Serikali: Wanafunzi waliopata mimba kuendelea na Masomo katika mfumo rasmi

Shule ya nani ?; Kama ni ya kwangu tafanya navyotaka ila kama sio yangu sina budi kufuata sheria na kanuni za shule husika...

Kwa kumkataza asiendelee tunamkomoa nani? Aliyepata Mimba, au mtoto atakayezaliwa na Mama asiye na mtaji wa Elimu ?, Na huyu Binti ambaye angekuwa nguvu kazi ya taifa hapo baadae kukosa kwake skills na bado kuwa mzazi ni faida kwa nani hasa ?
 
Binti akirudi shule baada ya kujifungua atakuwa tifauti sana na wenzake, hivyo atakuwa psychologically tortured. Hataweza kusoma
 
Haki ya mtoto kusoma haihusiani na ujauzito
Wataoendelea na masomo hongera zao, ila naamini familia nyingi fukara hawata kubali awaachie mtoto na waendelee kumuhudumia mzazi shuleni, labda serikali iende mbali zaidi ishiriki jinsi ya kumtunza mtoto. Kwa familia zenye uwezo suala la elimu kwa mtoto wao haikuwa tatizo toka hapo, walimudu kimpeleka private bila kelele!
 
Mbona baba anafungwa miaka 30 jela kwa kumzaa mtoto
Sheria irekebishwe, tamaduni zinamtambua baba sheria zinamsababisha baba atengane na mtoto wake hivyo mtoto kukosa huduma na upendo toka mzazi wake, tutafakari upya!
 
Sheria irekebishwe, tamaduni zinamtambua baba sheria zinamsababisha baba atengane na mtoto wake hivyo mtoto kukosa huduma na upendo toka mzazi wake, tutafakari upya!
Tafakari inatakiwa hapa, kwann baba afungwe jela na kutenganishwa na mwanae kwa kosa la kumzaa ni kumyima mtoto haki ya kuwa na baba.
Kuzaa sio kosa.
 
Mwanafunzi akizaa arudi shule ila atengwe na wasiozaa Ili asiwaharibu awekwe kwenye wanafunzi wazazi kama adhabu fulani ya saikolojia ya aibu japo kuzaa sio dhambi.
Lengo la QT na elimu ya watu wazima si imewalenga wanafunzi wazazi.
 
ruhusini kutoa mimba uwe Kama ugonjwa mwingine watu watibiwe our serikali sidhani Kama mabweni itajenga
 
Na vipi wanafunzi wanaowapa walimu wao mimba nao warudishwe kuendelea na masomo? Hili halijajibiwa na Waraka wa Mhe. Waziri. Lazima pawepo na gender balance na consistency of actions kwenye kadhia hii ya mimba mashuleni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…