Serikali ya Awamu ya 6 kuanza kuwapa wafungwa mitaji. Hii ndio "legacy" itakayoishi daima

Serikali ya Awamu ya 6 kuanza kuwapa wafungwa mitaji. Hii ndio "legacy" itakayoishi daima

Mfano Bilionea Rugemalila angefungwa akitoka angepewa mtaji wa kuanzia maisha?

Au hiyo mitaji itakuwa inatolewa kwa kivipi maana mwingine anaingia jela akiwa Tajiri hatari
 
Mfano Bilionea Rugemalila angefungwa akitoka angepewa mtaji wa kuanzia maisha?

Au hiyo mitaji itakuwa inatolewa kwa kifupi maana mwingine anaingia jela akiwa Tajiri hatari
Mimi nadhani kutakuwa na Mchujo. Yaani kutakuwa na Mchakato wa kuwapata Wahitaji/Walengwa halisi. Unaweza kukuta mwombaji sio tajiri lakini kwa namna ya mwenendo wake anavyofahamika e.g. wale "makokap' " au "wakorofi naturally" = "wasumbufu" watakuwa hawapewi. Hapo ni Weledi utumike katika kuwapata Walengwa. Kwa Mfano - Mchakato unaotumiwa na TASAF kuwapata Walengwa. Mapungufu yatakuwepo lakini kadri muda utakavyoenda, kutakuwa na kufanya maboresho.
 
Kwanza waboreshewe magereza,

Pili walipwe mishahara kwa wanachofanya gerezani.

Mambo ya kumlipa mtu 50000 baada ya kutumikia kifungo ndy umemsaidia nn?
Kulipwa salary ni jambo halipo,hiyo Kazi wanafanya ni sehemu ya mafunzo yao ya kurekebishwa tabia na wajibu wao kujenga Nchi.

Ndio maana wakimaliza kifungo wanapewa kiasi cha kuanzia maisha uraiani.
 
Lakini wafungwa wengi ni maskini,hizo sio pesa za kugawa tuu so vigezo na masharti kuzingatiwa.
 
Kulipwa salary ni jambo halipo,hiyo Kazi wanafanya ni sehemu ya mafunzo yao ya kurekebishwa tabia na wajibu wao kujenga Nchi.

Ndio maana wakimaliza kifungo wanapewa kiasi cha kuanzia maisha uraiani.
Kupasua mawe ndy kumfunza mtu tabia?

Mimi nilidhani watapelekwa shule na kuwafundisha kazi za stadi za mikono?

Yaani kumlimisha mfungwa na kumpa bakuli la uji usio na chumvi ndy kurekebisha tabia.

Kwa maana hyo hata huo mtaji baada ya kifungo itakuwa ni stress za uchaguzi za 2025..

Ndy maana tukaona kuna mwanachama mmoja ameamua kupeleka kesi mahakamani kuruhusu wafungwa wapige Kura.

Sasa ndy nimeelewa.
 
Nawasalimu kwa jina la JMT.

Kuelekea kuadhimisha mwaka mmoja wa Rais Samia S. Hassan, nimekutana na hii habari iliyonikosha sana.

Kwamba Serikali ya mama itaanza kutoa motisha na mitaji ya fedha na vifaa kwa wafungwa wanaomaliza vifungo vyao.

Kwa kuanzia wataanza na gereza kuu la mkoa wa Mbeya.Hii ni habari njema kwa wafungwa ambao wanakuwa waneshiriki katika uzalishaji mali wakiwa magerezani lakini wanaachwa solemba wakimaliza vifungo.

Hili ni jambo jema na moja ya legacy yenye nguvu ya kukumbukwa kwa madam President atakapomaliza mda wake.

Kongole kwa wahusika wote.

View attachment 2147669
huko ni kuchochea ongezeko la uhalifu nchini, kwanini mtaji wasipewe wanavyuo wasio na ajira waliotumia muda kupambania Elimu au wananchi wasiojiweza kabisa na waliopo ktk hali ngumu?
 
Lakini wafungwa wengi ni maskini,hizo sio pesa za kugawa tuu so vigezo na masharti kuzingatiwa.
Ni kweli wafungwa wengi ni maskini na pesa hizo hazitakuwa ni "Mgawo". Lakini pia kumbuka kuna Maskini-Jeuri. Hata huku uraiani wapo. Unakuta mtu hali yake sio nzuri ki-vile lakini hata akihamasishwa haelekei e.g. haendi/hahudhurii kwenye mikutano na hataki/hakubali aonekane hivyo na kila jambo yy analipuuzia au anapinga bila sababu.
Vivyo hivyo inakuwa kwa Wafungwa. e.g. Wapo wafungwa wanasubiri tu tar. ya kumaliza kifungo na waondoke na huwaona Maafisa Magereza kama ni mojawapo wa Maadui.
Ni kama watasema "Niache kama nilivyo"
 
Kwanza waboreshewe magereza,

Pili walipwe mishahara kwa wanachofanya gerezani.

Mambo ya kumlipa mtu 50000 baada ya kutumikia kifungo ndy umemsaidia nn?
Mkuu; Nakubaliana na wewe hoja ya Magereza yaboreshwe(Ikiwa ni pamoja na Huduma wanazopata Wafungwa). Lakini eti walipwe mishahara? HAPANA. Kama wanapewaga Tzs 50,000/= baada ya kutumikia kifungo, nadhani hiyo ni Ubinadamu/Hisani na ni kwa ajili ya kumsaidia aweze kupata au aitumie kwa ajili ya nauli kurudi makwao. Kama huwezi kushukuru hata kwa kile kidogo ukipatacho, Hutashukuru hata ukipewa kikubwa.
 
kwanini mtaji wasipewe wanavyuo wasio na ajira waliotumia muda kupambania Elimu au wananchi wasiojiweza kabisa na waliopo ktk hali ngumu?
Wanavyuo wasio na ajira wapo huru na fursa zipo nyingi - Nyingi sana. Tatizo kwa hao wasomi wa leo ni kushindwa kubaini (Identify) fursa zilizopo, kuchagua mojawapo na kuwa Tayari kuthubutu kufanya. Wanataka wafanye kile walichosoma vyuoni. Swali: Je, Hizo Ofisi za kuwameza wote hao zipo? Kama hazipo, basi ni muhimu wao waanzishe Ofisi zao wenyewe i.e. Wajiajiri wenyewe. "Ofisi" hizo ndo Fursa iliyopo yaani Biashara, Kilimo/Ufugaji na Utoaji Huduma halali e.g.Bodaboda,Udereva n.k. Wanao Ndg. Marafiki, Wafadhili, Vikundi n.k.
Wafungwa hawako Huru. Hawana hata chaguo/Fursa moja. Hawana pa kushika. Sasa kunajitokeza haka ka-mwanga kwenye hili la Kupewa(Sio kukopeshwa) Mtaji wa kuanzia. Sasa tena ww unataka hata hichi kidogo wanyang'anywe wapewe wale walionacho?
Jamani tuwe na Huruma.
 
Mtaji wa shilingi laki5 au hata milioni1 kwa mtu aliye tumikia kifungo cha miaka10 unamsaidia nini?? Zaidi zaidi ataenda kulewea
Kama kweli aliweza kuvumilia kifungo kwa miaka 10 atakuwa amejifunza kazi fulani, atakuwa amepata uzoefu katika Fani fulani, lakini zaidi atakuwa amejifunza Umuhimu na Maadili ya kuwa Raia mwema. Kwa mantiki hiyo akipewa laki tano au hata milioni moja na akipewa Mafunzo na Kusimamiwa/Kufuatiliwa vizuri nina uhakika atakuwa amesaidiwa sana. Mtaji watakaopewa utakuwa na Utaratibu wake wa Kuzingatiwa. Hivyo Kulewea Mtaji huo itakuwa si rahisi ki-vile. By the way, hebu wapewe halafu majibu yataonekana ni +ve au -ve. Time will tell.
 
Nchi zilizoendelea mfungwa kila kazi anayofanya ya uzalishaji pesa yake anawekewa pembeni siku akitoka anapewa malipo yake
 
Back
Top Bottom