Serikali: Visa vya COVID-19 vyafikia 53. Vyuo na Shule kuendelea kufungwa hadi Serikali itakapotoa tamko jingine

Wazo ni zuri ila technologia hapa kwetu bado ni ndogo internet ni gharama na walimu ni washamba na wanafunzi ni washamba watanzania ni washamba internet speed ndogo TUTAWEZA WAPI
 
Inaitwa UFARA naomba niishie apo
 
Hii comment inabidi iwafikie watu wote

Mpaka sasa sioni Logic ya kutangaza idadi ya wagonjwa wa Corona,haipo kabisa
Kama mtu kagundulika ana ugonjwa apelekwe karantini,apewe huduma zinazotakiwa na in case amefariki basi ndugu zake wapewe taarifa kama ilivyo kwa vifo vingine vinavyotokea kila dakika

Serikali ijikite kuhasisha watu kujiepusha na njia zote zinazoweza kusababisha maambukizi
Kama idadi ya watu wanaoukufa kila siku kwa sababu yoyote ile ingekua inatangazwa kama huu ugonjwa?...kungekua na faida gani sasa
 
Iko shida moja mkuu, hofu inaubaya na uzuri wake pia hasa Kwa jamii yetu hii, mtu anachapwa bastola pale Kwa jirani, na jirani yake anakimbilia kwenda kuangalia aone kinachotokea,

Tuspotangaziwa, ule umakini na namna ya kuchukua tahadhari itapungua na huenda ikawa ni sababu ya jamii kubwa kuambukizwa

Wakitangaza, Napo kuna Ile kunyanyapaana hata kama mtu unahoma Ile ya siku zote
 
Basi nafikiri solution ni la mtu binafsi kufata maagizo yote yaliyotolewa na serikali pamoja na ku avoid pia Social Network .
Personally huwa sipendi kusikia habari za vifo kila siku japo najua wanakufa....Hazisaidii
 
Hapo maana yake Vyuo na Mashule vimefungwa kwa muda usiojulikana.

Alafu hiyo sherehe ya Mapinduzi ya April 26 ni ipi hiyo?
Ofisi ya Waziri Mkuu imejaa vilaza watupu, wanashindwa kutofautisha kati ya sherehe ya muungano na sherehe ya mapinduzi!

Shame on them!
 
Hili nalo litapita tuzidi kuwa na subira na kuchukua tahadhari, kama tunaipanda jamii yetu basis hatuna budi kuchukua tahadhari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…