Serikali ya CCM haifurahi ukiwa na kiasi kikubwa cha fedha benki, unafilisiwa kwa kupewa kesi ya Uhujumu Uchumi

Si ajabu benki zote Nchini hutakiwa kila siku kupeleka Serikalini list ya wateja wote wenye akiba kuanzia milioni 100 kwenda juu ili ipange mikakati ya kupora asilimia kubwa ya pesa hizo au kukomba zote. Utabambikiwa kesi fake ili warahisishe dhulma yao. Tanzania si Nchi SALAMA.
 
Mkuu figganigga ,ulichokiandika kina ukweli mkubwa sana.
Mimi ni mhanga wa unyama wa serikali ya awamu ya tano.
Kilichonisaidi tu ni kwamba nimefanya kazi taasisi/idara nyingi kulikopelekea kuwa na wingi wa watu ninaofahamiana nao na walioshika mpini, na pia kuwa na jina la ukoo wa kiongozi mmoja mkubwa wa enzi za Mwalimu Julius.
Nimejifunza kuhusu cryptocurrencies,na ndio nawekeza huko.
 
Vilevile kuna hukumu zinatolewa bila hata ya Kwenda Mahakamani. Mfano TCRA iliwapiga faini Airtel: 1.6 bilioni, TTCL: 1.6 bilioni, Halotel: 900 milioni, Zantel: 850 milioni, Tigo: 500 milioni na Vodacom: 450 milioni.
Mkuu hata Marekani,huwezi kuweka mamilioni ya dola bila kuulizwa umepataje,
Pia nenda kasome sheria ya mawasiliano kwanza halafu uje kulalamika kuhusu fine kwa hao defaulters wa taasisi za mawasiliano
 
Yeah true black market inasaidia kukuza uchumi..
inachotakiwa ni kidhibiti na sio kusafisha kabisa inchi iwe ya kilokole....
Serikali inatakiwa kuwa na watu smart kujua namna ya kucheza na mambo hayo
Ndomana mtu kama uhuru ukienda kenya na hela na unataka kuwekeza kwake hakuulizi pesa umeitoa wapi as long tu we utawekeza kwake na mambo kwake yataendaa
Kwengine ukingia na hela nyingi kwanza utahojiwa hela umeitoa wapi blh blh
Ndomana unaona kuna nchi fulani mijengo kibao imesimama
Pesa yoyote chafu ukipata unaweza itumia kwa kufanya kitu kisafi na pesa safi unaweza itumia kwa kufanyia kitu kichafu....huu ni kama mchezo

Ova
 
Unaleta hela nyumbani lakini bado inaonekana adui, ukisikia uzwazwa ndio huu.
 
Nimesoma comment nyingi na inaonekana mleta thread hii kafanikiwa kuwafanya wachungaji kuwa emotional.

Je tunafurahia watu wanaomiliki pesa bila takwimu sahii za mapato na Kodi?

Unatoa wapi pesa kihalali ili zijae tu banki? Acheni ujinga lipa Kodi

Wengi wanaolialia ni wezi , matepeli n wizi wakubwa. Fuateni njia halali na muwe bold kujustfy utajiri wenu
 
Siongezi neno lolote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…