Serikali tusaidieni kuondoa Magogo mabuchani

Serikali tusaidieni kuondoa Magogo mabuchani

Kila kitu ukitaka kukikosoa kinakosolewa tu.
Vipi kuhusu mashine za kusaga mahindi, vile vyuma huisha mara kwa mara, n.k.
Ya ngoso mwachie - - -
Hiyo ya magogo sioni madhara, cha kuzingatia ni usafi.
Yaaaa wazingatie usafi lakini sio kukata nyama juu ya gogo direct waweke hata nailoni juu ya gogo wakikata damu iishie kwenye nailoni liwezalo safishika kirahisi
 
Hii asome Mshana Jr tu, kwenye sherehe za Machifu jana kulikuwa na akinamama watatu hivi, mmoja akipeta nafaka kwenye ungo na wawili wakisaga nafaka kwenye mawe, mawe yale wanayosagia huisha, unga unaosagwa huwa na unga wa jiwe la kusagia hivyo taratibu familia inayotumia jiwe hilo hulimaliza kwa kulila bila kujua na maisha yanaendelea bila kudhurika! Ina maana unazaliwa mpaka unazeeka utakuwa umekula huenda robo ya jiwe lako la kusagia.
Na ndio yametukuza hayo mpaka tuna familia na wajukuu
 
Ila gogo lililochakaa huleta kero kwenye nyama kwani muoshaji hubidi avinyofoe vipande vya gogo mpaka viishe siyo kama jiwe.
Kila kitu kinahitaji utunzaji na usafi sio gogo tu hata mazingira ya bucha pia
 
Mkuu unajua kuwa mpaka leo bado kuna vijiji havina umeme na huko kuna butchery? Unafahamu kuwa mashine zinatumia umeme?
 
Umenikumbisha mbali sana kuna mahali nilichukua nyama kumbe lile gogo ni nyungu kweli kweli.
 
Mkuu hivi mnaposema mikoani huwa mnamanisha wapi?

Lakini mada yako nimeipenda, huwa najiuliza pia, kwanini magogo?
 
Mi nashauri tu magogo yawepo kwa dharura na mashine za umeme za kukatia pia ziwepo,mteja achague mwenyewe
 
Mkuu Dodoma kuna butcher Safi bhana! Japo chafu hazikosekani nawapongeza kwa kweli.
Dodoma Manispaa mwaka 2016 nilikuwa huko, tulisimamia kikamilifu kila mwenye butcher kuhakikisha ana mashine.
 
Habari za mda huu

Naenda moja kwa moja kwenye mada. Serikali tumekuwa tukikatiwa nyama kwenye magogo toka enzi za uhuru. Bucha nyingi hasa mikoani ni magogo.

Binafsi sijaona madhara au kusikia madhara ila ukweli ni kwamba kutokana na mabadiliko ya teknolojia yanayoenda kasi dunian kote na pia hulka ya binadamu, kila mtu anapenda kitu kizuri.

Tunaomba mtutolee haya magogo buchani kama mliweza mifuko ya Rambo hili sidhani kama kwenu ni shida. Tunaomba msamini pia kipato chetu tunapata kwa shida sana bado kodi kama zote basi tunaomba na sisi tupate anagalau kitu bora, isue ya mizani buchani hiyo imewashinda kucheki kama inapima sawa au sio sawa, ila hilo la magogo lipo ndani ya uwezo wenu.

Kuna kipindi nilisikia mnataka kutoa magogo badae ikawa kimya. Ila hongeren sana kuweza kusimamia ili la usafi jumamosi za mwisho wa mwezi hapa mkoani kwangu panarizisha sana.

Asanteni
Mm siungi mkono hoja kwa sababu. Ukitoa gogo unawekewa plastiki ya kukatia nyama ile plastini nayo inakwisha kama gogo na vie vupande vinakuwepo ktk nyama, sasa hatari iliokuwapo kwenye plastik ni kwamba haiyozi kwa hiyo ukila plastik inakaa tumboni milele je kati ya gogo na plastini nipi kiwepo buchani?
 
Si kweli mtaani kwetu mabucha mengi vigogo tumesahau kabisa. Vile vigogo kwa kuwa hawavisafishi vizuri kwa maji ya moto kabisa vina uchafu mwingi sanaa...
Siyo kweli nini! Hakuna maeneo umeme hukatika kila siku? Kuna wakati maeneo ya Kariakoo kila siku ni majenereta yanaunguruma, Kigoma ilikuwa haina umeme kwa siku kadhaa, usipende kukataa kitu usichokijua.
 
Mm siungi mkono hoja kwa sababu. Ukitoa gogo unawekewa plastiki ya kukatia nyama ile plastini nayo inakwisha kama gogo na vie vupande vinakuwepo ktk nyama, sasa hatari iliokuwapo kwenye plastik ni kwamba haiyozi kwa hiyo ukila plastik inakaa tumboni milele je kati ya gogo na plastini nipi kiwepo buchani?
Mkuu sijakuelewa plastic gan unaongelea?
 
Back
Top Bottom