Serikali: Watanzania 66 wameukana Uraia

Serikali: Watanzania 66 wameukana Uraia

Nina wivu na nchi yangu hasa nikiangalia nchi zote Duniani zinavyodhibiti Raia wa kigeni katika nchi zao lakini Tanzania WAGENI wanaingia kiholela na kununua viongozi wote wananua Ardhi kupitia viongozi Wetu lakini tunachekelea wanaishi Nchini Kwa kiburi na kufanya dhuruma mbalimbali EBU WA Tanzania tuamke jamani.
For as long as ccm imetamalaki mambo yataendelea kuwa hivyo na kuzidi🙄
 
Ulaya hata Ukiwa na passport yao, utajua kabisa kuwa hapa Sio kwetu hata kama maisha umeyapatia. Wazungu hawataweza kukuona mwenzao Ila wanaweza kutumia ujuzi wako na akili Zako. Wanajua kuheshimu vipawa. Lakini watakukumbusha kwa namna nyingi kuhusu kwenu na uduni wetu.
Ndiyo sababu ni muhimu Kwa Tz kuruhusu uraia pacha
 
Watanzania hata wakishaingia hizo nchi kwanza hata hawajisumbui kutaka kujua ubalozi wao ulipo au balozi wao ni nani, sababu hata likitokea la kutokea hizo balozi hazijawahi kuwa na misaada sanasana watakua wanawatafuteni kuwapigeni virungu vya ooh changieni nyumbani tujenge barabara, changieni nyumbani kuna mafuriko, changieni nyumbani tukajenge shule, changieni nyumbani tukajenge hospital wakati wenyewe wakiishi maisha ya anasa na wakopewa posho kubwa na kila kitu utafikiri hawatoki hiyo nchi ombaomba
Upo sahihi Mkuu sasa mimi niende Ubalozini kufanya nini wakati nikipata matatizo ndugu na jamaa ndio watakahusika kwa kila kitu Ubalozini wataenda kuchukua barua tuu na wala hawaleti wao tofauti na Balozi za Nchi nyingine huyo Waziri yupo Bungeni hata siku moja ajawahi kuonana na Watanzania waishio Nje ya Nchi kujadili hata Vivutio vya Nchi wapo humo kukamilisha ratiba tuu...
 
Sasa, kama maisha anayotamani ameyapata huko? Nini kawa mganda, hata angekuwa ni Mrundi kabisaa! Kuliko kuwa mtanzania mwenye maisha magumu!
Ndugu yangu Juma; uzalendo wa kutesekea dunia haulipi, labda ingekuwa ni mambo ya Mungu ni sawa.
Niliwahi kufika Paris nikaona maisha ya Waafrika (wengi weusi) huko aisee sikuyatamani Yale maisha
 
Kwa utawala wa nduli mwendazake, nusu ya watanzania wangeukana uraia
 
Mbona sijawekwa kwenye list soon nimetoka kuukana uraia wa Tz nipo Zambia huku
 
Aise uganda oman na falme za kiarabu ' big no bora ni baki tz nilime mahindi. Ila hapo namibia na usa nimepapenda sna
 
Kwanini unapenda unachoamini wewe na wengine wawe hivyo. Fursa ipi kwa mfano. Kuna changamoto sana kuishi nje ya mahali ambapo umekuzoea na kukulia na kujiskia huru na home.

Ulaya hata Ukiwa na passport yao, utajua kabisa kuwa hapa Sio kwetu hata kama maisha umeyapatia. Wazungu hawataweza kukuona mwenzao Ila wanaweza kutumia ujuzi wako na akili Zako. Wanajua kuheshimu vipawa. Lakini watakukumbusha kwa namna nyingi kuhusu kwenu na uduni wetu.

So inategemea wewe binafsi na malengo yako maishani. Kuna raha sana unapotua nyumbani. Changamoto zipo pia. Unatua, then ukianza kuingia Sasa dar mtaani mpango wa majengo na uchafu nk. Unakutia simanzi. Ila ukishatulia unamaliza likizo kwa rahaaaaaa na uhuru usio na hata maelezo. Maswali ya wie lange sind sie schon in Deutschland, wie lange noch? Gibt es bei euch sauberes Wasser wie hier bei uns? Schaut man auch bei euch Fernseher an? Usw.

Kuna Wakati unapata Shida ukipanda train iliyojaa kwa maana ya seat Mbili moja Ina Mzungu tayari na nyingine leer oder frei. Wapo wenye busara anakuwahi na kukuuliza Kama utapenda kukaa. Ni changamoto sana hata kama una miaka 20 na zaidi huku.

Hakuna lebo ya rangi na muda mtu aliokaa na changamoto zitabaki. Mambo Kama haya kwa wengine ni madogo na wengine ni makubwa. Mimi ntakula ma purée yao lakini ntabaki Raia wa Tansania with unbefristetes viza. Lakini wengine wanaona kuna maslahi na haki zinawapita kwa kutokuwa raia. So wanaamua kukana ili wanufaike. Ila daheim ist daheim. Nyumbani Ni nyumbani.
Cha kushangaza nyie wazalendo mkiambiwa mrudi bongo hamrudi. Pumbavu
 
Shehe habari za vuga?
Ni mateso tu ya kijana wa Mkuranga tuliyewekewa na Magufuli. Anatuona sisi ni mafala na harakari zake Za kujitia misikitini huku akiiba Mali Za nchi Kama vile hatumwoni
 
Nina mpango wa kuchukua Uraia Wa Angola au bostwana.

Am serious about this na ntalitimiza
Hata mm pia ndgu nina mpango huo kitambo ongezea namibia hapo.hzo nch naipenda kuliko kwa weupe uropa full kubaguana kisa ngoz tu.ila kwb hao ndgu zetu hakuna hilo hata shamba na bibi napata
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni leo amewasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2023/2024 ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba yake ni kwamba hadi kufikia mwezi May, 2023 Watanzania 66 waliukana uraia wa Tanzania na kupewa uraia wa Mataifa mengine.

“Watanzania hao wamepewa uraia wa Mataifa mengine ikiwemo Canada (6), China (1), Hispania (2), India (3), Marekani (11), Namibia (1), Newzealand (2), Oman (12), Ubelgiji (1), Uingereza (2), Ujerumani (23), Uganda (1) na Umoja wa Falme za Kiarabu (1).

“Hivyo, kwa mujibu wa Sheria ya Uraia Sura ya 357 Rejeo la 2002, wote walioukana Uraia wa Tanzania wanapoteza haki ya kuendelea kuwa Watanzania, katika kipindi kama hicho mwaka 2021/22 Watanzania 40 waliukana Uraia wa Tanzania”.
Mbona ni wachache sana? Why?
Kwa nchi zenye tawala za ki-dhalimu na za kidikteta kama hizi za kwetu hapa Afrika, uamuzi wa kuukana uraia wako ni mzuri, lakini uamuzi wa kuwa na uraia-pacha ni mzuri zaidi.
 
Back
Top Bottom