Serikali ya Awamu ya 6 kuanza kuwapa wafungwa mitaji. Hii ndio "legacy" itakayoishi daima

Serikali ya Awamu ya 6 kuanza kuwapa wafungwa mitaji. Hii ndio "legacy" itakayoishi daima

Kwani Awamu ya 6 IMEINGIA KWA UCHAGUZI GANI? Msitupotoshe hii ni ya AWAMU YA 5 KIPINDI CHA PILI CHA KUHITIMISHA MIAKA 10 YA AWAMU YA 5
Labda ueleweshwe awamu inahesabiwaje. Awamu ni kipindi anachokaa madarakani rais. Awamu ya rais husika hukoma pale anapoondoka kwenye madaraka haijalishi amekaa vipindi vingapi. Hivyo awamu ni rais, vipindi ni uchaguzi.

Hivyo hamna kitu cha rais B kumalizia awamu.ya A.

Kulingana na katiba yetu rais anaepokea kipindi kilichokuwa cha awamu ya mtangulizi wake na kipindi hicho hakijavuka nusu yake, kipindi hicho kitahesabiwa kipindi cha kwanza katika awamu ya rais huyo mpya. Hivyo rais huyi atakuwa na fursa kuongoza tena kwa kipindi kingine kimoja
 
wafungwa huwa wanafanya kazi asubuhi hadi saa nane mchana, kazi ngumu alafu wanapewa chakula mara moja tu kwa siku tena ugali maharage nusu sahani.

hio mitaji labda itakuwa elf 30 na hapo kuna rushwa kidogo inabidi afande achukue 10 yake akuachie 20
 
Nawasalimu kwa jina la JMT.

Kuelekea kuadhimisha mwaka mmoja wa Rais Samia S. Hassan, nimekutana na hii habari iliyonikosha sana.

Kwamba Serikali ya mama itaanza kutoa motisha na mitaji ya fedha na vifaa kwa wafungwa wanaomaliza vifungo vyao.

Kwa kuanzia wataanza na gereza kuu la mkoa wa Mbeya.Hii ni habari njema kwa wafungwa ambao wanakuwa waneshiriki katika uzalishaji mali wakiwa magerezani lakini wanaachwa solemba wakimaliza vifungo.

Hili ni jambo jema na moja ya legacy yenye nguvu ya kukumbukwa kwa madam President atakapomaliza mda wake.

Kongole kwa wahusika wote.

View attachment 2147669
😍
 
Wafungwa wanazisha sana huko Magereza na wengine walikuwa wanatumikishwa kulima mashamba ya watu na wakubwa wanachukua hela

Kuna miradi mingi na huko kwa hiyo ni wazo zuri wapewe hela kidogo ya kuanzia ila sidhani kama uhalifu utaongezeka kwa sababu mtu mwema hawezi kuwa mbaya ghafla kisa kuna laki 5 au 1m baada ya kifungo

Kumbuka hakimu anaweza kukufunga kwa mujibu wa vitabu na sheria zilivyo kwa mfano unakuta kifungo kuanzia miaka 3 hadi 10 sasa inategemea hakimu atakavyoamua

Yaani nikafungwe miaka 10 kwa ajili ya laki 5 hizo ni akili kweli
 
Badala ya kuboresha maisha ya wafungwa,
Na kuwalipa mishahara kwa kazi wanazofanya gerezani,
Mnatwambiya Mambo ya kuwapa mitaji.

Hivi mfungwa amepasua mawe,
Amelima hekari kibao.
Amepasua mbao kwa miaka 10.

Uje umpe mtaji milioni au milioni 2 mkopo?

Ingekuwa anapata mshahara angepata sh ngp akitoka?

Mfungwa anaishi mazingira mabovu,
Machafu,
Magumu.

Unadhani anawezaje kuishi gerezani kwa miaka yote ?
Atoke salama aje apewe huo mkopo?

Vitu vingine ni vyanzo vya upigaji na wala havipo kwenye kusaidia wafungwa.

Weka system kila mwezi mfungwa alipwe pesa kutokana na kazi anazofanya.
 
Nawasalimu kwa jina la JMT.

Kuelekea kuadhimisha mwaka mmoja wa Rais Samia S. Hassan, nimekutana na hii habari iliyonikosha sana.

Kwamba Serikali ya mama itaanza kutoa motisha na mitaji ya fedha na vifaa kwa wafungwa wanaomaliza vifungo vyao.

Kwa kuanzia wataanza na gereza kuu la mkoa wa Mbeya.Hii ni habari njema kwa wafungwa ambao wanakuwa waneshiriki katika uzalishaji mali wakiwa magerezani lakini wanaachwa solemba wakimaliza vifungo.

Hili ni jambo jema na moja ya legacy yenye nguvu ya kukumbukwa kwa madam President atakapomaliza mda wake.

Kongole kwa wahusika wote.

View attachment 2147669
Mama anatafuta popularity ya kisiasa tu!hiyo haina tija!!ameshindwa kuandaa mitaji ya graduates. Wa chuo kikuu ambao wanalia ajira hamna anakuja na mitaji kea wafungwa si ndio!!??
 
Mama anatafuta popularity ya kisiasa tu!hiyo haina tija!!ameshindwa kuandaa mitaji ya graduates. Wa chuo kikuu ambao wanalia ajira hamna anakuja na mitaji kea wafungwa si ndio!!??
Haina tija kwa nani labda,atafute cheap popularity ya nini hasa?
 
Badala ya kuboresha maisha ya wafungwa,
Na kuwalipa mishahara kwa kazi wanazofanya gerezani,
Mnatwambiya Mambo ya kuwapa mitaji.

Hivi mfungwa amepasua mawe,
Amelima hekari kibao.
Amepasua mbao kwa miaka 10.

Uje umpe mtaji milioni au milioni 2 mkopo?

Ingekuwa anapata mshahara angepata sh ngp akitoka?

Mfungwa anaishi mazingira mabovu,
Machafu,
Magumu.

Unadhani anawezaje kuishi gerezani kwa miaka yote ?
Atoke salama aje apewe huo mkopo?

Vitu vingine ni vyanzo vya upigaji na wala havipo kwenye kusaidia wafungwa.

Weka system kila mwezi mfungwa alipwe pesa kutokana na kazi anazofanya.
Sio mkopo,watapewa pesa ya mtaji ya bure kwa kuthamini Kazi yao wakiwa magerezani.

Badala ya kupongeza unapinga ,hii ni hatua nzuri, maana kuna kipindi wanatoka hawana pa kuanzia wanafanya tena uhalifu wanasema Bora wakaendelee na maisha ya kifungo waliyozoea.
 
watu wanafanya kazi asubuhi hadi saa nane mchana, kazi ngumu alafu wanapewa chakula mara moja tu kwa siku ten ugali maharage nusu sahani, hio mitaji labda itakuwa elf 30 na hapo kuna rushwa kidogo inabidi afande achukue 10 yake akuachie 20
Sio poa kila jambo kuwaza negative
 
Mtaji wa shilingi laki5 au hata milioni1 kwa mtu aliye tumikia kifungo cha miaka10 unamsaidia nini?? Zaidi zaidi ataenda kulewea
 
Mtaji wa shilingi laki5 au hata milioni1 kwa mtu aliye tumikia kifungo cha miaka10 unamsaidia nini?? Zaidi zaidi ataenda kulewea
Kwanza kwa hiyo laki tano ni ya kupanga frem au ya biashara kwani awezi kufanya Machinga kwa kuwa harusiwi.
Hapa bado wanaodanganya hawamsaidii.
Swali la kumuuliza ni hili kati ya Wamachinga na Wafungwa ni ipi idadi kubwa kwani hili swala limekuja kisiasa baada ya kujifarakanisha na Wamachinga.
Nakumbuka kuna Wakili amepanga kufungua kesi ya Wafungwa warusiwe kupiga kura.
Sasa imeshaonekana huyu Wakili anaenda kushinda kwa hiyo itafutwe njia ya kuwatumia ili kura zisikosekane.
Ila swala la Machinga Chama changu kimekosea sana namna ya kudili nao.
Mfano pale kwa Msuguri kuna watu walikuwa na biashara pale na wameondolewa na ukipaangalia ilikuwa hakuna haja ya kuwaondoa wale watu hata jana kuna gari ilikuwa inavunja hapa Kimara Korogwe sijui kama Mama analijua hili au anaujumiwa bila yy kujua.
 
Sio mkopo,watapewa pesa ya mtaji ya bure kwa kuthamini Kazi yao wakiwa magerezani.

Badala ya kupongeza unapinga ,hii ni hatua nzuri, maana kuna kipindi wanatoka hawana pa kuanzia wanafanya tena uhalifu wanasema Bora wakaendelee na maisha ya kifungo waliyozoea.
Kwanza waboreshewe magereza,

Pili walipwe mishahara kwa wanachofanya gerezani.

Mambo ya kumlipa mtu 50000 baada ya kutumikia kifungo ndy umemsaidia nn?
 
Nawasalimu kwa jina la JMT.

Kuelekea kuadhimisha mwaka mmoja wa Rais Samia S. Hassan, nimekutana na hii habari iliyonikosha sana.

Kwamba Serikali ya mama itaanza kutoa motisha na mitaji ya fedha na vifaa kwa wafungwa wanaomaliza vifungo vyao.

Kwa kuanzia wataanza na gereza kuu la mkoa wa Mbeya.Hii ni habari njema kwa wafungwa ambao wanakuwa waneshiriki katika uzalishaji mali wakiwa magerezani lakini wanaachwa solemba wakimaliza vifungo.

Hili ni jambo jema na moja ya legacy yenye nguvu ya kukumbukwa kwa madam President atakapomaliza mda wake.

Kongole kwa wahusika wote.

View attachment 2147669
Kwa kweli ni jambo jema mno na huenda likaigwa na Mataifa mengine kwa kujifunza kutoka kwetu. La msingi sasa ni kuweka dhamira ya dhati katika Utekelezaji wake. Aidha Wahusika ( Watoa Mtaji = Serikali na Waliopata Mtaji=Wanufaika) kuzingatia Taratibu zitakazowekwa(Vigezo na Masharti) ili kupewa Mtaji. Jambo lingine ni Kuzingatia Viashiria vitakavyowekwa hususan vile vya Udhibiti wa Usimamizi na Ufuatiliaji (Supervision,Monitoring and Evaluation) wa Utekelezaji kwa Upande wa Walengwa/Wanufaika. Yule Mnufaika atakayebainika kufanya Matumizi au kwenda kinyume cha Malengo kama alivyobainisha Mwenyewe kwenye Hati ya kupewa Mtaji awajibishwe. Wanufaikaji wapewe ka-Elimu kidogo ihusuyo namna ya Utekelezaji wa Miradi wanayokusudia kwenda kufanya kwa kutumia Mitaji watakayopewa. Elimu hiyo itolewe Kabla ya kupewa Mtaji.
Kwa upande wa Wasimamizi na Wafuatiliaji (Watoa Mtaji) iundwe Timu Shirikishi itakayojumuisha: Maafisa wa Magereza, Maafisa wa Halmashauri na Watu-raia binafsi wa kuteuliwa. Iwe ni Hitajio la Lazima kwa wasimamizi KUTOA TAARIFA ya Mwenendo wa Utekelezaji KILA mwezi na watakaoshindwa kutimiza hilo Wawajibishwe Ipasavyo mara moja.
 
Back
Top Bottom