Serikali ya CCM haifurahi ukiwa na kiasi kikubwa cha fedha benki, unafilisiwa kwa kupewa kesi ya Uhujumu Uchumi

Serikali ya CCM haifurahi ukiwa na kiasi kikubwa cha fedha benki, unafilisiwa kwa kupewa kesi ya Uhujumu Uchumi

Ukqeli mtupu huu, yajayo yanaogopesha.
Benk siyo mahala salama pa kuweka pesa kwani zinawindwa na TRA vinara wa Rushwa wafunge account huku vyombo vingine vikiwinda wakubambikie kesi za utakatishaji fedha na uhujumu uchumi wapate kukupora hizo fedha
 
Inatia hasira sana hii,ma DC, RC ,wakurugenzi,mawaziri nk wao ruksa kufanya chochote,ila wavuja jasho ambao hata hawajui mitaji wameipataje wanahenyeshwa sana
Account ya viongozi wa umma hata ikiwa na trilion 10 hawasumbukia nayo, wabebakia kupora Account za wafanyabiashara wa kawaida kwa uonevu manyanyaso makubwa kwenye Nchi yao
 
Waanze kufunga Account za watumishi wote wa TRA na BOT watakaobainika kuwa na pesa nyingi kinyume na vipato vyao halisi, kwani wao hufunga Account za wafanyabiashara kienyeji kwa uonevu kutengeneza mazingira ya Rushwa, sasa iwe zamu yao kufunga Account zao wajue uchungu wa mtu kufungiwa Account kienyeji
 
Na kweli katika kipindi hiki kigumu inakuwaje unapata hela kuliko sisi?
Huu ndiyo upumbavu unaleta Athari za Benk kukosa wateje , kwani kuwa na pesa nyingi lazima ziwe zimepatikana sasa? Watu wana akiba zao za kipindi kirefu na bado zinaporwa kienyeji kwa njia haramu za kishetani, watu wanauza nyumba mashamba mazao madini na vinginevyo waache kuweka pesa Benk kisa wewe una wivu na hao TRA vinara wa kufunga Account nao wana njaa ya Rushwa? Acha wivu tafuta pesa zako Wivu utakuua ukiwa masikini mkubwa.
 
Benk siyo mahala salama pa kuweka pesa kwani zinawindwa na TRA vinara wa Rushwa wafunge account huku vyombo vingine vikiwinda wakubambikie kesi za utakatishaji fedha na uhujumu uchumi wapate kukupora hizo fedha
Haswaaaaah
 
Mabenk yasipozinduka na kukataa ujinga wa Account za wateja wao kufungwa hovyo hovyo na TRA wajiandae kufirisika kwa kukosa wateja baada ya imani na mabenk kuendelea kushuka zaidi
Tatizo Bank wakigoma BOT wanaweza kuwafutia leseni....Nchi inaongozwa na washamba!! Hawaangalii impact itakayosababishwa na uhuni wao.
 
imani na mabenk inazidi kushuka hasa baada ya wateja kugundua mabenk hayajachukua hatua zozote kuzuia ujinga wa maofisa wa TRA kufunga Account za wafanyabiashara hovyo hovyo kienyeji kwa njia haramu za kishetani kutengeneza mazingira ya Rushwa .
 
Tatizo Bank wakigoma BOT wanaweza kuwafutia leseni....Nchi inaongozwa na washamba!! Hawaangalii impact itakayosababishwa na uhuni wao.
Siku Benk zikianza kufa ndipo BOT watajutia ujinga wao ambao Uganda Zambia kenya wametumia fursa hizo kuwaalika wafanyabiashara kwenda kuweka fedha zao huko kusiko na usumbufu wowote, mmiliki wa pesa yupo huru na pesa yake.
 
Kama mnahifadhi ndani hakikisheni ni dollar etc za kigeni maana Hawakawii kuprint note mpya Halafu siku ya kurudisha ikawa ndio msala zaidi... Kenya majuzi walivoprint note mpya watu walitaka wazilete hadi tz wabadilishe....
 
Nimesoma comment nyingi na inaonekana mleta thread hii kafanikiwa kuwafanya wachungaji kuwa emotional.

Je tunafurahia watu wanaomiliki pesa bila takwimu sahii za mapato na Kodi?

Unatoa wapi pesa kihalali ili zijae tu banki? Acheni ujinga lipa Kodi

Wengi wanaolialia ni wezi , matepeli n wizi wakubwa. Fuateni njia halali na muwe bold kujustfy utajiri wenu
Wazazi wako wamepata hasara
 
Salaam Wakuu,

Nmeanza kuelewa kwanini Matajiri wengi wa Tanzania wanaficha fedha zao nje ya Nchi. Siwalaumu tena. Na kama hii hali ikiendelea, Benki nyingi zitatikisika kiuchumi kwani watu watasusa kupeleka hela.

Zamani Watanzania wengi walikuwa hawapeleki fedha zao benki. Walikuwa wanazichimbia mashambani na wengine kuzilalia kwenye Vitanda vya Kamba. Hii walikuwa wanafanya kwa kuhofia kunyang'anywa fedha zao na Serikali. Mabenki yalifanya Kampeni kubwa kuwabembeleza watu wapeleke fedha benki na Wakafanikiwa.

Hii hali sasa imerudi kwa kasi hivi Karibuni. Nini kinafanyika?

1. Wanafuatilia benki una kiasi gani, Wakikuta hela ni nyingi Wanazizuia, Ukienda kutoa hazitoki wanakuambia zinafanyiwa Uchunguzi.

2. Wanabuni mbinu watazipataje hizo hela, hivyo ramani inachorwa ya kuzipata kwa kuangalia makando kando yako. eidha unaweza ambiwa:
i) Unamiliki fedha zisizoendana na Kipato chajo
ii) Hujalipia kodi, au umepata kwa Udanganyifu.

3. Utakamatwa na kufunguliwa kesi isiyo na dhamana Uhujumu Uchumi.
i) Utakatishaji fedha
ii) Kuongoza genge la Uharifu
iii) Kukwepa kodi nk

4. Unalazimishwa uonge nao mfanye Makubaliano ni kiasi gani cha fedha utawapa ili Uachiliwe huru

5. Unalazimishwa ukiri kosa halafu Unapigwa faini na fedha zako zinachukuliwa. Faini haizidi fedha ulizo nazo, wanazijua hivyo wanajua utalipa tu.

Baada ya hapo Wanakuachia huru unaendelea na kazi zako. Unaanza upya kujitafutia kipato, kikiongezeka Mzunguko unaanza tena hapo kwenye maelezo namba moja.

Hakika aduni wa Mtanzania ni Mtanzania.

Hapa chini naweka Mifano Michache ya Watu waliochezewa hii style ya kunyang'anya watu fedha zao ukiachilia mbali Tariq Machibya maarufu Mr Kuku.

1. Mwandishi wa Habari za kiuchunguzi Ndugu Erick Kabendera

2. Aliyekuwa Rais wa Migodi ya Pangea North Mara, Exploration na Bulyanhulu, Deogratius Mwanyika

3. Wafanyabiashara saba wa mafuta wakiwemo Wakurugenzi wa Kampuni ya SHIN UP Tanzania limited Zhang Zhi XIN, LINCOLN

4. Mkurugenzi mkuu wa Benki M Tanzania, Sanjeev Kumar

5. Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura

6. Astery Ndege aliyekuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers

7. Mfanyabiashara Daniel Chizua aliyedaiwa kukutwa na Kobe Wawili

8. Raia wa China, Liang Hu aliyedaiwa kuua Tembo 511

9. MKURUGENZI wa Uwezeshaji wa Kampuni ya Yapi Markez inayojenga Reli ya kisasa Standard Gauge, Yetkin Genc Mehmet

10. Wafanyabiashara Noah Mmasanga, Richard Boniface, Ally Said na Mosses Mbojo na wengine wengi.

Vilevile kuna hukumu zinatolewa bila hata ya Kwenda Mahakamani. Mfano TCRA iliwapiga faini Airtel: 1.6 bilioni, TTCL: 1.6 bilioni, Halotel: 900 milioni, Zantel: 850 milioni, Tigo: 500 milioni na Vodacom: 450 milioni.

Je, ni lini Tutapata Mabilionea Wapya sababu Waliopo Wanazidi kuaga dunia.

Nashauri wachunguzi wa mambo wafanyie kazi Vifo vya hawa Matajiri wa Kitanzania ambao wamekufa kwa kufuatana . Isijekuwa ni hela zao zimewatoa roho. Mungu alaze roho zao mahali pema peponi Subhash Patel, Mr Reginald Mengi, Dr Rajni Kanabar, Ali Mufuruki, Salim Hassan Turky, Mr Salum Shamte nk.


Umenikumbusha wanaijeria na wanawest Africa wengi wanaofanya shughuli ndogo ndogo ambao wakitaka kutuma hela wanaomba kusaidiwa na Sisi wenye Account zinazoweza kutoacha maswali mengi kwa Serikali. Naomba kuwaarifu Hakuna Nchi yoyote makini iliyoendelea isiyofuatilia accounts na ulipaji kodi. Unapataje hela yako Nk. Hakuna. Naomba muache kudanganyana HUKU MNADAI maendeleo. Maneno mengi Kumbe washamba tu. Hamjui hata mnataka Nini Sasa.
 
Sasa hali imekuwa mbaya zaidi na taasisi zisizo za kifaida zinafugiwa account. Kuna shule huko Arusha The School of St Jude imefungiwa na yenyewe.
 
Na kweli katika kipindi hiki kigumu inakuwaje unapata hela kuliko sisi?
Wewe hata uwezo wa kununua computer ya laki 4 huna sishangai unachukia wenye hela, utashangaa wamekuja kumuoa mama yako.






 
Back
Top Bottom