Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Wiki hii watu wametokwa na povu sana kutokana na matukio mbalimbali yalioashiria mwanzo wa kuanza kutomaswa tomaswa kwa dini zao ambazo zilikuwa zimepewa hadhi maalum ya kuwa zisizogusika au 'untouchables' kwa muda mrefu.
Mzee wa Upako ni mmojawapo wa watu waliotokuwa na povu hilo hadi kufikia hatua ya kutoa vitisho mbalimbali kwa utawala ambao muda mrefu amekuwa swahiba wake wa karibu sana. Wapo waliotokwa na povu na kamata kamata zinazofanywa makinasani
Ni wakati sasa wa Serikali kujifunza na kuisogeza dini mbali kabisa na mambo yake.
Hakuna haja kila jambo la kiserikali linapofanyika likaunganishwa na mambo ya kidini. Hakuna haja ya kuwa na mabaraza ya kidini yenye muelekeo wa ushawishi wa kiserikali.Hakuna haja ya kubebana na viongozi wa kidini katika kila tukio la kiserikali.
Mambo ya kidini yakiwekwa mbali na serikali. Itakuwa na faida kubwa kwa serikali, viongozi wa dini na waumini wa dini kwa sababu wote watakuwa na uhuru mkubwa wa kutenda na kusimamia yale wanayoamini ni sahihi na yenye maslahi kwao.