Serikali tusaidieni kuondoa Magogo mabuchani

Kila kitu ukitaka kukikosoa kinakosolewa tu.
Vipi kuhusu mashine za kusaga mahindi, vile vyuma huisha mara kwa mara, n.k.
Ya ngoso mwachie - - -
Hiyo ya magogo sioni madhara, cha kuzingatia ni usafi.
Yaaaa wazingatie usafi lakini sio kukata nyama juu ya gogo direct waweke hata nailoni juu ya gogo wakikata damu iishie kwenye nailoni liwezalo safishika kirahisi
 
Na ndio yametukuza hayo mpaka tuna familia na wajukuu
 
Ila gogo lililochakaa huleta kero kwenye nyama kwani muoshaji hubidi avinyofoe vipande vya gogo mpaka viishe siyo kama jiwe.
Kila kitu kinahitaji utunzaji na usafi sio gogo tu hata mazingira ya bucha pia
 
Na ndio yametukuza hayo mpaka tuna familia na wajukuu
Ndio maana akili ziko kidogo shauri ya kula nyama za kukatwa kwenye magogo kukua sio shida afya ya akili ndio maneno
 
Mkuu unajua kuwa mpaka leo bado kuna vijiji havina umeme na huko kuna butchery? Unafahamu kuwa mashine zinatumia umeme?
 
Tusaidieni? Wewe na nani? Magogo yaendelee kutumika.
 
Umenikumbisha mbali sana kuna mahali nilichukua nyama kumbe lile gogo ni nyungu kweli kweli.
 
Mkuu hivi mnaposema mikoani huwa mnamanisha wapi?

Lakini mada yako nimeipenda, huwa najiuliza pia, kwanini magogo?
 
Mi nashauri tu magogo yawepo kwa dharura na mashine za umeme za kukatia pia ziwepo,mteja achague mwenyewe
 
Mkuu Dodoma kuna butcher Safi bhana! Japo chafu hazikosekani nawapongeza kwa kweli.
Dodoma Manispaa mwaka 2016 nilikuwa huko, tulisimamia kikamilifu kila mwenye butcher kuhakikisha ana mashine.
 
Mm siungi mkono hoja kwa sababu. Ukitoa gogo unawekewa plastiki ya kukatia nyama ile plastini nayo inakwisha kama gogo na vie vupande vinakuwepo ktk nyama, sasa hatari iliokuwapo kwenye plastik ni kwamba haiyozi kwa hiyo ukila plastik inakaa tumboni milele je kati ya gogo na plastini nipi kiwepo buchani?
 
Si kweli mtaani kwetu mabucha mengi vigogo tumesahau kabisa. Vile vigogo kwa kuwa hawavisafishi vizuri kwa maji ya moto kabisa vina uchafu mwingi sanaa...
Siyo kweli nini! Hakuna maeneo umeme hukatika kila siku? Kuna wakati maeneo ya Kariakoo kila siku ni majenereta yanaunguruma, Kigoma ilikuwa haina umeme kwa siku kadhaa, usipende kukataa kitu usichokijua.
 
Mkuu sijakuelewa plastic gan unaongelea?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…