulazwe! Mwili wako una chuma kwenye damu
 
Watu wanaona ufahari tu nyama ikatwe na mashine wajione washua[emoji28]!!! Bucha ilikata nyama kwa gogo na shoka toka uko kinda na ulikula bila kelele leo una kikazi chako na unafuu wa maisha unadharau bucha linalokata nyama kwa shoka na gogo
Very well said...! Usasa unatusahaulisha thamani ya ukale iliyotulea kufikia huo usasa
 
Yale magogo hatari kiafya damu ya miaka nenda rudi huozeana kwenye gogo hivyo huwemo wadudu usioona kwa macho.

Dawa wananchi tuanze kususa kununua nyama yenye gogo na tuwaambie kabisa wenye hizo bucha
Serikali izifunge tu hizo bucha zenye magogo
Heheheheh cha ajabu wanaokula nyama za mabucha ya vioo ndio wanaoongoza kwa cancer! Organic lifestyle imetubeba sana vizazi kwa vizazi mpaka leo tuko strong ila chunguza kwa makini kizazi cha 2000’s kilivyo dhaifu!

Tunailemaza miili kwa kisingizio cha teknolojia mpaka kufikia mwili hata ku fight na mafua hauwezi!
 
Safi sana bro. Nilikua najaribu kuwaelimisha watu kwamba gogo ni organic kwa maana linaweza kuoza ila plastic au chuma wanavopigia kampeni ndo vibaya zaidi kiafya. Alietoa mada nafikiri ni mjinga ambae hana elimu ya organic na inorganic matter. Ye anachofikiria ni kuona nyama inakatiwa kwenye plastic nzuri zilizopakwa rangi
Sasa hivi ulaya baada ya kupata athari kubwa zitokanazo na usasa wanarudi kwenye organic.. Sisi ndio kwanza tunautaka usasa[emoji848][emoji848][emoji848][emoji2827][emoji2827][emoji2827]
 
Very well said...! Usasa unatusahaulisha thamani ya ukale iliyotulea kufikia huo usasa
Huu usasa ndio unalemaza miili yetu kuanzia lifestyle, vyakula na utegemezi wa madawa! Wenzetu wa ulaya washagundua processed foods sio salama na sedentary lifestyles!

Sie tunaona ufahari ukanunue mavitu mengi supermarket na utembelee gari kila siku hutaki kuuchosha mwili kwa kuchapa mguu!

Magonjwa ya kisukari na BP yatazidi kuwa major hit yakiongozwa na cancer!
 
Yale magogo hatari kiafya damu ya miaka nenda rudi huozeana kwenye gogo hivyo huwemo wadudu usioona kwa macho.

Dawa wananchi tuanze kususa kununua nyama yenye gogo na tuwaambie kabisa wenye hizo bucha
Serikali izifunge tu hizo bucha zenye magogo
Utasusa peke yako.... dawa ni kuangalia namna gani ya kubadili sio kususa.
Je umeme ukikatika siku nzima nyama watakatia nn?? Wakati mashine zinatumia umeme?
2. Kipi bora kati ya kula kipande cha gogo au kipande cha chuma?
 
Back
Top Bottom