Serikali ya CCM haifurahi ukiwa na kiasi kikubwa cha fedha benki, unafilisiwa kwa kupewa kesi ya Uhujumu Uchumi

Sasa kwa nini wakulazimishe ukubali makosa kwa DPP pindi wanapokusomea kesi kwenye mahakama ambayo haina uwezo wa kusikiliza kesi yako
 
Kwahiyo kumbe Jiwe kaifirisi nchi tayari sasa anataka aingie kwenye vim-pesa,vibubu & viziwi
 
Umesahau kuwa awamu hii waliambiwa: wote waliokuwa wanaishi kama malaika sasa wataishi kama mashetani. Wamewahi kwenda kwa malaika waendeleze maisha yao huko. Pepo ikichukuliwa na Shetani si pepo tena!
We acha watu wema na wa maana kwenye Jamii wanaondoka yanabaki mabashite type
 
Najua kesi ya jamaa yangu wa karibu kabisa aliyepigwa zaidi ya mil 90. Kashindwa kutoa hela, kaenda kuuliza anaambiwa nenda makao makuu ya Benki, huko wakamwabia serikali inasema kuna mashaka na hela yako... kabanwa mbavu aeleze amezipataje. Bahati mbaya jamaa biashara zake hazikuwa rasmi (kilimo), akakosa vithibitisho. Wakataifisha.
 
Unatakiwa kuelewa kodi ni nini na aina za kodi. Unaweza kuwa na fedha nyingi benki lakini kusiwe na uhitaji wa kulipa kodi. Kwa maoni yangu naisihi serikali kupitia TRA iachane na huu mtindo wa kuzuia account. Hakuna kazi kubwa kama kuwafanya raia waamini bank.
 
Watu wengi tayari wameshaweka mahela yao ndani,sema kitakachofuata ni serikali kubadilisha note hasa za elf kumi na elfu tano.wataweka deadline ya muda mfupi ili walio na mahela nyumbani yawafie humo.

Dawa ni kutunza fedha za kigeni,dolar,pauni,Eur .

sema pia wakati wa ubadilishaji kama unataka hela nyingi watakuzingua.

Ila bank siyo salama tena mkuu.kama kuna mchezo wa kubambikiwa makosa na kunyang'anywa akiba zako.mtu umejinyima umekusanya vimilio mia kadhaa kwa malengo maalumu halafu unatupiwa kosa la uhujumu uchumi
 
We acha watu wema na wa maana kwenye Jamii wanaondoka yanabaki mabashite type
Ile Tanzania ya kisiwa cha amani ni ndoto. Ilikuwa pepo kwa mzawa na mgeni pia. Sasa ni jehanamu kwa wote. Hakuna mwenye furaha. Tabasamu la kinafiki tu. Kumbuka hao tumewaombea wawekwe mahali pema peponi. Kufa ni faida! Kuna siku niliwaza hawa Ruge, Singa na masheik wa Uamsho watatoka lini jela ya bila hatia! Nikapitiwa.

Kuamka nikamsikia anayewashikilia huko akisema hatosaini wauaji wanyongwe hadi kufa. Nikawaza kuwa naye ni muuaji anayesutwa na dhamiri yake. Nikamaizi sijaamka naota tu. Jinamizi la mchana!
 
Kiwa na hela bank siyo salama kabisa katika utawala huu wa kijamaa wenye vi-element vya kikomunist mamboleo
Wakishamaliza kuzichungulia kwenye mabenk wataamia kwenye simu.
Salama ni bank za nje unavuka boda unaweka unarudi,siku hazigandi ikipita awamu hii unazirejesha Kama walivyofanya watu Zama za Nyerere
 
Duh, hii inasikitisha unakuta Mtu umejinyima mengi kukusanya hizo pesa...labda ili ulitaka uje uanze jambo lako la maana hapo mbeleni.
 

Bila kuusujudia na kuhubusu msalaba hao watu wataozea jela
 
Duh, hii inasikitisha unakuta Mtu umejinyima mengi kukusanya hizo pesa...labda ili ulitaka uje uanze jambo lako la maana hapo mbeleni.
Am telling you... kujionyesha kama una hela sasa hivi ni hatari. Uwe na maelezo ya kutosha

Watakubana kutaka kujua kama ni halal, wakitoka hapo watataka kujua kama umelipa kodi etc etc
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…