Serikali: Visa vya COVID-19 vyafikia 53. Vyuo na Shule kuendelea kufungwa hadi Serikali itakapotoa tamko jingine

Serikali: Visa vya COVID-19 vyafikia 53. Vyuo na Shule kuendelea kufungwa hadi Serikali itakapotoa tamko jingine

Rais John Magufuli ameagiza Sh500 milioni ambazo zilitengwa kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 56 ya sherehe za muungano zipelekwe kwenye mfuko wa kupambana na corona wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Source: Mwananchi

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna mabilioni ulipwa mashulen kila mwezi sasa mashule yamefungwa hayo mabilion ya mwezi 1yanaweza kupambana na corona
 
Wenye nazo watatoa ndugu yangu...wapo tu watakaotoa Ila majority ya watz wenzangu hali zetu tunazijua
sio sawa kabisa ndugu, hata kama nina uwezo siwez toa , sio sawa, naona ni kama ufisadi tu ...
ina mana sisi tunavyojitapa kununua ndege kwa cash na kwamba tuna madola bilioni , ni nini? nchi zingine serikali inapambana kuwasaidia wananchi kifedha, chakula na mahitaji mengine, na zaidi wanapewa mikopo na imf, unadhan kwanini tumenyimwa mkopo na imf

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa akili za ki-utu uzima ni rahisi mkuu ila kwa akili za kiuanafunzi, itawachukua muda na nguvu kidogo kurejea katika hali ya kitaaluma psychologically maana kukaa mwezi mzima na sehemu bila serious classes lazima akili ilale kidogo, hivyo wakitafutiwa namna itakuwa bora zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mawazo yako mazuri sana ila kwa muktadha wa Tanzania- sidhani kama hiyo Elimu itakuwa sawa kwa wanafunzi wote. (Hakuna miundombinu wezezeshi Ku 'facilitate' hiyo Elimu)
 
yaani we acha tu.......ndo maana baadhi ya wenye mamlaka wanaamua kujipigia tu wakipata nafasi; maana vyovyote iwavyo watasemwa tu! mwisho wa siku, kutoeleweka kwetu tunaishia kuumia wenyewe tu!
Nchi ina wanafiki na vigeu geu wengi sana, ukiwa kiongozi piga tu na familia yako basi.
 
Mimi nashauri shule zamsingi na secondarily za vijijini zifunguliwe ila sizipokee mwanafunzi mpya nawala asitokee mwanafunzi wakijijini akaja mjini naikitokea akija mjini basi asirudi tena kijijini hii iende sambamba nakwawalimu wao pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sioni kama unaisha leo huu labda January.
Ile spannish flu, ambayo iliua watu kati ya 24m na 39m, ilianza mwaka 1918 ikaisha 1920.

Hapa huu ugonjwa hauwezi kwisha siku za karibuni. Kwisha kwake ni mpaka ipatikane chanjo. Wataalam wa masuala wa chanjo wanasema, the earliest ni baada ya miezi 18.

Tujiandae kisaikolojia kuendelea kuwa na ugonjwa huu kwa muda mrefu.
 
Uwezekano wa kufunga shule J3 haupo, napendekeza mfuko wa kupambana na Covid19 uvisaidie vyuo na mashule viwezeshi vya kuandaa magunzo kwa njia ya mtandao. Imekuwa kawaida walimu na wahazili huamka kwenda ofisini na kurudi nyumbani nothing to do, mbona wasijiongeze kuwawezesha wanafunzi wao kipondi hili cha lockdown ya corona.
Wewe watu tuko kijijini network inazingua kinoma
 
Hivi hamkujua ni tatizo kubwa, ni kubwa kweli. Tusikie tuache ushabiki wa vyama usio na Tija katika janga hili.
Kweli kabisa, hili tatizo ni kubwa pengine tofauti na tunavyolichukulia,
 
Tungelikuwa fuata ushauri was mchungaji msigwa alio utoa bungeni wakati ule wa kabla hata maambukizi hayajaingia nchini tungalifaulu kwq mipango yetu lakininkwa bahati mbaya , uchama na busara za speaker zikaikatisha hoja mbadala kabisa Sasa leo tunaanza kuyaona madhara.

Uongozi SI kubeba cheo na ukuu ni kuwa na maono katika mambo mengi

Sent using Jamii Forums mobile app
Hili tatizo kulikuwa na uwezekano kubwa kabisa ya kulizuia mapema hata kabla halijaingia. Hata pengine lilipoingia kulikuwa na uwezekano mkubwa kabisa kulizuia kwenye stage ya mwanzo.
 
Watoto wanamambo mengi kichwani uwezi amini tunaona vurugu zao huku mtaani

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
Mambo mengi Kama yapi?! Wanawaza Kodi, Ada, stress za kazin na biashara??

Ndo Mana nikasema sekondary na primary hawana effect kubwa kwa sababu wakirudi shule it is very easy to catch up kuliko chuo kikuu.

Na elimu ya juu mfano nchi za wenzetu wanaendelea na online classes(na Wengine pia, ingawa sisi level ya chini haiwezekani).

So ushauri wangu ni kwa elimu ya juu
 
Nchi ina wanafiki na vigeu geu wengi sana, ukiwa kiongozi piga tu na familia yako basi.
na bado unaweza kuwaachia vimaneno flani vya kuudhi wakahangaike navyo huko mbele......km vile 'vijisent', 'ya mboga', 'mimi ni nyoka wa makengeza' n.k😁😁😁
 
Back
Top Bottom