Serikali: Visa vya COVID-19 vyafikia 53. Vyuo na Shule kuendelea kufungwa hadi Serikali itakapotoa tamko jingine

Serikali: Visa vya COVID-19 vyafikia 53. Vyuo na Shule kuendelea kufungwa hadi Serikali itakapotoa tamko jingine

Nina jamaa yangu ameniambia jana mjomba ake alidondoka ghafla pale Mnazi Mmoja akafa on the spot na mwili umezuiwa na serikali kwa vipimo zaidi.

Guys....this shit is really tuwe makini na hii kitu.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
opondo,
Hata kama mtu ana uhitaji wa mwalimu hawezi kukupa ww, una matatizo ya herufi H, angalia hapo ulipoandika Hila, pia hapo ulipoandika Hiki badala ya Ili. Nyie ndio wale mkipewa mwanafunzi wa kike unaishia kumpa account ya facebook.
 
Sema mkuu, utatumia vifaa gani kuwafikia wanafunzi wako Kwa kuwa hatupasi kuchangamana
WaPo ambao nafika kwao majirani wanaonizunguka hapa, walioko mbali na walio serious natunga mtihani nawatumia whatsap then wakishamaliza wananirudishia kwa whatsap nawasahisha then nawatumia whatsap pamoja na marking scheme hili waone walipokosea ni wapi.
 
Mmh!

Watanzania watu wa ajabu sana,si mlikuwa mnapiga kelele kwamba serikali inaficha wagonjwa au?
yaani we acha tu.......ndo maana baadhi ya wenye mamlaka wanaamua kujipigia tu wakipata nafasi; maana vyovyote iwavyo watasemwa tu! mwisho wa siku, kutoeleweka kwetu tunaishia kuumia wenyewe tu!
 
Tarehe 26 April ni sherehe za mapinduzi tokea lini?
Mpaka barua inatumwa hakuna aliyeona makosa hayo?
 
Isee!!!

Biashara sasa zimedorola na zingine kuelekea kukata kabisa Kwa sababu mtu hufanyi biashara Ila mwisho wa mwezi unatakiwa kurejesha madeni Bank, Mabenk ya kwetu yanaendelea kukomalia marejesho ya mikopo, Wakati nchi zilizokopa huko WB,IMF na sehemu zinginezo wanalia kusimamishwa Kwa marejesho Yao au kufutwa kabisa!

Hili la kusimamishwa marejesho ya mikopo Kwa wafanyabiashara hapa kwetu mbona haliongelewi?

Unayo hoja ya msingi. Hapa tulipo ni kisebu sebu na kiroho papo. Tupo hatupo. Si moto wala baridi. Ilibidi kuchagua moja:

Kuna Corona tuache yote mengine tupambane naye, au hamna Corona turudi 100% kwenye shughuli za uzalishaji. Hili la nusu nusu halimsaidii mtu yeyote. Kimsingi kwa sasa biashara hamna mengine kama marejesho ya benki, faini na kodi za serikali yako pale pale.

Unayo hoja mkuu.
 
Ninashauri fedha zilizochangwa kwa ajili ya corona zaidi ya billion 7 na ambazo Mh Rais amesema zitumike kusaidia wananchi wa jiji la Dar ili jiji Hilo liwe lockdown haraka iwezekanavyo kwani kutokufanya hivyo Hali itazidi kuwa mbaya Sana.
 
Nina jamaa yangu ameniambia jana mjomba ake alidondoka ghafla pale Mnazi Mmoja akafa on the spot na mwili umezuiwa na serikali kwa vipimo zaidi.

Guys....this shit is really tuwe makini na hii kitu.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
mh!! hatari sana jamani
 
Hata kama mtu ana uhitaji wa mwalimu hawezi kukupa ww, una matatizo ya herufi H, angalia hao ulipoandika Hila, pia hapo ulipoandika Hiki badala ya Ili. Nyie ndio wale mkipewa mwanafunzi wa kike unaishia kumpa account ya facebook.
Sawa mkuu nitajirekebisha, samahani.
 
Inashangaza eti adi vyuo vikuu vinafungwa kwa mda usiojulikana wataftiwe namna Tz ya leo hakuna sehem ambayo haishiki japo mtandao mmoja tu mnaosema hawana computer sjui smartphone huu ni uzembe wa mzazi kumpeleka mwanao chuo bila izo nyenzo sawa na kumtelekeza wanaishia kufanywa vibaya kisa kugongea simu na laptop za wenzao
 
Mkuu si kweli ,hii ni sawa na mtu kukuambia mto X una mamba ,na wewe ni lazima uvuke huu MTO,sasa hii itakupa umakini katika kuvuka na pengine unaweza ahirisha kule ulikokuwa unaenda na kukufanya uwe safe zaidi,so serikali inafanya jambo la kheri kutujulisha idadi yaa wagonjwa na hivyo kutufanya kuwa makini zaidi,hasa kwenye maeneo yenye wagonjwa wengi kama Dar

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa mfumo wa Hospital discharged patients huwa hawahesabiwi ktk wagonjwa waliopo wodini,hii ni mpya.
 
Back
Top Bottom