Serikali: Tutaongeza nguvu kazi, miundombinu na bajeti kwa taasisi na vyuo vinavyofundisha Kiswahili

Serikali: Tutaongeza nguvu kazi, miundombinu na bajeti kwa taasisi na vyuo vinavyofundisha Kiswahili

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Serikali imesema itaongeza nguvu kazi, miundombinu na bajeti kwa taasisi na vyuo vinavyofundisha Kiswahili ili viendelee kuandaa wataalamu zaidi watakaotumika duniani kote.

Akizungumza kwa njia ya simu katika Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani yanayofanyika Jijini Dar es Salaam, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema Serikali itaendelea kutoa nyenzo na mafunzo ya kisasa kwa wakalimani, waandishi wa vitabu na wafundishaji wa Kiswahili kwa wageni.

Katika Maadhimisho hayo, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Elimu ya Msingi ya Jamhuri ya Afrika Kusini zimetia saini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika mambo mbalimbali ya Elimu ya Msingi ikiwemo kufundisha lugha ya Kiswahili.

Utiwaji wa saini umefanywa mbele ya Mhe. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda kwa upande wa Tanzania na kwa Jamhuri ya Afrika Kusini umefanywa na Waziri wa Elimu ya Msingi, Matsie Angelina Motshekga.

Akiongea kabla ya utiaji wa saini Prof. Mkenda amesema baadaya ya kukamilika kwa maandalizi ya Hati hiyo Rais Samia Suluhu Hassan aliagiza kutiwa saini rasmi makubaliano hayo Siku ya Kiswahili Duniani.

"Kazi ya kuandaa makubaliano haya ilifanyika kwa muda ikiongozwa na viongozi mbalimbali ambapo baada ya kukamilika Rais alituagiza tusaini makubaliano haya leo katika siku hii muhimu kwa nchi yetu," amesema Pro. Mkenda.

Naye Waziri Matsie Angelina Motshekga amesema lengo la kusaini hati hiyo ni kufundisha Kiswahili katika shule za msingi na vyuo pamoja na kukisambaza nchi nzima ili kuwawezesha Waafrika Kusini kuitumia lugha ya Kiswahili.

Motshekga ameongeza kuwa kwa Afrika Kusini Kiswahili ni zaidi ya lugha muhimu sana kwani itasaidia kuunganisha watu wake na Bara la Afrika ambapo Kiswahili kinaongelewa.

"Kiswahili kwa Afrika Kusini kitaunganisha watu wa Tanzania na kwetu pamoja na kuimarisha mahusiano ya muda mrefu yaliyopo kati ya nchi hizi mbili, na ni lazima tuhakikishe lugha hii inaunganisha watu wetu hususani vijana," amefafanua Waziri huyo wa Afrika Kusini .
IMG-20220707-WA0038.jpg
IMG-20220707-WA0037.jpg
IMG-20220707-WA0036.jpg
 
Back
Top Bottom