Serikali walikosea kwenye swala la uuzaji wa mahindi

Mkuu hizi roho za kwanini tunazo huku kwetu uswahilini kwenye kuuza bagia na maandazi na bidhaa zingine za dukani, utamzuiaje Zambia asipitishe mahindi kupeleka Kenya wakati ya kwako yapo bei juu? Kinachotakiwa ni kujifunza kwanini mahindi ya Zambia na umbali wote yanakuwa bei rahisi kuliko sie ambao tupo pua na mdomo na Kenya bei inakuwa juu
 
zambia kuna settlers wanaozalisha mahindi mengi na yanaubora mkubwa hao ni wale mugabe aliowafukuza zimbabwe walienda zambia kuendelea na shughuli zao
Ahsante kwa ufafanuzi..badala yake watu tusilalamike tuangalie namna ya kujifunza kutoka Zambia maana sie Kilimo hatukipi uzito unaostahili, watu wanaofanya biashara ya mazao wanaweza wakawa mashahidi kwa hili hasa inavyofika msimu wa mavuno yaani wanakusanya kidogo kidogo mpaka fuso inajaa ni wakulima wachache unaweza ukampelekea gari na likajaa moja kwa moja
 
Mkuu kwa mujibu wa mleta mada anasema wamekataa sababu hawataki mahindi ya Tanzania. Labda tu nitaomba ufahamu wako kuhusu bei za mahindi yetu na Zambia kwa kwa kilo au gunia au vyote.
 
Sidhani kama 2017 tunahitaji kujifunza namna ya kuuza raw materials,
Fikiria zaidi ya hapo mkuu!
 
Ukizuia watapitisha beira port hayooo mpaka Mombasa port, pia kuna ndege za mizigo, mnatuharibia sana hii nchi.
 
Sidhani kama 2017 tunahitaji kujifunza namna ya kuuza raw materials,
Fikiria zaidi ya hapo mkuu!
Napo sema kujifunza sijamaanisha namna ya kuuza raw materials bali kujitathimini wenyewe kwa kuhoji kwanini mahindi ya Zambia ni bei nafuu kuliko yetu pamoja na umbali wanaosafiri plus delay za mipakani (tukifanya hivyo tutakuja na wayforward) ...ndicho nilichofikiria zaidi ya hapo mkuu wangu game over
 
Ukiyasafirisha kwa Ndege unajua kua gharama zake zitakua juu?Kinacho takiwa Nchi hiz zinazo pakana zinahitaji mawaelewano mazuri kwakua zinategemeana kwa kiasi kikubwa.
 
Tatizo kubwa ni mikataba ya kimataifa tunayoingia kama taifa. Unakumbuka Tanzania ilijitoa COMESA wakati wa utawala awamu ya 3 wakat Waziri wetu alikuwa Mh. Idd Simba. Zambia na Kenya bado wako COMESA. Tanzania na Zambia wako SADC. Kenya na Tanzania wako EAC.

Sasa hapa ndiyo migongano ugumu inapoanza. Ukikataza mahindi ya Zambia yasipite Tanzania kwenda Kenya , kwanza unavunja mikataba ya SADC na EAC, pili unaharibu uhusiano na nchi hizi.
 
Mkuu kwa mujibu wa mleta mada anasema wamekataa sababu hawataki mahindi ya Tanzania. Labda tu nitaomba ufahamu wako kuhusu bei za mahindi yetu na Zambia kwa kwa kilo au gunia au vyote.
Mkuu ngoja nifuatilie kuhusu bei mie nimedandia uzi tu kwa kusoma mada nikakuta mstari wa mwisho amezungumzia kuhusu unafuu wa bei ya mahindi ya Zambia na ndipo ilikuwa msingi wa comment yangu ya awali (labda cha msingi ni kupata bei ya mahindi wanayouza Zambia na bei ya mahindi ya kwetu)
 
Kwani lazima yauzwe Kenya, hapo kwa wananchi wa Sumbawanga, Mbeya, Songwe na Ruvuma watayauza Zambia na Kenya watayanunua wakijua yametokea Zambia
Siyo rahisi kivile. Hivi unawajua Wazambia? Pia ujue bei yao ni ndogo kuliko yetu kwa sababu ya Economy of scale,wana mashamba makubwa ya kufa mtu.
 
Ukizuia watapitisha beira port hayooo mpaka Mombasa port, pia kuna ndege za mizigo, mnatuharibia sana hii nchi.
Ndugu, kwanza fahamu kwamba na mimi ni mkulima ambae nina mahindi ndani yanasubiri bei ipande yauzwe ili pesa iingizwe kwenye kilimo tena.
Pili itakuwa vyema endapo utanipatia gharama za kupitisha mahindi toka Zambia, Zimbabwe/Malawi then beira port Mozambique kisha yapakiwe kwenye meli hadi Mombasa port. Baada ya hapo tulinganishe na kutumia tazara railway au Capetown-Cairo highway. Vivyo hivyo na kwa usafiri wa anga pia.
Mwisho lakini muhimu sana, NAIPENDA SANA NCHI YANGU, na KAMWE sitathubutu kufanya/kushiriki jambo au kutoa ushauri wa KUHARIBU nchi yangu, siwezi KABISA.
Na hapo mwishoni kama umesoma vizuri nimetoa pendekezo nini kifanyike.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…